ZANZIBAR HAINA SHERIA YA UCHIMBAJI MAFUTALICHA ya Zanzibar kutokuwa na sheria ya kuchimba mafuta wala haiwezi kutoa leseni kwa ajili ya kazi hizo, Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijaizuilia Zanzibar kuchimba mafuta yake.
Sheria iliopo hivi sasa ya kuchimba mafuta ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar inataka suala la mafuta liondolewe katika mambo yaliopo katika orodha ya mambo ya Muungano.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo Zanzibar, Omar Yussuf Mzee ameliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akifanya majumuisho na kujibu hoja mbali mbali za bajeti yake katika kikao kinachoendelea huko Chukwani Mjini Unguja.
“Waheshimiwa wajumbe Zanzibar haijazuwiliwa kuchimba mafuta yake lakini tatizo hadi sasa hakuna sheria ya kuchimba mafuta….sheria iliopo ni ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kama tukichimba basi mafuta hayo yatakuwa pamoja na Muungano hayatakuwa peke yetu” alisema Mzee.
Mzee alilazimika kutoa ufafanuzi wa kina katika suala la mafuta na gesi kufuatia wajumbe wengi waliochangia bajeti ya serikali kulalamika kwamba serikali haijaeleza lolote kuhusu suala la mafuta na gesi ambalo tayari limeamuliwa na baraza la wawakilishi kwamba liondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano.
Asilimia 70% ya wajumbe wa baraza la wawakilishi waliochangia bajeti ya serikali kwa mwaka 2011-2012 walizungumzia suala la mafuta na kuitaka serikali haraka kuharakisha mipango ya uchimbaji wa nishati hiyo ambayo kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba mafuta yapo pamoja na gesi katika mwambao wa visiwa vya Unguja na Pemba.
“Mafuta ni sehemu ya uchumi wa Zanzibar na mambo ya uchumi wa Zanzibar hayamo katika mambo ya Muungano hivyo wawakilishi kutaka suala la mafuta litolewe katika mambo ya Muungano ni sahihi”alisema Waziri Mzee.
Alisema suala la mafuta zipo sehemu ya alama nne zinazoonesha kuwepo kwa mafuta, ambapo tayari yapo makampuni mbali mbali kutoka Uingereza, Urusi na Brazil wameonesha nia hapa nchini kwa ajili ya kazi za uchimbaji mafuta.
Hata hivyo alisema wawekezaji watakaokuja kuchimba mafuta watahitaji kupatiwa leseni za kazi za uchimbaji ambapo hutolewa na jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa sababu Zanzibar haina sheria ya mamlaka ya kuchimba mafuta.
“Waheshimiwa wajumbe tukiamuwa leo tunataka kuchimba mafuta basi tunaweza kufanya hivyo…lakini je tujiulize sheria ya kuchimba mafuta tunayo? Na jee utoaji wa leseni? Alihoji waziri huyo.
Alisema inawezekana kuamuwa kuchimba mafuta sasa kwa kushirikiana na muungano au kusubiri hadi kukamilika kwa taratibu za kuliondowa suala hilo katika orodha ya mambo ya Muungano.
Waziri huyo alisema Zanzibar inataka kuliondowa suala la mafuta katika orodha ya mambo ya muungano ni kulipeleka suala hilo bungeni na huko kufuata taratibu zake kwa kupigiwa kura na wajumbe wa bunge la Jamhuri ya Muungano.
Hata hivyo Mzee alisema suala la kuondoshwa mafuta katika orodha ya mambo ya muungano linahitaji nia njema na kupata baraka kutoka kwa rais Jakaya Kikwete akishirikiana na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Sheni tu.
“Waheshimiwa wajumbe wenzangu hili ni suala la kuwepo kwa nia njema kwa viongozi wetu mheshimiwa Rais Kikwete na mheshimiwa rais Dk Shein” alisema waziri huyo.
