Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari
ameyasema mambo kumi na moja waliyokubaliana serekali ya tanganyika na zanzibar ni
Abubakar aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba wananchi wengi hawaujuwi mkataba wa Muungano wa asili amabpo mwaka 1964 mkataba wa Muungano uliorodhesha mambo 11 ya awali ikiwemo katiba ya Jamhuri ya Muungano, mambo ya nje, ulinzi na usalama, polisi na mamlaka juu ya mambo yanayohusu hali ya hatari.
Mambo mengine ni uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika serikali ya Muungano, kodi ya mapato na ushuru wa forodha na bandari, usalama wa anga, posta na simu.
1)KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO.
2)MAMBO YA NJE.
3)ULINZI NA USALAMA.
4)POLISI NA MAMLAKA JUU YA MAMBO YANAYOHUSU HALI YA HATARI.
5)UHAMIAJI.
6)MIKOPO NA BIASHARA ZA NCHI ZA NJE.
7)UTUMISHI KATIKA SERIKALI YA MUUNGANO.
8)KODI YA MAPATO NA USHURU WA FORODHA NA BANDARI.
9)USALAMA WA ANGAA.
10)POSTA
11)SIMU
sasa haya ndio mambo tuliyokubaliana na serekali ya tanganyika na sio sisi tuliyokubaliana ni nyerere na mzee karume maana mzee karume hakuwashauri mawaziri wake wala hakuwauliza wananchi wake iliungana kwa uwonga wake na uroho wake wa madaraka ili asipinduliwe nyerere alikuwa akimtisha utapinduliwa wee utapinduliwa.sasa swali ni hili katiba ya jamhuri ya muungano sote tunajuwa ni katiba ile ile ya tanganyika ndio iliyogeuzwa na kuwa ya jamhuri ya muungano sasa muungano huwo vipi maana wakati wa mzee karume kama alikuwa na katiba yake kwanini haikuwekwa ktk ile ya tanganyika kisha ikaundwa katiba moja..?
mambo ya nje toka 1964 mpaka leo mambo ya nje yanafanywa na watanganyika ni nani na nani znz aliyekwenda nje nakusema mimi natokeya ktk serekali ya znz nimekuja kuiwakilisha ktk mambo ya nje nani...?
ulinzi na usalama ooooyee tunauwona ulinzi na usalama kila siku tunaingiliwa na majambazi,wizi,vibaka,na siku jeshi au polisi wakilewa wanapinga watu kama hawana akili vizuri na siku za chaguzi watu wanauliwa hatharani na wengine kisirisiri je ulinzi na usalama huo uko wapi..?
polisi na mamlaka juu ya mambo yanayohusu hali ya hatari naona hapa znz hakuna hata hali ya hatari zaidi ya kuingiliwa na majambazi na polisi hawawakamati hao majambazi wala wauza unga wameja kila kona na hao hao polisi ndio wanaopiga rai sasa wa ndio hatari au..?
uhamiaji kwanza hawatupi sisi rai wa znz paspoti mpaka uliwe millioni na usheya pili watu wanaingia znz kama danguroni hakuna lolote uhamiaji imeka kula pesa za haramu za paspoti na kuzuia mizingo ya wafanyabiashara masikini za mungu je ndio uhamiaji hiyo...?
mikopo na biashara za nchi za nje hakuna mkopo unaokoja znz wala znz haitambulika nchi za nje kama serekali sasa nani ataipa mikopo na biashara nchi za nje ni karafu na imethibitiwa na wajuku wa karume ZSTC mwananchi habuwi kitu mpaka asafirishe magendo karafu zake mwenye kuza kwa mangendo je ndio mikopo hio na biashara nchi za nje ilivyo...?
utumishi katika serekali ya muungano ahahaha bora nicheke maana wacha serekali ya muungano hata serekali ya zanzibar basi sio wazanzibar itakuwa serekali ya muungano kwali..?
kodi ya mapato na ushuru wa forotha na bandari ndio mukatuletea TRA-HIV/AIDS sio ijekutumaliza maana munakusanya mapato na kodi za bandari ya zanzibar ila pesa hazionekani zote zinaishia katika matumbo yenu watanganyika au munakata..?
usalama wa angaa hahaha sijaona hata siku moja znz kuwa na denge za kijeshi labda bara sasa ikiwa tutashambuliwa tuwapingiye simu nyinyi kwa vodacom kisha ndio muje na denge zenu mutuhami sio..?mumusikia wapi upumbavu huu..?
posta mawe unatuma baruwa dar mpaka znz inachukuwa miazi 3 na hio ikifika ni salama yako kwanza baruwa munazifunguwa na kuiba kila kilichomo ndani ya barua nani asiyeyejuwa haya munafikiri zanzibar wanahaja sana ya posta..?
simu na umeme ni sawa sawa unapiga dakika 3 unaletewa bili millioni moja nani mwenye haja ya simu ya nyumbani miaka hii ni komputa na simu za mkononi tu hakuna tena simu za ndani au munataka kusikiliza watu wanasema nini katika simu...?
mimi naona mambo yote 11 ni upumbavu mtupu haya znz tunaweza kufanya wenyewe bila ya muungano na wala hatuna haja ya muungano kwanza TRA ikiondoka vijana wengi watapata kazi polisi machogo na majeshi machongo wakirudi kwao wengi vijana znz watapata ajiri ya kuilinda nchi yao na kuihami nchi yao bandari itakuwa bandari huru znz itainuka na itakuwa watu wote wanakazi sio sasa vijana wote bangi,unga mtu hatuna haja ya muungano nauvunjwe nauvunjwe nauvunjwe
No comments:
Post a Comment