Sunday, June 5, 2011

WAZANZIBAR VYAMA SIO VINAVYO KOMBOWA NCHI NI WATU NDIO WANAOKOMBOWA NCHI NA NI SISI WAZANZIBAR MDAA UMEFIKA


Umoja ni NGUVU.
Ndugu wazanzibar,kuna ukimya umekisiri sana juu ya katiba mpya,viongozi wetu nao wamelikalia kimya hili suala la katiba mpya bila ya kukaa katika BLW kulijadili kisheria na kutumia nguvu zao zote la baraza na kudai haki za msingi katika katiba hiyo inayo kuja na kupenyezwa penyezwa kisiri siri na  hata uundwaji wake ni wakini macho.
Ni vyema sasa hivi wazanzibar kuacha ufuasi wa chama kwani wakati wa siasa umepita,sasa tutumie nguvu zetu na mapenzi yetu kuipenda ZANZIBAR kwa hali yoyote ile kama tulivyokuwa tukikipenda chama cha CCM NA CUF kwa kutetea haki zetu,tulipigwa,tuliwekwa marumande,tumechomewa moto mali zetu,tumekuwa walemavu,tumepoteza hata maisha ya ndugu zetu,yote kwa kuvipenda vyama tu.
Sasa ni wakati wa kuipenda ZANZIBAR tushikamane kwa umoja,tufanye kitu cha uhakika,ili serikali itutambue kama wananchi tumeamua hili hatutaki tena kutawaliwa na watanganyika na kuongozwa na watanganyika na kuamuliwa kila kitu cha nchi yetu na watanganyika,kubwa ni muungano maana ndio chaka la kila uchafu na mabaya wanayotufanyia na kututhalilisha nakututia umasikini na kutufanya kam sio watu haswa ni muungano ndio chaka lao walilojifichia,tuuvunje muungano.
Tufanyeni maandamano,tunaomba viongozi wa jumuiya zote,tutoe ushirikiano kwa ajili ya kuitetea nchi yetu ya ZANZIBAR,wakati ndio huu wa kupigania uhuru wetu,nchi zote zilizo tawaliwa tayari washapigania haki zao,jee sisi tunasubiri nini ? Hivi kwa akili zetu watanganyika watatupa haki zetu juu ya muungano au watatuambiya haya basi chukueni nchi yenu hii?
Hata siku moja,mapezi ya vyama sasa tuyaacheni tuipende ZANZIBAR,tuwe tayari kupigania ZANZIBAR kwa hali yoyote kama tulivyokuwa tukipiganiya CCM ishinde kila uchanguzi au CUF ili ishinde kila uchanguzi sasa ni wakati wa kuipiganiya ZANZIBAR na kama tulivyokuwa tukipenda CCM  na kuipenda CUF sasa tugeuke na kuipenda ZANZIBAR kwa hali na mali tumepingana mpaka tumepata serekali ya umoja wa kitaifa nguvu zile tuzitumiye kuikombowa ZANZIBAR ili tujitawale wenyewe na kila kitu tuendeshi wenyewe wazanzibar.
Umoja ni nguvu

No comments:

Post a Comment