Wednesday, June 1, 2011

POLISI Z;BAR WAKAMATA ALIYEKUWEMO NASIYEKUWEMO PWANI MCHANGANI



Wananchi mbali mbali wakiwa nje ya jengo la mahakama ya wilaya ya Mfenesini wakifuatilia kesi za wananchi waliokamatwa wakidaiwa kuchoma moto mabanda ya biashara huko kaskazini Unguja


PWANIMCHANGANI imegeuka gharika. Tangu pale wanakijiji walipoteketeza mabanda ya biashara ya wajasiriamali kutoka Tanzania Bara, polisi wamepiga kambi na kukamatakamata watu.
Hakuna kiongozi wa polisi anayekubali kusema watu wangapi wameshakamatwa, lakini taarifa zilizonifikia kutoka kijijini na kwa walinzi wa mazingira na haki za binadamu, zinasema “ni wengi.sana”
Wanasema askari anagonga mlango wa nyumba yako, wanachukua anayetoka. Bali wanaotakiwa hasa ni wanaume.Zinakuja taarifa kumbe siku moja kabla, wanakijiji kupitia mkutano na viongozi wao, walijadili kwa kina mashakil (matatizo makubwa) yanayoletwa na wajasiriamali na kupitisha azimio la kuteketeza mabanda.
Wanakijiji wa Pwanimchangani wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusu vitendo viovu vinavyofanywa na wahamiaji wanaofurika maeneo ambayo moja ya biashara yao kubwa, ni ulevi,bangi,madawa ya kulevya,pombe za kienyeji na uhasharati wanawake kujiuza kwa pesa. – baba wa maasi.
Wanywaji wakishautwika, kinachofuata ni muziki wa sauti kubwa, kelele na vituko ambavyo ni kero kijijini petu. Athari za vitendo hivyo zinatua kwa watoto na jamii kwa jumla.
Yote hayo ni mambo mageni kwa kijiji hiki na vile vya jirani. Ni kero kwa ukanda mzima wa kaskazini mashariki kama ilivyo kwa kusini mashariki mwa kisiwa cha Unguja.
Ulevi, kelele na vituko si katika utamaduni wao. Katika nchi inayoheshimu maadili na silka za wananchi wenyeji, vitendo kama hivi vingekwishadhibitiwa zamani ila z;bar viongozi wetu hata habari hawana na polisi wanaendeleya kuwasha aliyekuwemo na asiyekuwemo.
Hakuna wa kuvidhibiti isipokuwa wananchi wenyewe kwa utaratibu; lakini viongozi wa kiserikali ndio wenye dhamana ya kulinda mila na desturi za watu.
Kwani Zanzibar haina viongozi? Mbona wapo wengi na katika kila ngazi. Yupo rais, yupo waziri anayehusika na ulinzi wa haki za kiraia, wapo mawaziri wanaosimamia ustawi wa jamii, mazingira, biashara na utalii.Wapo wakuu wa mikoa/wilaya. Wapo masheha ila hawaonekaniki kabisa sasa maana uchanguzi siushakwisha na washapata wanalolitaka basi wananchi wacheni wafee watakao baki tutaonana baada ya miaka mitano kwenye uchanguzi mpya hawa ndio viongozi wa z;bar.
Nilipozuru vijiji vya mwambao wa bahari ya Hindi  nilielezwa tatizo kubwa la kutowajibika kwa viongozi wa serikali katika kutatua matatizo ya wananchi tangu sekta ya utalii ilipoanza kushamiri.Nilielezwa suala la wajasiriamali kuvamia maeneo ya ardhi na kuyashikilia. Kelele za wananchi kutaka waachiwe maeneo yao zimepuuzwa kwa majibu mepesi.
“Kila mtu ana haki ya kuishi atakapo katika Jamhuri ya Muungano.” Kama anaishi kisheria haihusu.sio mtu aje kutoka bara anaona kiwaja kitupu pwani anajenga bar na kuleta wanawake wake ili wajiuze ukienda polisi wanasema ni mtanzania anahaki ya kuishi ndio ila ni kiwanja changu  na mimi sitaki  sasa Uporaji wa ardhi katika ukanda huu ni tatizo kubwa. Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)walipo wanyanganya watu mashamba yao 1964 na kuwa wao ndio wamiliki wa ardhi yote ya z;bar  wamehodhi maeneo yanayotumiwa na wananchi kwa kilimo. Baadhi ya viwanja viliuzwa  kwa fedha nyingi  Nungwi na Kidoti na maeneyo mengi tu hapa z;bar.
