Wednesday, June 15, 2011

UJAMBAZI Z;BAR HAUTAPUNGUWA MPAKA TUWE NA COAST GUARD BOATS KUIZUNGUKA ZNZ NA KUVILINDA VISIWA VYETU PEMBA NA UNGUJA.



Unga na usafirichaji vitu vya wizi hutumiwa sana mwambao wa Z'bar .

GNU wapitishe bageti kuhusu patrol boat zakileo ili kuzibiti wezi na majambazi wanao kuja na viboti uchwara Zanzibar
Maalim Seif ashtukia dawa za kulevya

 
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akikangua shughuli zinazofanyika katika Bandari ya Malindi Zanzibar ambapo ameangiza mizigo ifanyiwe ukaguzi mkubwa katika kuthibiti Dawa za kulevya (Picha na Mwinyi Sadallah, Zanzibar)

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif  Sharif Hamad, amesema kuna tetesi kuwa Bandari ya Malindi hutumika kama uchochoro wa kupitishia dawa za kulevya.
Maalim Seif alisema hayo Katika mazungumzo yake na viongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) katika Makao Makuu ya shirika hilo, Malindi mjini hapa jana.
Alisema wakati umefika kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha shughuli za upekuzi wa mizigo katika bandari hiyo na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume ili kufanikisha vita dhidi ya dawa za kulevya.
“Kuna tetesi nimepata, dawa za kulevya zinapitishwa kupitia Bandari ya Malindi, ni vizuri maofisa wa forodha na vyombo vya ulinzi vichukue hatua za kuimarisha shughuli za upekuzi,” alisema Maalim Seif.
Alisema shughuli za usalama katika bandari hiyo, lazima zifanyike kwa umakini, ikiwa ni pamoja na kutumia  mbwa




  maalum kutambua madawa ya kulevya kabla ya mizigo kuruhusiwa kutoka katika bandari hiyo.
Alisema vifaa vya mitumba vya nyumbani vinaingizwa katika soko la Zanzibar, kama vile friji, televisheni na redio vifanyiwe upekuzi wa kina na kwamba wakati umefika kwa uongozi wa bandari kushirikikana na vyombo vya ulinzi na kutenga eneo maalum la kufanikisha kazi hiyo.
Alisema kwamba Bandari za Zanzibar inakabiliwa na ushindani mkubwa na bandari za Tanga, Mombasa na Dar es Salaam, hivyo ni lazima ziwe na vifaa vyote muhimu ili kusaidia kuharakisha utoaji mizigo kwa muda mwafaka.
Awali, Waziri wa Miundombinu, Hamad Masoud, alisema wizara yake imeamua kudhibiti uingiaji wa watu holela katika bandari ya Malindi na kuruhusu watu wenye vitambulisho maalum vya kazi.
Alisema hatua hizo zinalazimika kuchukuliwa kwa kuzingatia masharti Shirikisho la Usafiri Baharini Duniani (IMO) kuhusu usalama wa vyombo vya usafiri katika kukabiliana na vitendo vya UHALIFU  kama vile UNGIZAJI UNGA((DRUGS)) na MAJAMBAZI wa kuvunja nyumba za watu na hotel kisha hukimbiliya baharini na viboti vyao uchwara.






mimi naona kama itasaidi sana na kuipa hishima nchi ya z;bar kwa mara ya kwanza kabisa itahishimika na kutakuwa na ajiri kwa vijana wengi tu ikiwa nia ipo basi njia ipo au ndio itakuwa yale yale kuletewa watu wa bara waje wawe coast guard itakuwa haina maana hata pesa mbili wawe vijana wenyewe wa z;bar

No comments:

Post a Comment