Wednesday, May 4, 2011

KAMATI 49 ZILIZO UNDWA KUTATUWA KERO ZA MUUNGANO HAKUNA HATA MOJA ILIYOFANIKIWA NA HAKUNA HATA MOJA ABAYO MZANZIBAR YUMO NDANI JE KERO ZA MUUNGANO KWELI SITAONDOKA...?


mzalendo_aliseifiddbalozi
Kwanza nitakuulizeni swali: je, nani aliyewahi kusoma kile kitabu cha Bwana MSA kinachoitwa Siri ya Sufuri?
Imani yangu ni kuwa wengi mmewahi kukisoma na kukifahamu.Vitabu hivi vimekwua adimu sana hapa Zanzibar.
Mada yangu yangu italenga hapo, na itakuwa na vichekesho kidogo.
Unajua records zinaonyesha kuwa tokea umeanishwa Muungano 1964, zimeundwa kamati 46 kwa ajili ya kutatua kile kinachoitwa ‘kero za muungano’.
Kati ya hizi 49 hata moja hakuna iliyoongozwa na Mzanzibari; si mwenyekiti au katibu au angalau makamo mwenyekiti (Muungano Oyee).
* Kati ya hizi 46/49 — hakuna hata moja iliyoweza kutatua hata tatizo moja dogo tu linaloleta switilfahamu ya mahusiano yetu na Tanganyika. Zaidi, kama litatajwa tatizo katika vikao, ndio wenzetu wanakwenda kulikuza na kuwa kubwa zaidi, na kama ilikuwa litatute, basi ndio linakwama zaidi na kuselelea.
* Angalia siri ya sufuri inavyofanya kazi: Mzanzibari kusema kuwa anataka serikali tatu (mbili kuelekea ttau, inakuwa ni kosa kubwa la jinai) na anammabiwa anataka kuvunja Muungano. Atakayesema kama atakuwa Jumbe au Salmin au Seif Shariff Hamad, yeyote yule so long atakuwa ni Mzanzibari, basi hilo ni kosa la jinai/uhaini. Lakini akiwa ni Mzanzibari. Na ajabu ni kuwa Wazanzibari wote awe CCM au CUF; basi conciiously/naturally, atasema hivyo. Sijui kwa nini.
* Mtanganyika, akiwa Pinda au Mkapa, akisema kuwa wanataka serikali moja (mbili kwenda moja) si tatizo, wala hataki kuvunja Muungano. In fact, anapigiwa kofi na vigelele eti anataka kuimarisha Muungano. Na ajabu ni kuwa hakuna Mtanganyika anayteleza, conciussly/naturally, anayesema mbili kwenda tatu. It is OK two to ONE; but it is not OK two goes to THREE.
* Mnakumbuka ile hesabu ya 1+1 = 3. Nimejaribu sana kuitafuta theory hii tokea mwaka 1983, ni theory gani katika math…….!sijaipata jawabu yake. Lakini kimantiki ya Muungano/Msuguano wetu baina ya Tanganyika-Zanzibar; ni hesabu ya kweli kabisa.
* Kama Mzanzibari atauliza zile one milion pounds za kiingereza walizotoa Zanzibar kufanya central bank ya Tanzania (BOT) ziko wapi, na share holding yake iko wapi, au sisi Zanzibar tunasimimia wapi: jawabu unaambiwa kuwa ‘suirejeshe ya nyuma’. lakini hii ni haki yetu tokea 1967; ni mgao tuliopokea from EAC, ambayo Zanzibar ilikuwa mbele sana kulipa katika jumuiya kuliko hata Tanganyika — siri ya sufuri hiyo.
* Inasikitisha sana kuona kuwa bidhaa kutoka Zanzibar na hasa zile zinazozalishwa Zanzibar mpaka leo zinatozwa kodi mbili kinyume na hata taratibu za EAC tearty/protocol ya common market. Haya nilidhani akina Bi.Samia na Mahadhi au Pereira wa Wizara ya fedha watayazungumza na kuyatekeleza. Lakini leo tunaona Bi.Samia anataka mafuta yatayochimbwa mwambao wa Kizimkzai (kwao) na pemba n.k yaingie moja kw amoja katika mfumo wa wafalme wetu. yeye ataambuliwa kulipwa mshahara na kupanda Prado VX, na kuongezewa walinzi tu. Hii ndio fakhari yake na fakhari yao.