Ni pamoja na maeneo haya kumejengwa holela. Hata miundombinu ya huduma nyinginezo ilijengwa kinyemela. Hapana shaka hakuna ulipaji kodi. Wajasiriamali wanafanya kazi kama vile wapo msituni.
Zanzibar imekuwa na tatizo la siku nyingi la siasa kutawala kila nyanja. Tangu uchaguzi wa 1995, viongozi wa CCM walibuni mpango wa kuvuruga uchaguzi kwa kushirikisha wasiokuwa Wazanzibari. Wameutekeleza vizuri.
Kupitia mgongo wa serikali walifadhili vijana walalahoi katika wilaya za Dar es Salaam pamoja na Bagamoyo na Mkuranga na Tanga kuwapeleka Zanzibar wakati wa uandikishaji wapiga kura na wakati wa upigaji kura.Mpigapicha mmoja aliyestaafu aliwahi kutamka hadharani aliponyimwa ajira ya mkataba, kuwa viongozi wa CCM wamesahau alisaidia kufanikisha ushindi 1995 na 2000. Alidai kupelekwa Mkuranga akifuatana na mpigapicha kijana kupiga picha vijana waliokuja kuingizwa kwenye daftari la wapiga kura hapa z;bar.
Baadhi yao waliorudi – maana wapo waliogoma kwa kuhofia kupigwa na wenyeji – na kupiga kura wakati wa uchaguzi, na wengine waligoma kuondoka kwa kusema: “Ni zamu yetu kutafuta maisha kama wao viongozi wa z;bar wameshapata walichotaka.”Wengi wao waliobaki, walipelekwa vijijini ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Watu wanakumbuka namna wanawake waliotoka mkoa wa Tanga walivyohanikiza kijini cha Nungwi hata kusababisha wanawake wenyeji kuandamana hadi kwa mkuu wa wilaya wakitaka lazima wanawake hao wageni wafukuzwe kwani “walikuwa wanachochea zinaa kwa kuwalaghai waume zao.”
Walilalamika kuwa waume zao, hasa vijana, waliokuwa wakivua, wamekuwa wakitoroka familia zao na kutumia fedha zote kufuga vimada waliofungua makazi yao maeneo ya ufukweni.Katika kujibu malalamiko, wanawake wa Kitanga walisema: “Sisi tunaishi hapahapa na kama wanaume wanajiachia kwetu hatuwezi kuwanyima tutawapa wanachokikosa kwa wake zao hata kama ni kuwaramba nyao zao tutawaramba wazanzibar wanaume ni wazuri sana sisi hapa ndio tushafika haturudi Tanga ngoo. Tunawapa huduma ambazo wanazikosa kwa wake zao.”
Ni hapa kuliibuka misamiati ya kuonyesha namna gani mapenzi ya wanawake hao wa kitanga walivyo furahishwa na wanaume wa kizanzibar na jinsi wao wanavyo wapa wanaume wakizenji mpaka yamewazingua wanaume wa Nungwi hata kusahau familia zao. Leo ukienda masoko ya Mkokotoni na Kinyasini, utakuta wachuuzi wengi wa bidhaa ni wanawake waliotoka nje ya Zanzibar.Nataka ieleweke kwamba wanaoitwa wajasiriamali waliingia kinyemela. Walitwaa ardhi. Walijenga mabanda. Wanaishi bila ya kufuata taratibu.
Viongozi wa serikali, zilizopita na iliyopo, GNU au SUKARI  na CCM, wanalijua hili chini juu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania (Muungano), alipokuwa anasimamia wizara ya biashara, utalii na uwekezaji, aliwahi kuendesha operesheni ya kuvunja makazi holela.
