Monday, June 6, 2011

SMZ-GNU-SUKARI IME AHIDI KUTUNZA MAZINGIRA.MIMI NAULIZA WANANCHI LINI WATAAHAIDIWA KAMA MULIVYO AHIDI MAZINGIRAA..?

2 comments:

  1. Hapo kweli umenena muandishi,hawa viongozi kazi kupiga domo tu,wanajua njia zote za kuzibiti mazingira,umeme ghali tunauziwa,wananchi hawanuwezo wa kulipia bili za umeme,mtu anatumia light 4 tu,tena masaa machahe tu,anatumiwa bonge la bills,hivi kweli mtu ataweka cooker ?

    Gas nayo ndio hatuna kabisa,hainunuliki,hata kama inanunulika jee security kwa mtumiaji ipo ? Nyumba yake ikiripuka jee ? Kuna insurance gani ya kumlinda mwananchi ?

    Usafi wa jiji letu,serikali haina magari ya kisasa ya kufagia barabara,na ndio mana michanga inagika katika mitaro na kuziba,siku za mvua maji yanapotuwama ndio mabarabara yanapoharibika.

    Baraza la mji linatakiwa wapewe vifaa vya kisasa kama ulivyoweka muandishi hapo,ili waweze kukusanya taka mjini na vijijini,pia serikali isimamie maeneo ya makazi watu kujenga jenga ovyo bila ya serikali kupawa hati za ujenzi,kwani hili ndio tatizo moja kubwa la uchafuzi wa mazingira.

    ReplyDelete
  2. Serikali inatakiwa itoe mpango wa miji kwa ujenzi,pamoja na miundo mbinu wa maji taka,ili kuweza kupunguza uchimbaji wamashimo mashino katika majumba yetu,hii pia ni uharibifu wa mazingira,kuwe na miundo mbinu ya maji taka ambao wa kisasa wa kupeleka maji baharini moja kwa moja.

    Ujenzi wa majumba ndio umekisiri sana wa kiholela,serikali ilichukulie hatua haraka iwezekanavyo,la sihivyo tutajistukizia mji mchafu kwa ujenzi wa kiholela na utupaji taka,na ndipo kutaongezeka na vigenge ya watuta bangi na wapikaji gongo,na machafu mengine.

    Pia ujenzi wa holela huleta maradhi ya miripuko kutokana na miundo mbinu ya maji machafu kutapakaa ovyo.

    ReplyDelete