*Siri ya Sufuri: unanua kwa nini Zanzibar haitakiwi kujiunga na OIC? Katika tearty ya Union ya 1964,tuliungana katika “Mambo ya Nchi za Nje”; lakini limeongezwa neno ‘ Na Ushirikiano wa Kimataifa”. Kwa hivyo, kutokana na mantiki hiyo, ndio Zanzibar haiwezi kujiunga tena na OIC. Hii ‘na ushirikiano wa kimataifa’ imeingizwa juzi na JK, alipokuwa Foreign Minister (“Muislamu mwenzetu”).
- Yeye aliahidi Zanzibar au TZ itajiunga, lakini yeyey-yeye ndiye aliye complicate kila kitu. Wallah hatuyeshi — siri ya sufuri hiyo. Nchi kama Mozambique, Cameroon, na Uganda wana asilimia kidogo ya waislamu, lakini wamejiunga na OIC, Zanzibar au TZ haiwezekani, wafalme hawataki.
* Juzi yupo mchangiaji mmoja ananiuliza eti ni kipi kikubwa walichonacho Zanzibar zaidi ya hayo maji ya drop (someni ile mchango wake). Sasa mimi ninachotaka kumwambia ni kuwa – kweli kuna kiwanda kimoja tu cha drop; lakini hiyo imetokana na sera zao kuwa wametunyonyoa mpaka mbawa, hatuwezi tena kuruka.
Na kila investor anayekuja kutaka kuwekeza katika kiwanda anashindwa njaini hata kabla ya kuanza kazi. Raza ameshindwa hata kuzalisha sabuni ya chokaa.
Lakini kumbuka kuwa sisi tulikuwa giants tena sana. Soma historia ya Mercedez Benz. Utaona kuwa moja ya composition yake, enzi hizo, walikuwa wanatumia usumba kutoka Zanzibar, kutengeneza viti. Je, hilo dogo. Kwa nini wainunu katani kutoka Tanganyika na ilikuwepo? Lakini akutukanaye hakuchagulii tusi. Isotoshe waulizeni TRA wapi katika mikoa ya TZ wanakusanya fedha nyingi zaidi, kama sio Zanzibar. Kweli hatuna kitu, lakini hatujakuwa mafukara kiasi hicho. Tulikuwa na usumba, mafuta ya nazi, na Zanzibar ukisoma vziuri ndio ilikuwa centre of trading/business kwa afrika mashariki na kati. Tanganyika wlaipiga marufuku kuuza pembe za tembo/ndovu – Zanzibar ilikuwa rukhsa …huria. hiyo ndio historia yetu. leo tumenyonyolewa mpaka mbawa, hatuwezi tena kuruka.Tumekuwa kama kuku boi tu.
* Sisi Zanzibar mara ngapi tumeiokoa (bail out) Tanganyika kifedha. Tumetoa mpaka mishahara kuwalipia wafanyakazi wa Tanganyika (muulize Taimur Saleh) aliyekuwa waziri wa fedha Zanzibar. Mwisho alikataa kutoa 50,000 dollars kuwasaidia Tanganyika enzi za Jumbe, then, wakahitilafiana. Records zipo bado. Leo 50,000 utaziona kidogo, lakini miaka ya 70s na 80s zilikuwa nyingi sana.
* Zanzibar imeweza kuibeba Tanganyika katika vita vya vya Uganada financially, na vifaa vya kiejshi. Tulitumia meli zetu MV.Mapinduzi, Maendeleo kusaidia Nyerere katika vita vyake vya kusini mwa Afrika, Mozambique, Angola na Namibia. mwisho meli yetu ya M.V mapinduzi ilitaka kupigwa na makaburu. Smart captain wa kizanzibari walipata fununu na haraka sana walikwenda kupachua bendera ya TZ, na kuiweka ya Zanzibar chap chap. hapo ndio tuli-save. Tunayajua mengi, lakini hatutaki kuropokwa sana tu.
Sasa, naomba mnieleze ni vipi hizo kamati 46 au 49 za Muungano zilizoundwa kutatua kero zimefanya kazi vipi, na limetatuliwa lipi na kwa wakati gani

No comments:

Post a Comment