kama mnataka thulma isimame warudishiyeni wenye
haki wa nyumba za mji mkongwe wajuku wao wahai
la kama munataka kuendeleya na haramu sawa.
Najuwa wengi wenu hamutakubali na wengine watasema tunataka kumrudisha sultani.au hata kuropokwa bila ya maana ila kabla hujaropoka na kusema maneno ya ajabu.jiulize wewe ni muslamu..?kama ndio je unakula halali..?kama ndio je nyumba unayo ishi ni yahalali..?kama ndio basi alahamdulilahi kama sivyo basi hapo ndipo penye mtihani na nibora ukaji sahihisha kabla hujenda mbele ya haki.kwa nini nikasema hivyo nikuwa sote tuliyo unguja na pemba tunaelewa ni nini kilicho tokeya 1964 ikiwa wazee hawakukuambia basi umesoma kwenye vitabu n.k.
sasa ikiwa nyumba unayoishi ni ya haramu,mshahara unaopokeya ni waharamu,basi chakula unachokula ni cha haramu.sasa ikiwa kuanzia asubuhi mpaka usiku unarudi kitandani ni haramu tupu je kweli tutafika..?watu wengi walifukuzwa kwenye nyumba zao,mashamba yao na wengine kuliwa haswa na mali zao kuchukuliwa.kisha serekali ikawapa watu waliosema ni masikini 1964 sasa miaka imekwenda na miaka rundi sasa serekali inawanyanganya hao masikini waliyo pewa na kuwauzia matajiri na hao matajiri kujenga hotel za kitali wewe utalalamika wananifukuza ndio shukuru kuwa hawakukuwa kama walivyo wauwa watu 1964 kwani nyumba unayo ishi wewe kuna watu waliyo ijenga kwa jasho lao na walifukuzwa na mukapewa nyinyi sasa nyinyi pia munafukuzwa.
ndio nikasema haramu haitafutika itaendeleya kuwa haramu mpaka waliyo thulumiwa warejeshewe au walipwe au wasamehe la sivyo kila baada ya miaka kumi akija raisi mpya atakuja na thulma yake na ubabe wake kama kweli znz tunataka kuishi kwa salama na amani na utulivu basi waliyo thulumiwa walipwe au warejeshewe au waulizwe kama wamesamehe ili wewe unaishi ktk nyumba ile au shemba lile iwe ni halali kwako wengi mnajuwa fika kama nyumba munazo ishi sio zenu wala mashamba munayo lima sio yanu na nyinyi ni waislamu na kufunga ramadhani na kuswali swala tano wapi na nyinyi munajuwa nyumba unayoishi ni ya thulma shamba unalolima chakula ni la dhulma kwa hiyo ni kama unaye chota maji na chujio la nazi unachota lakini yanavuja chini na ndio maana 1964 yaliyo tokea hayajaishia hapo mpaka leo yanaendeleya ila kwa njia tafauti lakini ndio thulma ile lile hivi sasa.
Kuna habari za kutatanisha juu ya kudata nyumba ya ofisi ya wizara ya kilimo (sehemu ya utafiti) iliyopo Forodhani (nyuma na skuli ya Forodhani). Siku ya Ijumaa nyumba hii ilisikika ‘ikidata’ na wafanyakazi wametoka nje wote. Ghafla moja, tayari kuna habari kuwa serikali imetaka nyumba hiyo wafanyakazi wahame mara moja maana ni ‘hatari kukaa watu’.
Sasa, kinachoendelea siku hizi hapa Zanzibar, ni kuwa kama nyumba ya mji mkongwe inatakiwa na mwekezaji au serikali inataka kuiuza basi rule no.1 inadatishwa ili ionekane kuwa ni mbovu na haifai kukaa watu thulma hiyo. Haya na kama haya yameshafanyika, kuihujumu nyumba ili kuruhusu ujenzi wa hoteli na kumruhusu mwekezaji kuweka vinyago au kufanya bar au parlour au ‘sex tourism’. Mifano ipo…miiiiingi tu.
Katika eneo hili la nyumba iliyodata (ofisi ya idara ya kilimo) tayari pembeni kwake ipo hoteli imejengwa. na usoni kwake ipo hoteli inayoitwa ‘seyyida hotel’ mmiliki wake inasadikiwa kuwa ni ya mtoto wa Mzee Dr.Amani Karume.1964 john okello aliwafukuza watu mji mkongwe na kulikuwa kutupu kama pori ndio mzee karume akasema ati masikini wa znz wakapewe nyumba hizo haya sasa mjukuu sasa anazitaka nyumba za babu yake je waliyo fukuzwa 1964 wajuku wao wako hawataki nyumba hizo..? thulma juu ya thulma pia Kulia kwa hoteli hii kulikuwa na nyumba wanakaa watu, wametakiwa waheme, na wameshahama siku nyingi – pia inataka kufanywa hoteli.
