Monday, June 20, 2011

KIWANDA CHA NDIMU KINATAKA KUJENGWA KTK NCHI YA ZANZIBAR




TUOMBE M/MUNGU AJALIYE KIJENGWA NA WANAKIJIJI NDIO WAJERIWE KTK KIWANDA HICHO SIO ILETWE MIJITU MENGINE KUTOKA WAPI SIJUWI NA WAZENJI WENYEWE HAWANA KAZI YA KUFANYA.

JUMUIYA ya kukuza na kuendeleza wakulima wa ndimu Zanzibar katika eneo la Chwaka wapo katika hatua za mwisho za kujenga kiwanda cha kusindika zao hilo.
Mmoja ya wanachama wa jumuiya hiyo, Adam Muhsin alitoa taarifa hiyo wakati alipozungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kati, Maalim Ali Kassim aliyetembelea jumuiya hiyo.
Alisema, wameshapata baraka kutoka kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo Shirika Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) ambalo limekuwa mstari wa mbele kuwasaidia ikiwemo kuwapatia ushauri wa kitaalamu.
“Tupo katika hatua za mwisho za kujenga kiwanda cha kusindika bidhaa ya ndimu ambazo kwa sasa zinazalishwa kwa wingi kiasi cha kukosa soko,” alisema Muhsin. Alisema wakulima chini ya jumuiya hiyo, wanazalisha jumla ya tani 3,500 za ndimu ambazo zinakosa soko na kuharibika bure.
Muhsin alisema, UNIDO limewasaidia kuwapatia ushauri wa kitaalamu katika kujenga kiwanda hicho pamoja na kuwapatia mashine.
Kiwanda hicho kitakachogharimu Sh milioni 56 kitakuwa na uwezo wa kusindika ndimu kwa ajili ya matumizi mbali mbali.
Mkuu wa Wilaya ya Kati aliwapongeza wakulima wa ndimu katika wilaya hiyo kwa juhudi zao ikiwemo mpango wa kujenga kiwanda.
Alisema, “Serikali imefurahishwa na juhudi zenu pamoja na uamuzi wa kujenga kiwanda cha kusindika ndimu…ni uamuzi sahihi kabisa ambao utaongeza ari na motisha ya wakulima wa ndimu,” alisema Kassim. Wakulima wa ndimu katika Wilaya ya Kati kwa sasa wanalima zaidi ya hekta 4,500.

No comments:

Post a Comment