Akizungumzia suala la kujikwamua na uchumi alisema serikali ya Zanzibar imeweka kipaumbele katika sekta ya uwekezaji ikiwemo ya viwanda kama mkombozi na kuongeza ajira kwa wananchi wake.
Alisema hadi sasa mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa ni mdogo sana hivyo mkazo utawekwa katika kuwekeza viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia kuongeza ajira na sekta ya uzalishaji wa vyakula.
Katika kuimarisha dhana ya utawala bora alisema serikali imo katika hatua za kutayarisha sheria ya viongozi kutangaza mali zao ikiwa ni sehemu ya kuimarisha dhana ya utawala bora.
Alisema baadhi ya viongozi waliomo katika baraza la wawakilishi tayari wametangaza mali zao kupitia bunge la jamhuri ya muungano ambalo linao utaratibu kama huo wa kutangaza mali za wajumbe na viongozi wa serikali.
“Mheshimiwa spika mimi tayari nimetangaza mali zangu kule bungeni…..hapa yupo makamo wa pili wa rais balozi Seif Ali Iddi amefanya hivyo pamoja na waziri Haroun na Fatma Fereji na wengine” alisema.
Waziri huyo alisema katika kusimamia maadili ya viongozi waziri mwenye dhamana ya waziri wa nchi afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame afanye iwezekavyo apeleke haraka sheria ya kutangaza mali za viongozi ambazo wazoefu wapo wataweza kumsaidia katika suala hilo.
“Kiongozi aliechuma mali kwa nguvu zake hawezi kuongopa kutangaza mali zake mheshimiwa Spika”.alisema Mzee.
Waziri huyo akifafanua bajeti hiyo kwa wajumbe alisema sekta ya viwanda inahitaji kupewa msukumo mkubwa kwa sababu ili nchi iweze kukua uchumi ambapo nchi nyigi duniani zenye viwanda zimefanikiwa kukua uchumi wake kwani kila mwaka hupanda kwa kiasi kikubwa.
Alisema mbali ya viwanda lakini nguvu ielekezwe ndani ya ufugaji uvuvi na kilimo cha mboga mboga kwani hivi sasa mahoteli yaliopo Zanzibar yanaagiza mboga mboga kuto nje ya Zanzibar hivyo alielekeza wananchi kujikita zaidi katika kilimo na mboga mboga.
Wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa kauli moja wamepitisha bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
ZNZ haina sheria ya kuchimba mafuta na ikichimba basi mafuta hayo yatakuwa ya shirika pamoja na watanganyika.unazungumza kama uko chooni mzee sasa kama znz haina vipi tanganyika wameweza kujichamba gasi yao na tanzanight zao na thahabu zao na znz haikupata kitu....? umewashika wenzako waeleze mali zao na wewe ushaeleza bungeni dodoma kwani wewe umechanguliwa dodoma au znz..? kama ni kueleza mali zako eleza hapa hapa baraza la wawakilishi.unawabana wanzako ili waogope wasisemetena kuhusu mafuta sio...?na kunuku(( kupata baraka kutoka kwa rais Jakaya Kikwete))kwani kikwete ni nani mtume..?sahaba..?m/mungu..?mbona munakufuru ati baraka anaye towa baraka ni SUBUHANA WATAALA peke yake mzee kama hujuwi nakujulisha acheni kufuru. sisi rai tunawajuwa kama nyote ni wezi nyote humo baraza la wawakilishi ila kinacho tuma sisi ni kwanini kila kitu mpaka tanganyika waseme ndio znz ifanya mumekuwa kama (hawara wa tanganyika)au (kidampa wa tanganyika)au ((kinuka mkojo cha watanganyika))au ((kibarathuli cha watanganyika))((kichangu dowa chawatanganyika))hao watanganyika wakisiki munavyosema wanawacheka wanaona hao vinuka mkojo vinatetemeka. watu washasema zamani hawataki muungano sasa kama ni leseni ya kuchimba mafuta tutanunuwa nchi za nje kwisha musitulete sijuwi tang kinyoko vile wala kinyoka hivi.
No comments:
Post a Comment