Friday, June 10, 2011

WABUNGE WA ZANZIBAR NI WABUNGE WA MATUMBO YAO NA FAMILIYA ZAO


MBUNGE WA ZANZIBAR IKITOKEA DODOMA

Tumekuwa tukishangazwa sana na wabunge wetu kutoka zanzibar pale wanapohuzuria katika bunge la tanganyika mjini dodoma,nashindwa kuelewa kabisa nini hasa kinachowapelekea hawa wabunge wetu kuhudhuria bunge lile la watanganyika huko dodoma.
Kwanza tunajiuliza wanapoingia bungeni nini hasa wanachokijadili katika masuala ya serekali ya tanganyika au maswala ya serekali ya zanzibar ? Na hicho wanachokijadili  vipi kinawafaidisha wazanzbari ? sijawahi kusikia bunge la serekali ya tanganyika limepitisha bajeti yake ya tanganyika na zanzbar nayo imefaidikia katika bajeti hiyo.
Sijawahi kusikia mbunge amepokea pesa kadha wa kadha za kuendesha jimbo lake hata siku moja ila akirudi huwa kanawiri na mambo yake sio mabaya kama alikuwa anaishi ktk nyumba ya kukodisha hagfla utasikiya anabonge la jumba kiembe samaki au migombani au bububu,toka nipate akili yangu timam sasa ni miaka kumi namoja,sijasikia mbunge kupewa mfuko kutoka kwa watanganyika aliendeshe jimbo lake hapa zanzibar.
Sijawahi kusikia serikali ya tanganyika itasaidia serekali ya zanzbar katika nyanja za elimu kwa vile zanzibar ni moja ya part ya muungano huu feki unao wala roho na kuwabuguthi wazanzibar,hata bajeti yao halengi zanzbar.
Sijawahi kusikia bunge la tanganyika/tanzania la muungano feki kutoa mfuko wa fedha katika suala la miundo mbinu hapa zanzbar unguja na pemba,mfano barabara,umeme na maji na madawa ktk hospitali au ambulensi gara la kubebeya wagonjwa,hata siku moja toka uazishe muungano feki huu mwaka 1964.
Ukweli upo zahiri kabisa,tembelea huko pemba barabara zote zimechoka,maji hayatoki tena miji imekuwa mikubwa,umeme hakuna na kama uko ni sehemu chache na sehemu nyengine hauja fika kabisa na huu ni mwaka 2011 je hao wabunge waliyoteuliwa zanzibar nzima wa unguja na pemba wanafanya nini huko bungeni ikiwa wananchi faida haiwafiki..?
Pia kuna mfuko wa misaa ya kigeni ya kusaidia mazingira ambayo yameharibika kwa Global warming,mfano katika kanda za bahari,maji yanvyo panda juu,kuna mfuko ulitoka kwa suala hili lakini zanzbar imeambulia patupu au wabunge wetu wa zanzibar wamepewa ila washazipiga karata na kujiendeleza wao na wake zao na watoto wao na huku wananchi tuna haha na maisha.
Tumeshuhudia serikali ya tanganyika ikifungua University kila mikoa ya tanganyika huko bara,lakini hata kusema tuwafungulie hawa wenzetu wa muungano feki,huko pemba chuo japo cha kutoa Diploma,lakini wapiiii.
Tumeshududia serikali ya tanganyika ikipokea misaada ya njee ya pesa za kusaidia miundo mbinu ya train,tena misaada hiyo inakuja kwa jina la tanzania ndio kama znz tumo ila ni koti tu wao ni tanganyika na sote tunajuwa,basi na sisi tupeni hizo pesa japokuwa hatuna railway lakini tunabarabara zimechakaa,nyengine zinatakiwa kutanuliwa na nyingine zinataka kujengwa sasa haswa maana haziko pia hatupewi pia.
Sasa nauliza hawa wabunge wetu kutoka zanzbar nini wanaenda kujadili katika Bunge la tanganyika huko bara mjini dodoma.. ? Je Zanzibar inafaidika vipi katika kupitia muungano feki huu sasa tunakariibia miaka 50 nusu karne ?
Tunachotaka wabunge wetu watueleze kile wanachoenda kukijadili na vipi tumefaidika ndani ya miaka kumi tu sitaki mingi watueleze kuanzia 2001 hadi sasa 2011,vipi tumefaidika..? na kama hawawezi kutueleza basi hatuna haja ya wabunge wasiokuwa na faida wabunge jina upumbavu mtupu znz haina haja ya wabunge ni wawakilishi basi na nchi itakwenda ikiwa hawa wawakilishi pia hawatakuwa wezi maana tuliyo nao sasa wote ni wezi tu maana hatujaona jambo hata moja kubadilika.
Kwa upande wangu sioni haja ya kuukumbatia muungano feki na mukiendeleya kukumbatia ndio munazidi kutuchafuwa na kujuwa kuwa munaukumbatia kwa kuwa ndipo penye chaka lenu.
 la mathabi yote munajuwa fiki mukiliwacha mutakuwa hamuna tena mahala paa kuficha maovu na machafu na mabaya na wizi wenu ndio maana wabunge wa zanzibar munaendeleya kukumbatia muungano feki,na naamini wabunge wote wa zanzbar ni wabinafsi kabisa, hawawezi kutueleza matunda yoyote yale ya muungano feki kwa sababu hayo matunda hayawafiki wananchi yanawafikiya nyinyi na wake zenu na watoto wenu basi chungeni sana au na nyinyi pia mutaishia kama mubarouk,ben ali,gaddafi na saleh wote wanakiona sasa na familia zao na nyinyi tieni maji kabisa kamba hatuja anza kuwanyowa.

No comments:

Post a Comment