Sunday, May 8, 2011

MICHEWENI PEMBA WANAUMIYA NA NJAA JE MUUNGANO UKO WAPI..????


hizi kweli ni sura za kuonyesha kuwa wanawajali watuwanao teseka na njaa pemba..?

muungano mbona pemba watu wanaumiya na njaa...?

faida za muungano ndio hizi

huffffffffffffffff
Micheweni ni mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi ambapo hivi sasa njaa imetamalaki huku mifugo nayo ikikosa malisho na maji. Ukosefu wa mvua umesababisha ukame katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya mashariki ya kisiwa cha Pemba. Kwa ujumla, hali ya maisha ya watu wa Micheweni inasononesha huku wanaosononeka zaidi ni kinamama na watoto.
Mengi ya mabonde yamekauka huku mpunga uliopandwa ukinyauka, mtama na uwele, mazao ambao ndiyo chanzo cha kipato kwa wilaya hiyo Micheweni kikiwa kimeathirika kutokana na ukavu wa ardhi uliotanda huku migomba, muhogo nayo ikiwa imeungua kutokana na ukame.
Itakumbukwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa wilaya hiyo kukumbwa na njaa kwani ni miaka ya hivi karibuni iliripotiwa watu kula mizizi kama chakula kiitwacho Chochoni ambacho ni hatari kwa lishe ya binadamu kutokana na kuwa na sumu , lakini Waswahili husema, lisilo budu hutendwa, hivyo wananchi wa Micheweni huwa chakula hicho kutokana na ukame ulioyakumba maeneo yao.
Wilaya ya Micheweni iliyopo Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002 ilikuwa na wakaazi 83,531 ikiwa imejaliwa kuwa na utajiri mkubwa wa samaki aina mbalimbali pamoja na kuwa na mifugo. Shughuli kubwa ya watu wa wilaya hiyo ni ufugaji na uvuvi.
Hali ya ukame imesababisha mifugo pia kuathirika kwa njaa, hivi sasa Micheweni watu huwapitia mbali ng’ombe na mbuzi maana wamechongeka (kukonda) kutokana na ukali wa njaa na ukosefu wa maji. Kwa muda wa miezi mitano sasa baada ya eneo kubwa la mashamba ya wakulima kuonekana kutokuwa na uzalishaji wa chakula cha aina yoyote kutokana na hali ya hewa ya jua kali (kiangazi) inayoikabili Micheweni miti kadhaa imeonekana kukauka.
Akizunguma na wananchi wa Micheweni katika ziara yake, Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi, alishuhudia hali halisi ya ukavu wa ardhi na ukosefu wa chakula unaowakabili wananchi wengi wa vijiji hivyo na hutaka hatua za haraka zichukuliwe ili kukabiliana na tatizo hilo.
Licha ya viongozi wa Serikali kuwatembelea watu wa Wilaya hiyo,lakini ni muda mrefu sasa tangu walipotembelewa hakuna mabadiliko yaliyotokea na watu wanaendelea kuteseka, lakini kauli za kisiasa zinazotolewa kwamba serikali itahakikisha hakuna mtu atakayekufa njaa, kwa upande wao wananchi wanaeleza kuwa wanalazimika kuishi kwa mlo mmoja kwa siku.
Watu karibu 7,000 wanakabiliwa na njaa huko Micheweni huku kiwango cha umaskini kikizidi licha ya kuanzishwa kwa radio jamii katika kusaidia kuinua uchumi wa Wilaya hiyo.
Hivi karibuni, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la umoja wa mataifa(FAO), Louise Setshwaelo alielezea umuhimu wa uhakika wa chakula kwa jamii akisisitiza kuwepo kwa mkakati madhubuti katika kile alichokiita hatua za kukabiliana na uhaba wa chakula.
Mwakilishi huyo ameihakikishia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kwamba FAO itatoa kila aina ya msukumo kuisaidia kufikia malengo yake ikiwa pamoja na kushawishi Washirika wa maendeleo kuendelea kuisaidia hasa katika uhakika wa chakula na lishe.
Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mansoor Yussuf Himid anasema SMZ ilitarajia kuwasilisha katika Baraza la Wawakilishi muswada wa sheria wa uhakika wa chakula na lishe katika kikao cha mwezi uliopita (Aprili).
Akizungumzia mkakati wa SMZ kuhusu uhakika wa chakula, Waziri Mansoor anasema uhakika wa chakula na lishe bora ni jambo linalopewa umuhimu wa juu na ndio maana Serikali iliandaa muswada huo wa sheria ambapo pia katika sheria hiyo imependekezwa kuwepo kwa Ghala la Taifa la Akiba ya Chakuka Zanzibar.
Mansor anakiri kwa sasa hali ya chakula Zanzibar sio nzuri kwani umaskini wa chakula kwa wananchi ni asilimia 13. “Hapa kwetu umaskini wa chakula umefikia asilimia 13, Wizara yangu imejikita katika kuona kwamba tutaondoka katika hali hiyo,” anasema Mansoor
Waziri Mansoor anasema kwamba mpango mkakati wa SMZ kwa sasa ni kuwa na uhakika wa chakula na kuongeza kasi ya uzalishaji ili sehemu kubwa ya chakula kizalishwe hapa nchini na kupunguza uagiziaji.
Kwa hakika, mabadiliko ya tabianchi yanaiathiri Zanzibar ambapo kwa kawaida mvua za kupandia zinanyesha kati ya Desemba hadi Machi, lakini mwaka huu huu licha ya wakulima kuburuga (kuandaa) mashamba yao,hakuna mvua iliyonyesha.
Wakati Serikali ikiwa katika mkakati huo, ni vyema ikachukua hatua za haraka kuwasaidia watu wa Micheweni kupunguza ukali wa maisha na hususan njaa inayowakabili.
vunja mifupa kama bado meno yapo

2 comments:

  1. Dancing president? Lahaula Walakwata. Nchi anayoongoza huyu, itakuwa na maendeleo kweli?

    ReplyDelete
  2. mabadiliko yanahijaka!Tunahitaji tupate vijana ambao watakuwa tayari kujitolea kuleta mabadiliko katika taifa lao.

    ReplyDelete