Monday, June 20, 2011

DR SHEIN ASEMA DAWA YA MFUMUKO WA BEI ZA VYAKULA NI KUANZISHA KILIMO CHETU WENYEWE


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (SMZ), Dk. Ali Mohamed Shein ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mlezi wa Mkoa wa Mjini Magharibi amesema kuwa dawa ya mfumko wa bei ni kuimarisha sekta ya kilimo na kuzalisha kwa wingi vyakula vinavyotumiwa sana na wananchi nchini.
Dk. Shein ameyasema hayo leokatika ukumbi wa Tawi la CCM Kiembesamaki wakati alipokuwa akizungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya ya Magharibi ikiwa ni mfululizo wa utaratibu wake wa kuzungumza na viongozi wa CCM wa Wilaya zote za Unguja na Pemba.
Kutokana na hatua hiyo, amesema , SMZ imeshaanza mikakati ya kuiimarisha sekta hiyo ya kilimo ikiwa ni pamoja na kuendeleza kilimo cha mpunga hasa cha umwagiliaji maji sambamba na kuweka fedha nyingi katika kilimo ili kukuza zao hilo pamoja na kujitosheleza kwa chakula.
Amesisitiza kuwa, na mazao mengine nayo yataimarisha likiwemo zao la muhogo, mtama, mahindi na mengineyo.
Akizungumzia zaidi uimarishaji wa sekta ya kilimo, Dk. Shein amesema, kituo cha Utafiti cha Kizimbani ambacho ndiyo cha mwanzo cha Afrika Mashariki na amekipandisha kutoka kituo kuwa Taasisi hiyo ni kutokana na kazi kubwa ya kituo hicho.
Amesema, miongozi mwa kazi kubwa inayofanywa na kituo hicho ni pamoja na kuanzisha utafiti wa mbegu mpya ya mpunga ya NERIKA ambayo tayari imeshapandwa heka tano za mbegu na baada ya hapo watapewa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa kuazia heka 100 na baadaye kwa wakulima wote na hivi sasa linaandaliwa bonde la Kibondemzungu kwa ajili ya kilimo cha mpunga.
Serikali imeamua kufanya mapinduzi ya kilimo, na kuahidi kuimarisha kilimo cha kisasa na umwagiliaji, mbegu bora, mbole na kuongeza matrekta, akisema tayari serikali imeagiza matrekta 50.

haya sasa tuombe m/mungu yatekelezwe maana yamesemwa mengi sana na hayo matrekta na wapewe hao rai ili wapungukiwe na kulima kwa majembe maana ndio yanayowazeesha hayo majembe na mashoka na mapanga ulimaji huo umepitwa na wakati sasa mambo ya kilimo ni tekenologia tuu utaona mkulima nchi za wenzetu kava suti hapa kwetu kama aliyetapikwa na chatu sio sawa kabisa nawapewa vitu kama hivi kisha wauzo mazao ya na kuilipa serekali wao watafaidika na serekali pia.
oneni jinsi watu wanavyo lima na kuitunza ardhi na wenzetu hawana ardhi kama yetu ni nzuuri zaidi na baraka kibao sisi tujifunze ukulima kama huu ndio fiti safi na ardhi imetulia kabisa
cheki mambo haya wakulima wa znz wapewe kama haya
haya ni makrekta yanamwagia maji je vijana wangapi watapata ajiri ikiwa
serekali yatu itanzisha haya sio kuiba na kujaza matumbo yao
oneni mambo vijana wote watapata kazi za kufanya na asiyetaka kufanya
basi huyo anawalakini .
hakuna jembe wala panga wala shoka mijekrekta tu ndio
inayo fanya kazi hata mtu mwenyewe anaona raha kufanya kazi
kilimo bora mazao bora

No comments:

Post a Comment