Wizara sita Zanzibar zimekumbwa na kashfa ya kutumia fedha za umma kinyume na sheria ya fedha ya mwaka 2005, ikiwemo kufanya malipo ya mamilioni ya fedha yasiyokuwa na mikataba kinyume.
Kashfa hiyo imebainika katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu (CAG), za serikali Zanzibar ya mwaka 2008/2009 iliyotolewa hivi karibuni mjini hapa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ni kwamba malipo ya sh. milioni 413.6 yalifanyika bila mikataba kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya fedha ya mwaka 2005.
Wizara zilizotumia kiasi hicho cha fedha bila kuwepo mikataba ni Fedha na Uchumi ambayo imetumia milioni 350, iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ ambayo imetumia shilingi million 11.7, wakati Shirika la biashara la Taifa (ZSTC) limetumia sh. milioni 31.8 na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) sh. milioni 20.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ni kwamba malipo ya sh. milioni 413.6 yalifanyika bila mikataba kitendo ambacho ni kinyume na sheria ya fedha ya mwaka 2005.
Wizara zilizotumia kiasi hicho cha fedha bila kuwepo mikataba ni Fedha na Uchumi ambayo imetumia milioni 350, iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ ambayo imetumia shilingi million 11.7, wakati Shirika la biashara la Taifa (ZSTC) limetumia sh. milioni 31.8 na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) sh. milioni 20.
Ripoti hiyo imeeleza pia kwamba Sh. milioni 103.2 zilitumika bila kuwepo stakabadhi kitendo ambacho ni kinyume na kifungu cha 95 (4) cha kanuni za matumizi ya fedha ya mwaka 2005.Ripoti hiyo imebaini baadhi ya Wizara ikiwemo ya Fedha na Uchumi, zimekuwa zikifanya malipo vielelezo vinavyotakiwa kuambatanishwa na hati za malipo kutoka kwa wadai, kitendo ambacho kimesababisha serikali kutumia sh. milioni 138 pamoja na dola za Marekani 94,209, kinyume na taratibu za sheria.
Wizara zilizoshindwa kuonyesha vielelezo vya matumizi ya kiwango hicho cha fedha ni Wizara ya Fedha na Uchumi Zanzibar ambao wametumia sh. milioni 75.5 iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Sh. milioni 15, iliyokuwa Ofisi ya Waziri Kiongozi, Sh. milioni 19.1 pamoja na iliyokuwa Wizara ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, Sh. milioni 5.8.Inaeleza kwamba Sh. milioni 14.2 pamoja na dola za Marekani 35,928 zimetumika bila ya kuwepo vielelezo vya wahusika katika hati za malipo kupitia miradi wakati Sh. milioni 26, ambazo ni fedha za miradi zimetumika bila kuwepo stakabadhi za malipo yake.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Shirika la Utalii Zanzibar (ZTC), limegundulika kumetumika dola za Marekani 7,471 bila ya vielelezo vya matumizi yake.
Kadhalika, vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 29.2 mali ya serikali vimenunuliwa bila ya kuingizwa katika daftari la serikali, jambo ambalo linaviweka kwenye hatari ya kupotea yakiwemo magari.
Wakati huo huo, hoteli ya Kimataifa ya Bwawani, ambayo inamilikiwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), pia imekumbwa na kashfa ya kutoa huduma ya chakula na malazi kwa wageni bure na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha.
CAG katika taarifa yake, alisema kwamba kitendo hicho kimesababisha hasara ya sh. milioni 53 na dola za Marekeani 54,600.Ripoti hiyo imeeleza kwamba wageni wengi walipata huduma bure wakitumia vibali vya msamaha vinavyotelewa na viongozi, (Complimentary).
Akizungumza na Nipashe mjini Zanzibar juzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali Zanzibar, Fatma Mohammed Said, alisema baada ya ripoti hiyo kukabidhiwa serekalini hatua inayofuata ni kuona vitendo hivyo vinadhibitiwa kwa sababu vinakwenda kinyume na sheria na misingi ya utawala bora.
Alisema tangu kuanzishwa kwa Ofisi hiyo mafanikio yameanza kuonekana katika kudhibiti vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma hususani tatizo sugu la mishahara hewa kwa watumishi wa serikali.
Ripoti hiyo imekuja huku Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi (BLW), wakiwa katika matayalisho ya kikao cha bajeti ya kwanza ya serikali ya umoja wa kitaifa (GNU) kinachotarajiwa kuanza Juni 15 mjini Zanzibar
HIzi wiza sita na mawaziri wake na watendaji wake wote wanatakiwa washatakiwe na wapelekwe mahakamani. na walipe pesa zote walizo ibaa na kama hawana basi watumikiye kifungu jela.maana wao wanakula mishahara yao na wanaibiya serekali ambazo hizo pesa zilitakiwa ziwafikiye wananchi waliyo taabani wao wanaiba tu mpaka nyengine wamegeuza ni karatasi za kufutiya vinyesi vyao chooni.sasa serekali mpya ya GNU-SUKARI na iwashatki wote laa sivyo tutajuwa kuwa nyote mumo ktk njia moja wezi wakubwa
No comments:
Post a Comment