Kuanzia jana wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wanaoagiza biashara kutoka nje ya nchi (importers) wamegoma kwenda kutoa mizigo yao hapo bandarini Zanzibar.
Sababu: USHURU MKUBWA USIOTARAJIWA UNAOTOZWA NA TRA. NI USHURU WA KUKOMOA, KUWAKOMOA WAZANZIBARI.
Athari ya suala hili, ubabe wa TRA kwa Wazanzibari, ni nyingi, kupanda kwa bei ya vitu, usumbufu wa wafanyabiashara na dhahir, ubabe, kiburi dhidi ya Zanzibar. Tutakuwa hivi mpaka lini?
Tumekaa kimya tunaumia. Tunazungumza BLW kama vile chiriku, hakuna ACTION. TRA imetakiwa kuondoka Zanzibar,kwa nini haijaondoka mpaka leo..? hizi ni dalili kuwa zanzibar tunatawaliwa na mkoloni mweusi tanganyika maana kama hawatutawali walipoambiwa waondoke basi wangeliondoka. na SMZ haijasema kitu maana hakuna WA KUSEMA YOTE MAJOGA. TRA imezuia mizigo ya Zanzibar katika bandari ya Zanzibar – ndani ya nchi yatu ya ZANZIBAR mizingo imezuiliwa na TRA ambayo ni ya tanganyika nani nchi yetu wenyewe wazanzibar na mizingo imezuwiwa mpaka walipe ushuru waliyo usema TRA ambao ni kuwakomowa wazanzibar.
Pia imewakomoa Wazanzibari waliopeleka mizigo yao Dar, ikiwemo gari 350 na ushei. TRA hiyo hiyo, imewaandama Wazanzibari wanaofanya biashara DAR; kwa kuwapiga penalty eti hawana ile machine ya TRA — lakini inamuwacha Mchanga aendele na biashara ila wazanzibar wanakula viboko tu sasa mchanga ni‘untouched’.
Swali ninalojiuliza mimi: hivi kweli Rais wa Zanzibar na wenzake hawaweiz kutatua tatizo hilo, ambalo ni tatizo la kutengenezwa?
Miaka ya 92-93, Bara walizuia makontena kiasi 40 ya wafanyabiashara wa Zanzibar. Dr.Salmin, aliyekuwa Rais wa Zanzibar alimuita Kighoma Malima, siku zile alikuwa waziri wa fedha. Na hakutaka story nyingi, alichomwambia ni kuwa ‘ninataka makontena yote ya Zanzibar yatolewe na yafike Zanzibar mara moja”. Naam… within 24 hrs makontena yalifika Zanzibar na hakuna maneno tena kama kasuku.
Leo, tunakuwa na MARAISI WATATU SHEIN,SEIF,IDDI –
na wote ni bogus, hawawezi hata kusema ‘weeeeee’ au ‘nyaamaniiiii’…….wamekuwa MAKOKO
na wote ni bogus, hawawezi hata kusema ‘weeeeee’ au ‘nyaamaniiiii’…….wamekuwa MAKOKO
Tumefika hadi kupiga kelele tu BLW. Wawakilishi wetu wanasema utadhani chiriku, lakini kazi bure. Kama nilivyosema hapo awali, kuwa BLW si chochote si lolote.
Jana wawakilishi wenyewe walisema hilo. Walisema kuwa suala la mafuta limeshaamuliwa na BLW, chombo cha juu kwa Zanzibar cha kutunga sheria.
Balozi Seif Ali Iddi, kinyemela (au kimya kimya) ameliingiza suala la mafuta katika list ya ‘kero za muungano’. Huko litajadiliwa tena na WAFALME WETU. Yaani hukumu imeshatoka, Balozi iddi analibatilisha na kulipeleka kwa jamaa zake kupata barka zaidi. Sasa, kwa nini BLW lipo...? HAPA ZANZIBAR BASI BORA LIFUNGWE TUWE NA DODOMA TU KAMA ALIVYOTA PINDA PINDUWA.
Naye Dr.Shein anazunguka visiwa vyote anatetea mfumko wa bei, anadanganya watu eti hali hiyo ni dunia nzima. Hataki kusema kuwa TRA ndio chanzo cha kuwa na maisha mazito na ya taklifu hapa Zanzibar.
Jamani eee….muda wa kupiga maneno umekwisha. Tunataka vitendo.
Issues kubwa katika BLW ya mwaka huu ni TRA na uchimbaji wa mafuta ya Zanzibar, na of course, katiba mpya
ambayo Mizengo Pinda ameshasema kuwa by 2014, TZ itakuwa na katiba mpya (mtake – msitake).Kama mtasema, mtalia, mtapayuka, mtachana rasimu, mtaitia moto – ndio hivyo hivyo — USHINDI LAZIMA. Na kupitia kwa vibaraka wetu wa Zanzibar, tayari wameshakubali kuipitisha rasimu hiyo – wakiongozwa na CCM-CUF- hapa Zanzibar, chini ya kivuli cha GNU.JE BADO TU WAZANZIBAR TUNAHITAJI KAMUSI NDIO TUJUWE KAMA HAWA WATANGANYIKA WANATAKA KUTUMALIZA?
No comments:
Post a Comment