Nayo nyumba hii pia ‘imedata’. Nyumba iliyopo nyuma ya hizo zote, walikuwa wanaishi watu, kuna habari kuwa wameambia wahame, na evaluation ya mamlaka ya uhifadhi wa amji mkongwe, inasema kuwa ‘nyumba hii imedata’ na haifai kuishi watu.je nyinyi munaoishi ktk nyumba hizo munakumbuka 1964 watu walipofukuzwa na kuliwa ndani ya nyumba hizo na mukapewa nyinyi muliona raha je babu aliwapa mjuku anazichukuwa na kuzifanya hotel je inawauma kutolewa na sio nyumba zenu je wenyewe walio jenga mnafikiri haziwaumi au hawazitaki..?narundia tena thulma thulma ndio hiyo inawafika na nyinyi pia ili muone uchungu wa wale waliyojenga hizo nyumba na wakatolewa.
Kuna kipindi ile wizara ya mawasiliano pia aliitaka bwana mkubwa…….xxxxx; na tuliambiwa kuwa ‘imedata’. na baadhi ya wafanyakazi walihama. Ile pale Shangani, zamani ilikuwa BoT – hii hatukuambiw akuwa ‘imedata’ ila tuliambiwa ni nyumba ya ‘mtu fulani….xxxxx……’ na inataka kufanywa hoteli.
SWALI: KAMA HAIFAI KUISHI WATU AU KUWA OFISI YA SERIKALI, VIPI INAFAA KUWA HOTELI AU BAR AU SEHEMU YA KULETA WANAWAKE WA BARA KUJA KUUZA TUPU ZAO KWA WAZUNGU....?
Hongera Mamlaka ya Mji Mkongwe kwa kuthulumu watu 1964 na sasa munaendeleya kuthulumu hao waliyogaiwa wakati wa 1964, chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, ALHAJI Issa Makarani Sarboko.
Hizi nyumba zinadata kama zilivyodata akili zenu nyinyi viongozi wa zanzibar kwa tamaa ya pesa kuliko utu kisha jioni ikifika munaingia msikitini allah akbari mawe. Hamuwezi kufikiri, hamuwezi kuamua – mumeweka pesa mbele za dhulma, kuwabeba wazungu kama ndio watu wa maana na kujirundikiya mali utafikiri mukifa munakwenda nazo huko akhera kumbe munaziwacha hapa hapa wangapi kama nyinyi washatangulia mbele ya haki sasa hivi nathani wanaomba watoke makaburini waje warudishe mali za thulma walizo wanyanganya watu na kuwaibia wananchi ila wapi wamechelewa.
Fikiria kuwa nusu ya nymba za mji mkongwe tayari zimegeuzwa kuwa ni hoteli, karibu beaches zote za Zanzibar zimekuwa ni sehemu za kitalii. Tena utalii wenyewe na uwekezaji wake ni wizi mtupu maana mume zipata kwa wizi na thuma na munaendeleya na mtindo huwo huwo wa wizi na thulma. Tunakwenda wapi. Ah….haya. Ardhi inauzwa, na mji mkongwe unauzwa…..kinachopatikana kiko wapi???
Shein amemaliza maneno yote, kuwa ‘mali ya serikali au serikali haiwezi kuhojiwa kuuza mali yake’. Pale amepewa Kempinski (eti wananchi wamefungua kesi…keis gani hiyo…..yagujuuuuuuu). Na hapo atapewa nani sijui……na kule atapewa Chicharito. Na kuleeeee Gando, atapewa Messi. Imebaki pale nyuma ya Afrika House (zamani ilikuwa English Club) ile open space ni vizuri kama Alhaji Issa Makarani Sarboko atatafuta mwekezaji haraka sana). Sisi tunapenda maendeleo ya nchi bwana alaaaa, nyie vipi?
Huu ndio utamu wa utawala bora chini ya SMZ. Hakuna kuhoji wala kukubali. Imekuwa kama sheria za uchawini, hata akitolewa mwanao kikoa usiulize wala usilie. Basi hata hiyo ibada ya sala, imamu akikosea, maamuma wanamsaidia……! lakini SMZ yetu… usiulize. Wote wajuba. Leo Shein anathubutu kusema kuwa ‘serikali haiwezi kuhojiwa kwa kuuza chake”. hata kama utakwenda katika mahakama, jaji atasema hivyo hivyo…kuwa ‘uamuzi huu ameshautoa rais wa nchi’ .
Kidumu Chama Cha Mapinduziiii cha cha mapinduziiiii jamani kidumu weee cha chetu cha mapinduzi mapinduzi daima mapinduzi daima mapinduzi daima.
muta thulumu,muta ibaa,muta uwa watu,mutanyanyasa wanyonge na mayatima,mutawatesa wanaosema ukwile au wanakuambiyani ukweli,muta tumiya nguvu za jeshi wakati wa uchanguzi japokuwa munajuwa hamukushinda,na mutaendeleya kula haramu na haramu lakini mwisho wenu ni kifo na munatakuwa ndani ya jeneza kama munavyoliona hapo mbele yenu iko siku ni wewe utakuwa humo ndani ndio utakapojuwa sasa yale mauwaji uliyokuwa ukiamrisha yafanywe na zile thulma ulizo wathulumu watu na uwongozi uliyojipa japo kuwa watu hawakukuchanguwa zote utamueleza allah humo ndani sikwambia nini kitafuatiya nakuwachia wewe mwenyewe uchakachuwe.
HII NDIO NYUMBA
No comments:
Post a Comment