Alilaumu viongozi wa maeneo hasa mkoa wa Kaskazini Unguja kwa kukaribisha wahamiaji kinymela. Mbele ya wananchi katika moja ya mikutano yake, alisema: “Nyinyi ndio mliwakaribisha,na muliwaleta hapa kuja kupinga kura sasa kura zishakwisha kwanini hawarudi makwao na  mkaidhinisha wapatiwe kitambulisho cha Mzanzibar”Bali inajulikana dhahiri masheha hawakuwa na ubavu. Mara nyingi wakisema wanatekeleza amri za wakubwa na ndio wakubwa hao walisema waletwe ili wawapingiye kura maana wanajuwa fika kuwa wazanzibar hawawataki tena viongozi hawa sasa ndio wanaleta walalahoi kutoka bara ili wawapingiye kura washinde waendele kuka madarakani na hao watu zawadi yao ndio kutuvamiya sisi katika vijiji vyetu na kuanzisha makazi.
kume ibuka malalamiko ya wenye hoteli wanasema watu wamejenga kiholele pembezoni mwa fukwe na ndio hao wabara maana wazenji wote wananyumba zao na wenye hoteli za kitalii kwamba makazi holela pembeni mwa hoteli, yanaharibu mandhari. Watalii waliyalalamikia na kutishia kutotembelea Zanzibar.Uliokuwa mtaji wa kisiasa, umekuwa kero ya kisiasa. Hii ni changamoto mojawapo ya waziri mpya, Nassor Ahmed Mazrui, anayetoka Chama cha Wananchi (CUF), chama mlalamikaji mkuu wa ufisadi katika siasa.
Hakuna ubaya kwa Mtanzania kutafuta maisha popote anapotaka, lakini je aweza kufanya hivyo kinyemela? Atoke Makunduchi, Bambi au Nungwi, akavamie eneo Kigamboni na kujenga? Ataachiwa?Wazanzibari wengi wamelewea Bara. Wamevamia ardhi? Wameanzisha maduka bila leseni? Hawalipi kodi? Niulize haya kwa sababu wapo wanaoamini unyama ule umefanywa kwa sababu wahusika ni watu kutoka Bara.
Nasema njia iliyotumika kudhibiti kero ni mbaya na ni uvunjaji sheria. Utaratibu ni kitu muhimu kufuatwa.Sasa Pwanimchangani kumejaa hofu. Mwandishi mwandamizi  aliyefika kijijini wiki iliyopita, alielezwa na familia za wanaoshikiliwa na dola kwa kesi ya tukio hilo, kuwa wanaumia.
Ni wanaume saba tu walioshikwa na wengine wengi wameshikwa bila ya hatiya yoyote. Nyumbani wameacha wanawake kadhaa na watoto 24, wakiwemo wanaosoma, hawana msaada. Vijiji hivi vya pwani vina umasikini mkubwa licha ya kuzungukwa na maliasili nono.Hawana msaada tofauti na wale walioathirika ambao wanasaidiwa na taasisi na hata serikali ina wasaidia sana waliyochomewa mabanda kuliko sisi rai ambao waumezetu wameshiko kwa ati kuchoma mabanda ya hao wabara sasa sisi ndio wenyeji hapa au sisi ndio wangeni tunaiuliza serekali ya SHEIN na SEIF..?.
Wenyeji wanajiona kama “wanaharamu” kwa wanavyofanyiwa ndani ya eneo lao na polisi ambao wengi wao ni wabara. Wanasikitika kutengwa na mbunge wao, Kheri Khatib, na Mwakilishi wao, Abdi Mossi, ambao hawajaonekana kijijini tangu tukio hilo litoke.

2 comments:

  1. I wish you, men & women of Zenji, could come together and come up for your HUMAN RIGHTS !!!

    My dua's are all for you to be UNIT in Zenji and come together and tell your politicians.... IT CAN'T GO ON LIKE THIS !!!!

    May Allah SWT bless you and give you iman to carry this burden.

    ReplyDelete
  2. Mungu atawajalia wale walipaya mitihani hiyo,lakini ni funzo kwao kwani hao ndio wapiga kura wa ccm,na wakilishi wao na wabunge ni ccm,sasa nani wa kuwasaidia ?

    ReplyDelete