MIAKA 50 YA UHURU WA NCHI YA TANGANYIKA NA MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA NCHI YA ZANIBAR MAJI 20% UMEME 20% ELIMU 0% HOSPITALI 1% MADAWA 0% MLO MOJA KWA SIKU TAFAKARI SANA.CCM MNASHANGA LOWASSA KUPANDA DALADALA HAMSHANGAI TWIGA KUPANDA NDEGE.VIONGOZI WA CUF WALIOSHINDA KATIKA UCHAGUZI 2015 WAKIONYESHA SHAHADA ZAO ZA USHINDI ZILIZO SAINIWA NA KUPIGWAMUHURI NA ZEC CCM HAYA HAMUNA,AIBU HAMUINI,FEDHEHA HAMUHISI,UBINADAMU UMEWATUKA,M.MUNGU HAMUMUOGOPI HEBU JIULIZENI NYINYI VIUMBE WA AINA GANI...?????
Wednesday, June 22, 2011
MAMA ASHA UNAWAPA WATU TV KWANI WATU WANAKULA TV..?
unaonaje ukauza hayo mabangili yako ya thahabu na kuwa nunulia chakula ili wasisumbuke kama kweli wewe unataka kusaidi na kuhimiza watu wa wasaidiye anza wewe basi kwanza.kuwanunulia chakula maana chakula kimapanda bei na unajuwa unakwenda kuwapa TV .wao watakula TV au ndio umewapa TV ili wakuoneni nyuso zenu kila wakati wakifunguwa TV huo ni UDIKTETA. wacheni kuwafanya watu wapumbavu kama munataka kusaidi saidiyeni sio TV,DVD,VIDEO,PANGA,JEMBE,SHOKA au UBALE WA KANGA.unajidai kumtaja mzee karume unajipendekaza sio kwa familiya ya karume wacheni ujinga ulimwengu ushamka mnachekwa tena sana mnachekwa kama hamuna la kufanya menyeni viazi nyumbani musijadai mayatima wala wazee wao wana mwenyezi m/mungu na nyinyi bakini na unafiki wenu na wizi wenu wa mali za serekali hizo thahabu umenunuwa na pesa zipi kama sio za mali ya umma ambayo ilikuwa iende kwa hao mayatima lakini hilo hulifikiri ni wewe upendeze kwanza kisha ndio ujionyeshe kwenye TV kuwa ati unachangia kusaidiwa kwa mayatima na wazee unafiki mtupu.
JAMII imeshauriwa kujenga utamaduni wa kuwapenda kwa kuwatunza watoto yatima na wazee ikiwa ni hatua ya msingi itayoweza kufuata misingi ya maadili ya Mzee Karume.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais Mama Asha Balozi, aliyasema hayo jana baada ya kuwakabidhi televisheni tatu Wizara ya Ustawi wa Jamii na maendeleo ya Wanawake na Watoto kwa ajili ya Watoto yatima wa Mazizini, Wazee wa Sebleni na Welezo ambapo kwa kila moja ina thamani ya shilingi milioni 1.5.
Sherehe ya makabishiano hayo ilifanyika katika Makao Makuu ya Wizara hiyo huko Vuga Mjini Zanzibar ambapo Mama Asha aliwataka viongozi wa Wizara hiyo kuona wanaendeleza maadili ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kuwapenda watoto na wazee.
Alisema Rais Karume aliyapenda makundi hayo kwa kuona nao wanbakuwa katika hali nzuri ya kimaisha na ndio maana baada ya Zanzibar kuwa huru aliamua kuanzisha nyumba za wazee pamoja na nyumba za watoto yatima.
Alisema kutokana na kuthamini utamaduni huo ndio maana serikali zote zimeamua kuona makundi hayo yanaendelea kupatiwa matunzo bora ya maisha na haitakuwa busara kuacha kuendeleza maadili hayo.
Alifahamisha kuwa serikali ya awamu ya saba itahakikisha inaendeleza maadili hayo ya Mzee Karume kwa kuwajali Wazee pamoja na watoto yatima kila pale inapoona haja ya kuwa nao pamoja.
Hata hivyo Mama Asha, aliwataka viongozi wa Wizara hiyo kuona wanawapa umuhimu wazee pale inapojitokeza kutaka kupatiwa msaada wa fedha kutokana na baadhi yao hujitokeza maofisini kuhitaji msaada baada ya kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.
“Kuna watu wanaweza kuwajia kuwaomba hata 500 ya nauli baada ya kwenda hospitali sasa msije mkawadharau kuwapa msaada wasaidieni kwani ukitoa moja Mungu atakupa nyengine tuwaenzini wazee” alisema Mama Asha.
Aidha, Mama Asha, aliwataka viongozi na wafanyakazi wa Wizara hiyo, kumpa ushirikiano mzuri Katibu Mkuu mpya kwa kuona kuwa wote ni wamoja kwa vile Wizara hiyo inatarajiwa kuwa kiungo kizuri cha kuwaunganisha wanawake kote nchini.
Nae Waziri wa Wizara hiyo, Zainab Mohammed, akitoa shukrani zake, alisema msaada huo utawawezesha walengwa kujenga upeo wao bora kwa kupata habari matukio na taarifa za maeneo mbali mbali duniani na ndani ya nchi.
Waziri huyo aliahidi kuona kuwa msada huo unawafikia walengwa ili waweze kuwaelimisha walengwa waliokusudiwa yakiwemo makundi hayo.
Waziri huyo alitoa wito kwa jamii kuiga mfano huo wa kutoa misaada yao kwa hali na mali kwani bado kutoa sio kama wanacho bali kuyasaidia makundi hayo ili nayo yawe katika hali nzuri za kimaisha.
Wakati huo huo, Mama Asha alikabidhi msaada kama huo ikiwemo na mashine ya DVD, kwa kituo cha Polisi cha Mfenesini na kuwataka askari hao kukitumia chombo hicho kuweza kufuatilia mambo mbali mbali duniani ikiwa ni hatua itayowasaidia kupata mbinu mpya za kukabiliana na wahalifu.
Alisema amelazimika kuwapatia msaada huo kwa vile muda mwingi hutakiwa kuwa macho kutimiza wajibu wao na kuwapo kwa vitu hivyo vitawasaidia kutekeleza vyema wajibu wao.
Msaada umetolewa na kwa pamoja na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mwanamwema Shein, ambapo kesho Mama Asha anatarajiwa kuwakabidhi wazee wa kisiwani Pemba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment