Thursday, June 30, 2011

NCHI YA Z;BAR INA BALOZI TANO TU NCHI ZA NJE NA ZOTE NI DOGO KWA NINI NA Z;BAR NI NCHI...??



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba ni Wazanzibar watano tu ambao wana hadhi ya kuwa mabalozi kamili wanayoiwakisha Tanzania nje ya nchi.
Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud Mohamed aliliambiya baraza la wawakilishi. Kati ya Wazanzibari hao wawili tayari wamestaafu kazi akiwemo aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Italia balozi Ali Karume.
Aboud alisema hayo wakati alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa ni wazanzibari wangapi ambao ni mabalozi kamili wanayoiwakilisha Tanzania nje ya nchi na vigezo gani vinavyotumika katika kuwachaguwa.
Akifafanua zaidi Aboud aliwataja mabalozi hao kuwa ni Balozi Mohamed Mwinyi Mzale ambaye anaiwakilisha Tanzania huko Sweden, balozi Ali Shauri anayeiwakilisha Tanzania Misri,balozi Omar Ramadhan Mapuri aliyeko China pamoja na Ali Karume aliyekuwa Italia na Hussein Said Khatib huko Oman ambao tayari wamestaafu kazi.
Alifafanua na kusema kwamba vigezo vya mtu kuwa balozi kamili anayeiwakilisha Tanzania ni kufuata ngazi mbali mbali ambazo zipo katika wizara ya mambo ya nchi za nje ikiwemo vyeo na elimu.
Aidha alisema uamuzi wa kuteuliwa kuwa balozi unatokana na rais wa nchi ambapo akiamuwa kumteuwa mtu kuwa balozi basi anakuwa balozi na kumtangaza.
Aboud alisema Zanzibar haina sifa kuwa na ofisi kamili za ubalozi wa nchi za nje ziliopo Tanzania ambapo kwa mujibu wa sheria za kibalozi,makao makuu ya nchi ndiyo huwepo ofisi za kibalozi.
Kwa sasa Zanzibar zipo ofisi ndogo za ubalozi wa nchi za nje ikiwemo ubalozi wa China.India pamoja na ubalozi wa Misri,Oman pamoja na Msumbiji na nchi za Skandinavia. Mambo ya nchi za nje.


mnataka kutuambiya wasomi wote waliyo jaa znz hakuna anaewezakuwa balozi nchi za nje sio..?  au hamutaki kuwachanguwa wasomi munampango wa kupeleka waume WA DADA ZENU NDIO WAWE MABALOZI WA ZANZIBAR NCHI ZA NJE...? MUTAHONGANA VYEO MPAKA LINI JAMAA HII 2011 ULIMWEGU USHABADILIKA SO TENA HUYU NI MTOTO WA CHACHI NA HUYU NI WAHALO SASA NI WASOMI TU NYINYI BADO NA UZEMBE WA KUHONGANA VYEO KISA KAMUOWA DADA YAKO DUUUUUH

TANGANYIKA VS ZANZIBAR
MABALOZI WA TANGANYIKA ULIMWENGUNI

ZIARA ZA MAALIM SEIF ZIMELETA TIJA

                                  WAZIRI FATMA ABDUL-HABIB FEREJ

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameipitisha bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais ambayo iliwasilishwa juzi Barazani hapo na waziri wa Wizara hiyo Fatma Abdul-habib Ferej huku akitetea ziara ya Makamu wa Kwanza wa Rais nje ya nchi kwamba zilikuwa na maslahi na faida kubwa kwa maendeleo ya nchi.
Bajeti hiyo ilipitishwa baada ya wajumbe wote wa baraza hilo kuridhishwa na ufafanuzi wa hoja na masuali yao waliyouliza wakati wakijadili ambapo alitaja ziara za Makamu wa Kwanza faida zake ni nyingi ikiwemo ile ziara ya nchi za Mashariki ya Kati alipokutana na wafanyabishara na wawekezaji ambao baadhi yao wameonyesha nia ya kushirikiana na Zanzibar katika uwekezaji kufungua mahusiano kati ya Zanzibar na nchi hizo.
Katika ziara ya nchi za kiarabu ikiwemo Oman Waziri huyo alisema Makamu wa kwanza katika ziara yake hiyo imefungua milango kwa kurejesha mahusiano mema kwa kuwa Zanzibar na Oman ni marafiki na ndugu wa muda mrefu ambapo katika mazungumzo hayo yameweza kurejesha upya safari zake kati ya Oman na Zanzibar, mazungumzo ya kuanzisha shirika jipya la ndege la Zanzibar na msaada wa uchimbaji mafuta.
Wakati wakichangia hutuba ya bajeti ya ofisi ya makamu wa kwanza wa rais baadhi ya wawakilishi walitaka kujua mafanikio yaliopatikana katika ziara za makamu wa kwanza wa rais kwa kuwa kitabu cha hutuba hakijaeleza mafanikio yoyote yaliopatikana katika ziara hizo.
Aidha waziri huyo alisema mbali ya faida hizo, pia yalifanyika mazungumzo ya kuomba msaada wa ujenzi wa Bandari mpya na kudumisha uhusiano mwema baina ya Zanzibar na nchi za eneo hilo.
Akizungumzia suala la madawa ya kulevya ambalo limechukua muda mrefu kujadiliwa na wajumbe na kuitaka serikali kujikita katika suala hilo kwa kuweka mkazo mahsusi kwa lengo la kuwanusuru vijana Waziri huyo alisema anakubaliana na maoni ya wajumbe na kuahidi kwmaba serikali itaendelea na juhudi zake na kupambana na tatizo hilo kwa kushirikiana na vyombo husika na wananchi.
Kuhusu maambukizi ya vizuri ya ukimwi Ferej alisema Zanzibar kwa akiasi fulani imefanikiwa kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na kueleza huku akijibu hoja za wajumbe ambao wamehji mfuko huo kutengewa fedha nyingi alisema ni kutokana na umuhimu wa kazi hiyo kubwa na kupambana na ukimwi.
Alisema Ofisi ya makamu wa kwanza wa rais ipo kwenye mikakati ya kuangalia mapungufu ya sheria ili kuweza kuzuia uingiaji wa dawa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiathiri vijana wengi na hatimae kupata maambukizi ya vizuri vya ukimwi.
Kuhusu uharibifu wa maliasili zisizorekebishwa alilifahamisha baraza hilo kuwa Ofisi yake ipo hatua za mwisho kuweka kanunui ambazo zitasaidia kuzilinda na kuzififadhi kwa manufaa ya vizazi vilivypo na vijavyo.
Alisema Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya tabia nchi, ikiwemo mashamba kuingia maji ya bahari, maji kuingia chumvi na hata baadhi ya maeneo kumengwa na bahari na kubainisha kuwa ofisi inaandaa mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Wakichangia bajeti ya Ofisi hiyo wajumbe hao wajumbe wa Baraza hilo waliomba nyumba za Sober House ambazo zimekuwa zikiwahifadhi vijana walioacha matumizi ya dawa za kulevya kujengwa mbali ya nyuma za makaazi ya watu.
Aidha alizungumzia suala zima la sekta ya utalii ambapo alisema zinapaswa kuwa na mikakati ya madhubuyi ya kupunguza kasi ya maambukizi ya ukimwi, pamoja na kuongeza kasi ya mapambano hasa ikizingatiwa kuwa Zanzibar imekuwa na uingiaji na utokaji mkubwa wa watu kutoka sehemu mbali mbali

Z;BAR IMEFUNGUWA MILANGO KWA WAZBAR WALIOPO NJE YA NCHI KUJA NCHINI Z;BAR


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefunguwa milango wazi kwa Wazanzibar waliopo nje ya nchi kuja nchini na kushirikiana na wananchi katika ujenzi wa nchi na kuleta maendeleo zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akiwasilisha makadirio mapato na matumizi ya bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha 2011-2012 hapo katika baraza la wawakilishi.
Dk Mwinyihaji alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambuwa mchango mkubwa wa wananchi hao katika kusaidia na kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo imeanzisha idara ya kuratibu maendeleo ya wazanzibari walipo nje inayojulikana kwa jina la Diaspora.
Alisema Idara ya Ushirikiano wa kimataifa na uratibu wa shughuli za Wazanzibari waliopo nchi za nje (DIASPORA) tayari imeandaliwa mipango ya kuwashirikisha wataalamu mbali mbali katika mikutano ya kikanda ikiwemo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika mjadala wa soko la sarafu.
Aidha Idara hiyo pia imeanza utaratibu wa kukutana na wazanzibari walionje ya nchi ikiwemo Uingereza na kuwataka kuwa tayari kushirikiana na serikali ya Zanzibar kwa kutoa michango yao baada ya kuandaliwa kwa mpango na sera inayowashirikisha na serikali yao.
Dk Mwinyihaji alisema mazingira ya kisiasa yaliopo sasa ni mazuri,ambapo Zanzibar ipo chini ya mfumo wa Serikali ya umoja wa kitaifa iliyowashiriikisha wanan chi wote kufanya kazi.
Aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba serikali tayari imeanza kufanya mawasiliano na wazanzibari waliopo nje kuja na kushirikiana na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa nchi.
Alisema mafanikio hayo yameanza kuzaa matunda ambapo wizara ya mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa kwa kushirikiana na umoja wa wazanzibari waliopo Uingereza kufanya mkutano mkubwa ambao ulikuwa na lengo la kuwakutanisha na kutambuwa Mchango wa Watanzania walio nje ya nchi.
“Mkutano ule ulikuwa na manufaa makubwa ambapo ulihudhuriwa na waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa Bernard Membe…..watendaji wetu kutoka SMZ walihudhuria na mambo mengi yalizungumzwa kwa faida ya Zanzibar ikiwemo kuitangaza Zanzibar”alisema Mwinyihaji.
Alisema tangu kufanyika kwa mkutano huo yamekuwepo mafanikio makubwa kwa baadhi ya wananchi wazanzibari waliopo nje kuonesha nia ya kuja nchini na wengine kusaidia shunguli mbali mbali za ujenzi wa taifa.
Mwinyihaji aliliambiya baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashirikishwa kikamilifu katika mikutano mbali mbali ya kimataifa na kanda ikiwemo taasisi za kimataifa.
Kwa mfano Mwinyihaji alisema kwamba Zanzibar itanufaika kwa kiasi kikubwa kufuatia kuanzishwa kwa eneo huru la biashara la utatu COMESA pamoja na Jumuiya ya Afrika ya mashariki pamoja na SADC.
Alisema eneo la soko hilo ni muhimu sana likiwa na nchi wanachama zipatazo 26 likiwa na idadi ya watu Milioni 600 na wastani wa pato la taifa linalofikiya dola za kimarekani Trilioni moja.
Mwinyihaji alisema kuanzishwa kwa soko huru la utatu utakuza biashara na kuongeza uwekezaji katika viwanda na kukuza miundo mbinu katika nchi wanachama wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
“Mheshimiwa hili eneo la biashara la utatu ni muhimu sana tukilitumia vizuri basi yapo manufaa makubwa ya kuimarika kiuchumi na biashara” alisema waziri huyo.
Aidha aliwaambiya wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba Zanzibar inashiriki kikamilifu katika vikao vyote vya jumuiya ya Afrika ya mashariki,ambapo watendaji wake wamekuwa wakishiriki katika mikutano ya matayarisho la baraza la mawaziri na wakuu wa nchi.
Mwinyihaji aliliomba baraza la wawakilishi kuidhinisha jumla ya sh.33,127,.2 Milioni ambapo kati ya hizo jumla ya sh.29,386.2 kwa ajili ya kazi za kawaida na jumla ya sh.1,930.0 kwa kazi za maendeleo katika mwaka 2011-2012.

TANGANYIKA NDIO WENYE JESHI Z;BAR NA SILAHA-WAZ;BAR HATUNA KITU YAKITOKEYA YAKOTOKEYA HAYAWAPATI NYINYI NI VIONGOZI HUTUPATA SISI NA DUNGU ZETU WALIO KIMBIA MUSITULETE UBABAIFU

 Waziri wa Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini namnuku alivyo sema(zaidi kufuatia kuwepo kwa mazingira mazuri ya kisiasa ya amani na utulivu nchini.)unasema kweli au unataniya watu wewe..?juzi juzi hapa kulikuwa na mabala ya mswaada na mpaka tukauchana na kutiya moto na mpaka leo bado tunamivutano.kisha unasema kama hivi unamanisha nini..? sio kama sitaki dungu zetu warudi kwao laa hasha ila vipi utawarudisha hapa na watu ndio kwanza tunapigania uhuru maana z;bar haiko huru bado tunatawaliwa na mkoloni mweusi nawashasema 2014 katiba mpya inakuja tukitaka tusitake ndio katiba na znz nzima hatutaki muungano.kama wewe na seif munataka wazenji warudi vunjeni muungano kisha nyamazeni kimya muona kama denge hazikutuwa kila leo ila mchezo huu hatutaki watu wakati wa ali hassan mwinyi alipokuwa raisi wa muda znz alisema hivyo hivyo znz ni jemaa atakae aje kisha akakimbiliya dar wakatuekeya salmin amour akatunywisha maji kikuku watu wakakimbia wengine wakaishi mombasa shimoni kenya hapo sasa munataka tena sio mchezo wenu huu mara hii sithani dungu zetu waliyokuwepo nje watakuwa wajinga kiasi hichi mpaka muungano uvunjwe hapo utaona.

Wednesday, June 29, 2011

JAMAA TANZANIA NDIO TANGANYIKA TUSIFANYWE WAJINGA WASHATUBURUZA MIAKA 47 SASA BADO TU.


TANGANYIKA YA ZAMANI

TANGANYIKA YA SASA WAKISEMA Z;BAR DOGO
KISHA WANATAKA KUJITAWALA WENYEWE KANCHI
KADO KADO KWELI
Kama Koko Abuu Bakari ni Mwana Sheria basi kuna vipengele vya sheria
hakuvipitia vizuri? kwanza ni sheria na haki za mthulumiwa, ambao
Wzanzibar kwa mujibu wa sheria ndio wathulumiwa wakubwa tokea mwanzo wa
huo mfumo mzima na utaratibu wake wa Muungano.
Haiwi nchi dogo kama hizi MALTA, ANDORRA, LIECHTENSTEIN,  LUXEMBOURG,ziko ktk umoja wa nchi za ulaya na wanakila kitu chao na wala hawakulazimishwa kujiuga mpaka wananchi wao walipokubali ndio nchi zikajiuga sio mambo kulazimishwa tu, sasa wahusika wa Muungano ni wzanzibar
wenyewe na hawakuulizwa na hivi sasa koko Abuu Bakari sijamfahamu alipo
sema hata hio mswada wa maoni ya katiba mpya basi wananchi wataangaliwa
maoni yao? alipo ulizwa na muwakilishi wa chake chake kuwa wananchi
wakiamua kusema Muungano basi jee vipi koko Abuu? koko asema eti tutapima na
hayo maoni yenye jee vipi hayato hatarisha ulaji wetu ? maana mimi
naona koko kajibu utumbo?.
Mara zote hakuna mtoto kumzaaa mzee? sasa kati ya Wzanzibar na akina
Abuu na wenzake ipi power? mimi naona koko Abuu nimiongoni mwa watu wenye
kuhitaji sifa kutoka Tanganyika na kuwakandamiza Wzanzibar.
Maana kisheria Wzanzibar Muungano upo au haupo? Muungano mimi nahisi
haupo maana huwezi kufanya ushirika na Kombo kesho ukambiwa umefanya
ushirika na Nyange? ushirika ninao fahamu mimi ni makubaliano yani ni
(agrement) hata ndoa basi zina Agrement M/mungu katuwekea(cheti cha
ndoa) sasa na huu Muungano wetu unao Agrement kama ipo na nisikiavyo
kuwa Agrement ni kati ya Tanganyika na Zanzibar? sasa kinacho
tuchanganya Wzanzibar nikuwa leo twambiwa Tanganyika haipo ipo Tanzania
From no where?.
Sasa kweli koko Abuu Muungano ni halali? na baado tuendelee kulinda na
kuenzi? mimi nahisi koko Abuu unamsadia Aduwi na Mradi wake wakuimaliza
Zanzibar kwa jina la ubatizo Tanzania.
koko Abuu katika huo mkataba wa Muungano(Artcle of Union) kuna kipengele
gani kilicho andika Tanzania? a.) b.) Kama Muungano kisheria ni halali?
Jee ilipo vunjwa Tanganyika na Bunge la Tanganyika na Katiba ya
Tanganyika ambae ndio mshirika wa Zanzibar Memba Baraza la Mapinduzi
au   Baraza la Uwakilishi la Sasa jee Mulishauriwa kisheria au vipi na
kama mulishauriwa uko ushahidi wowote?
C.)  Kama hamukushauriwa jee Bado Muungano nihalali? na Kama nihalali
jee mkataba wa Muungano umetaja Muungano huu sasa ni wa Tanzania na
Zanzibar? Yani mkataba umefanyiwa marekebisha na Sulusi 3 za wahusika wa
pande mbili za Muungano?
Jengine ni kiungo cha Mkataba wa Muungano Arcle of Union? Raisi  Wetu
wa Zanzibar ndio kiungo kikubwa cha Muungano kwa vile Rais kapigiwa kura
na Wzanzibar ambae anawakilishi watu wake sasa kiungo cha Muungano hivi
sasa kinacho wawakilisha Watu wa Zanzibar ktk Muungano ni kipi ikiwa
Rasi wa Zanzibar states yake ktk Muungano ni Waziri asio na wizara
maalum yani hata ofisi Bara hana ya Muungano na ni mjumbe wa baraza la
mawaziri . Jee bado Muungano ni halali.......?????
Na ikiwa tuchukulie anae wakilisha Muungano ni Dr Bilali sheria gani na
ridhaa gani ya kuwawakilisha wazanzibar? kama mimi siko ktk ccm/cuf au
ktk chama chochote jee bilali kapata ridhaa gani kwangu mimi Mzanzibar
aniwakilishe wakati mimi sio ccm wala sina chama?.
Na kama Muungano koko Abuu ni halali kisheria Yapi mambo yasio ya Muungano
Bara na yanasimamiwa na katiba gani isio ya Muungano ikiwa Tanganyika
ndio haipo? b.) Jee nivikaao vingapi vilivyo kwisha kaa  Baraza au Bunge
linalo jadili mambo na rasilimali za Tanganyika lililokaa kujadili
mambo yao ya sio ya Muungano?.
Na jee koko Abuu bakari SMZ na wajumbe wa Baraza la Uwakilishi na
Wanasheria kwa vile Muungano ni halali Jee tumerizika kuwa na mshirika
mpya Tanzania badala ya Tanganyika? na kwa zamira gani na nia gani kufaa
kwa Tanganyika ikawa haitajwi wala kusikika tena kama Zanzibar lengo na
mazumuni ni nini?.
Au nikupata mwanya wa kuwa utaifa wa Zanzibar na kuwa na sera ya
serekali 1 Tanzania lakini power tafauti? Hivi sasa kilicho badilika ktk
Serekali ya Tanganyika ni jina tuu nisawa na Zaire ya zamani kuita
Kongo lakini nembo za nchi nizile zile za awali za Tanganyika kama nembo
ya Taifa ya Adam na Hawa? na Katiba ya Tanganyika ndio hii hii ya
Tanzania kuna vipengele tu flani vimebadilishwa lakini haiizuru
Tanganyika.waz;bar tunasema imetiwa viraka teleeeeeee
Jee koko Abuu na Wajumbe wa Baraza Mumerizika na mapungufu yote mazito na
makubwa kuwa bado Muungano ni halali na tuwenzi na kuudumisha? kwa nini
Tanganyika isiwepo kama kweli Muungano ni halali.
Mimi nahisi Muungano umeshapoteza uhalali wake tokea kufa kwa Tanganyika
na nyiyi viongozi au munao jita wana sheria kuna mpango wakutupeleka
ovyo kutokana na maslahi yenu mulio wekeza Bara ya kibiashara, sisi
hatuko tayari Wzanzibar kuza nchi kwa maslahi ya wafanya biashara waloko
Bara au kusema ukivunjika Muungano watakwenda wapi? warudi nyumbani
bado tunawahitajia,la kama hawataki watakuwa kama dugu zetu waliyokuweko,OMAN,U.A.E,U.K,HOLLAND,CANADA,U.S.A. N.K , jee nibora kurudi nyumbani au kubakia ugenini huko tanganyia...????
Zanzibar itajengwa na Wzanzibar wenyewe wenye ari na uchungu wa nchi yao
na kila Wzanzibar wakiondoka basi ndio hasara ya Zanzibar maana mipango
ni kuingiza wageni kwa wingi na kuua Uzawa wa Kizanzibar, Zanzibar ni
ndogo hata ukilinganisha na Mkoa wa Murogoro una watu wengi kuliko
Zanzibar kwa hio kupotea kwa Identite ya Kizanzibar nimara moja tu.
Haingii akilini kabisa kwa mtu mwenye akili timamu kuwa watu million 44
kughaghania kuungana  na watu million 1.2 nikuonyesha wazi kuwa wanalao jambo mbona hawaugani na kenya,uganda,malawi na zambia na hizi ni nchi walizo shikana nazo haswa kimipaka hii sio halali ni thulma na uonevu mkubwa.
Mungu ibariki Zanzibar na ujalie imani nzuri viongozi wetu wabadilike ili kuinusuru Zanzibar na kizazi chake kisijeuangamia na asiye badilika basi wewe muhukumu hapa duniani na kesho akhera pia kama wanavotuthalilisha sisi na wao wathalilishe hapa duniani tukiwaona na kesho akhera pia..

MAALIM SEIF AWATAKA WASOMI WALIYOKUWEKO NJE WARUDI ZANZIBAR

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Maalim Seif Sharif Hamad amewataka Wazanzibari wasomi walio nje ya nchi kuwa wazalendo kwa kurudi kuitumikia nchi yao ili kukuza maendeleo ya kiuchumi.
Alisema Zanzibar imejizatiti na kujipanga kikamilifu katika kuongeza ajira na kuboresha mishahara ya watumishi, pamoja marekebisho ya stahiki kulingana na taaluma zao.
Alitoa rai hiyo mjini Morogoro wakati wa mahafali ya jumuiya ya wanafunzi wa Kizanzibari wanaosoma Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro.
Alisema, Wazanzibari wasomi na wafanyabiashara wakubwa waliopo nje ya nchi wanao wajibu wa kutambua kuwa wanahitajika kujitokeza kutoa mchango wao kwa misingi ya kujali zaidi uzalendo wa nchi yao.
“Ndugu zangu wasomi bila kuwa na uzalendo kwenye nchi yako kwa kurudi kuwatumikia wananchi hamtakuwa mmewatendea haki pindi mtakapoamua kukimbilia kikubwa zaidi nje ya nchi yenu, hamuifanyii haki Serikali yenu,” alisema.
Alisema SMZ imedhamiria kuboresha sekta ya elimu, afya, maji, kilimo na uwezeshaji wananchi kiuchumi hususan vijana.
Aliwashauri Wazanzibari kuwashawishi watoto wao kupenda kusoma masomo ya sayansi kuanzia ngazi ya chini hadi vyuo vikuu, ili waweze kutumika katika ajira zitakazohusu fani hiyo ikiwemo udaktari.
Kwa mujibu wa risala hiyo, kati ya wanafunzi 600 wanaosoma katika Chuo Kikuu hicho, zaidi ya asilimia 40 ni kutoka Visiwani Zanzibar , ambapo kwa Julai mwaka huu wanafunzi 93 wanatarajia kuhitimu masomo yao.

UKIUTETEA/UKIAPA UTAULINDA MUUNGANO BASI NI UKAFIR

UTAKE USI TAKE HUU NDIO UKWELI

Niirejee makala yangu hii kwa kumshuru muumba wetu kwa kutujalia kuwepo katika hali hii tulio nayo hii leo,pamoja na sala na salaam kwa kipenzi chetu muombezi wetu mtume wetu Muhammad [swa]
“ Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na wakweli”TQ
Enyi ndugu zangu hivi mpaka hii leo bado tuu hatuelewi ya kwamba dhamira ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwa na dhamira mbaya juu ya nchi yetu tuipendayo ya Zanzibar? na kwanini tuutetee muungano ambao haukuwa na malengo mema kwetu? Jamani tuwe wakweli kama kweli sisi waumini, mimi naona yeyote Yule anae utete muungano huu ni adui na kafir hasa kwani huwezi ukawa unaijuwa kweli nawe kwa maksudi unapotosha kwa sababu ya maslahi yako, kufanya hivyo ni sawa na kumshirikisha Allah [Subhanah wattaallah] kama alivyo sema
“Je! Umemwona aliye fanya matamanio yake kuwa ndiye mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamwacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake, na moyo wake, na akambandika vitanga machoni mwake? Basi nani atamwongoa huyo baada ya Mwenyezi Mungu? Hamkumbuki?”TQ

Sasa jiulize jee wewe huuelewi ukweli na dhamira ya muungano huu wa Tanganyika na Zanzibar hata husomi nyakati zilivyo pia?
Jee kama kungekuwa na dhamira ya kweli kwanini tuwe kwenye mitihani kila uchwao au kukicha hebu tuamke ndugu zanguni
“Na jengo lao hilo walilo lijenga litakuwa sababu ya kutia wasiwasi nyoyoni mwao mpaka nyoyo zao hizo zikatike vipande vipande. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima.”TQ

“Je! Hawaoni ya kwamba wanatiwa mtihanini kila mwaka mara moja au mara mbili? Kisha hawatubu, wala hawakumbuki.”TQ

“Je! Mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalo burugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.”TQ

Hii yote ni uthibitisho tosha ya muungano huu haukujengwa kwenye msingi unao kubalika na ndio sababu kila uchwao unamong’onyoka, na unawafalia wale tuu wenye kufuata matamanio ya nafsi zao , naamini kabisa kama kweli muungano huu ungelijengwa kwenye msingi ya kumcha mwenye enzi Mungu { UKWELI} haya yanayo tokezea yasingelikuwapo sote tungeli utetea kwa umoja wetu sote.
“ WATAKUTOLEENI UDHURU mtapo warudia. Sema: Msitoe udhuru; hatukuaminini. Mwenyezi Mungu amekwisha tueleza khabari zenu. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wataviona vitendo vyenu. Kisha mtarudishwa kwa Mjuzi wa ya siri na ya dhaahiri; naye atakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.”TQ

Jee ndugu yangu mzanzibari hatuoni kila kukicha hawachi udhuru” mara waseme hili mara lile yote haya ni mazingatio kwetu jamani tusiwaamini hawa, hawana nia wala njia ilio njema juu yetu.

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.”TQ

Jamani tuwatenge hawa kwani lengo lao ni kuendelea kutudhulumu tuu miongoni mwetu, tunawaonea haya kitu gani hawa ni adui zetu jamani sio ndugu zetu, asilani Abadan.
“ Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya.”TQ

“ Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.”TQ

{*Jee hebu tuwatizame wote wale wanao utetea muungano wa Tanganyika na Zanzibar hawana sifa hizo, jee miongoni mwao si ndio hao wanaokula viapo vya kuulinda muungano, na kufanya ndio kinga yao ya kuendeleza dhulma ndani ya nafsi zao..?????
Jee hawa maadui zetu wote hawa amini udhalimu wa muungano huu? Wanaamini ila kwa sababu ya kukufuru kwao, wameshapingwa muhuri juu ya nyoyo zao na sasa hawafahamu chote ila matamanio ya nafsi zao tuu.






NA WENGINE WOTE MUNAJIJU AMBAO PICHA ZENU HAZIKO HAPA ILA MUME APA KUULINDA MUUNGANO NA WANGINE SASA WANAUTETE HASWA KWENYE BARAZA LA WAWAKILISHI NA BUNGENI PIA.
“ Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao. Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” TQ

Kwakweli nikiwazungumza watu hawa nitahitaji miaka na sito wamaliza ilaa natoa inzari juu ya watu hawa tujiepushe nao.
 kuwasilisha.

1) Aya 120 Surati-l-Baqara
‘Mayahudi wala manasara (wakristo) hawatakuwa radhi nawe mpaka ufuate mila yao. Sema: “Hakika ya uwongofu wa MwenyeziMngu ndio uwongofu. Na kama utafuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa MwenyeziMngu”

2) Aya ya 103 Al Imraan
‘Na SHIKAMANENI kwa Kamba ya MwenyeziMngu nyote kwa pamoja, wala MSIFARIKIANE. Na kumbukeni neema ya MwenyeziMngu iliyo juu yenu: vile mulivyokuwa maadui baina yenu wenyewe kwa wenyewe; (Yeye SWT) akaziunganisha nyoyo zenu ; kwa neema yake mukawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto, naye akakuokoeni nalo. Kwa namna hii MwenyeziMngu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka’

3) Aya ya 118 Al Imran
‘Enyi mlioamini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasiokuwa katika nyinyi (mayahudi, manasara, majusi nk) HAWATAACHA KUKUFANYIENI UBAYA. Wanayapenda yanayokudhuruni. Chuki yao imekwisha fichuka kutoka midomoni mwao (yaani kwa wanayoyasema) na yaliyojificha (yaliyomo) vifuani mwao ni makubwa zaidi (yaani haya wanayotufanyia ni madogo kulikoni hayo yaliyomo nyoyoni mwao!). Tumekwisha kukubainishieni ishara ikiwa mtayatia haya akilini.’
MwenyeziMngu atujaaaliye katika wenye kusikiza maneno Yake na kuyatekeleza kwa vitendo.
WaLlahu waliyyu tawfeeq

ASALAAM ALEYKOUM

MUUNGANO WACHOKONOLEWA MPAKA UCHOKONELEKE


Spika wa Bunge, Anne Makinda
Mjadala kuhusu kero za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, umefika pabaya, kufuatia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar na Wawakilishi, kutaka Muungano huo uvunjwe kwa madai kwamba, unawapendelea wananchi wa Tanzania Bara na kuwaacha nyuma Wazanzibari katika maendeleo.
Matamshi hayo yalitolewa na wabunge hao kwa nyakati tofauti walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, bungeni, mjini hapa jana. Mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khatib Kai, alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano, ambayo iliunda mataifa mawili yakiwa na lengo la kuunda taifa litakalosimamia maendeleo ya nchi.
Hata hivyo, alisema kinyume cha matarajio hayo, kila siku Wazanzibari wamekuwa wakinung’unika zaidi kuhusu kubanwa na kero za Muungano, ambazo kila wakati zimekuwa zikizungumzwa bungeni, lakini hadi sasa serikali haijaeleza kama zimetatuliwa au laa. “Wakati mwingi Wazanzibari wananung’unika zaidi kuliko Watanzania Bara.
Wazanzibari imefika mahali hawana imani na Muungano huu kwa sababu wao ndio walio nyuma katika maendeleo, lakini ukiangalia Tanzania inasonga mbele,” alisema Kai.
Aliongeza: “Kwa hivyo, tunachokisema na tunachokiomba ikiwa serikali hii imeona kwamba Zanzibar imekuwa kikwazo ama imekuwa kero ama mzigo, basi ni vema watuache…narudia tena kusema ikiwa Zanzibar imekuwa mzigo na imekuwa kero, basi hebu tuachieni huo mzigo, uteremsheni kichwani ili muwe huru. La, si hivyo vinginevyo, basi afadhali Muungano huu uvunjwe, uundwe tena iwapo itawezekana.”
Kauli hiyo ilimfanya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kuingilia kati na kumtaka mbunge huyo kusubiri mchakato wa kuandika Katiba mpya ili watumie fursa hiyo kutoa maoni yao.
Hata hivyo, kauli hiyo ya Spika Makinda haikufua dafu, kwani Mbunge wa Mgogoni (CUF), Kombo Khamis Kombo, naye aliposimama kuchangia mjadala huo, aliendeleza hoja ya Kai kuhusu kero za Muungano.
Alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina wizara 26, ambazo kati ya hizo, sita ni za Muungano na kusema hali hiyo inamaanisha kwamba, mambo yote, ambayo si ya Muungano, yanapangiwa bajeti ndani ya serikali hiyo.
“Mheshimiwa Spika, tuangalie kutakuwa na usawa gani katika Muungano wetu wa Tanganyika na Zanzibar?” alihoji.
Alisema licha ya kwamba mambo ambayo si ya Muungano yamezungumzwa kwenye Katiba, kimantiki hakuwezi kuwa na usawa katika Muungano kama wizara za Muungano ni sita na wizara zilizokuwa si za Muungano ni 20 na bajeti ni moja.
Kombo alisema kama kweli serikali ya Jamhuri ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo ndani ya Muungano, anaamini mapendekezo ya JFC (Kamati ya Pamoja ya Fedha) yangelifuatwa kama yalivyo, lakini hayakufuatwa.
Alisema anaamini hakuna ukweli wa dhati wa kutatuliwa kero hizo na kuitaka serikali ikae ikijua kwamba, imewafikisha Wazanzibari kuona kwamba, Serikali ya Muungano wa Tanzania inawadhalilisha.
Kombo alisema kuna wanajeshi, polisi na wafanyakazi wengine Zanzibar, ambao wanatumia huduma visiwani humo, lakini hawalipi kodi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzinbar (SMZ), badala yake kodi zao zote zinaelekezwa Serikali ya Muungano.
Alisema Serikali ya Muungano imekuwa ni ‘juja wa maajuja’ kwa Wazanzibari kwa kuifanya Zanzibar haina haki wala uwezo wa kuweza kupewa nafasi ya kuitumikia Tanzania nje ya nchi. “Tuangalie mabalozi waliopo.
Zanzibar ina mabalozi wanne tu. Na hawa wote hupangwa katika nchi za Kiarabu, nchi za Kiislamu. Isipokuwa Mheshimiwa Mapuri (Ramadhan Omar) labda kapelekwa China.
Sasa niseme kwamba, Wazanzibari nao wana haki na uwezo katika Muungano huu na wana haki ya kupewa wafanyakazi kufanya katika ofisi za kibalozi,” alisema Kombo.
Alisema kuna kamati, ambazo huundwa mara kwa mara kushughulikia kero za Muungano, ikiwamo Tume ya Jaji Francis Nyalali, ambayo alisema ilikuja na mapendekezo yake, lakini mpaka leo hawajui yalikokwenda.
Kombo alisema pia kuna kamati ya Shellukindo, lakini ripoti yake mpaka leo haijatolewa na pia kuna ya Amina Salum Ali, ambayo hadi leo haijatolewa na kuhoji: “Hivi tuamini kuna kamati gani itaweza kukaa kutatua kero za Muungano?
Kutokana na hali hiyo, alisema haamini kwamba, Serikali ya Muungano ina nia ya dhati ya kutatua kero zilizomo kwenye Muungano, hivyo, akamtaka Waziri Mkuu kusimamia jambo hilo ili lipatiwe ufumbuzi ili Wazanzibari waweze kujenga imani ya dhati.
MWAKILISHI ATAKA KURA YA MAONI
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana alishauri Serikali ya Mapinduzi kuitisha kura ya maoni itakayoamua hatma ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
Saleh Nassor Juma (Wawi-CUF) alisema kura hiyo itumike kupata maoni iwapo wananchi wa Zanzibar wanataka au hawautaki Muungano.
Saleh alikuwa anachangia makadirio ya bajeti ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Baraza la wawakilishi jana, alisema walio wengi Zanzibar wanatofautiana kuhusu suala la Muungano uliofikiwa baina ya pande hizo mbili mwaka 1964.
Alisema makubaliano ya Muungano yanainyima Zanzibar fursa ya kuongoza taasisi nyeti kama vile Idara za Polisi, Usalama wa Taifa, Jeshi na Bunge.
“Mheshimiwa Spika, iitishwe kura ya maoni haraka … Zanzibar haijawahi kuongoza nafasi ya juu katika vyombo vya ulinzi na usalama,” alisema.
Saleh alisema kuwa marekebisho ya 10 ya Katiba ya Zanzibar yameipa Zanzibar hadhi ya kuwa nchi, hivyo pia ni lazima iruhusiwe kujiunga na Jumuiya Afrika Mashariki bila kupitia mgongo wa Serikali ya Muungano.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamisi Bakari, alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni halali kwa sababu uliridhiwa na wabunge kutoka pande zote za Muungano.
Waziri Abubakari alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi, Omar Ali Sheha (CUF) wa Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.
Alisema kwamba mkataba wa Muungano uliridhiwa na wabunge wote kutoka Tanzania bara na Zanzibar jambo ambalo linaonyesha uhalali wake.
Alisema kwamba mkataba wa Muungano ulitakiwa kuridhiwa na Bunge na Baraza la Mapinduzi Zanzibar (BLM) taratibu ambazo zimezingatiwa baada ya wabunge kutoka pande mbili za Muungano kuridhia mkataba huo.
Hata hivyo, alisema kwamba jambo lolote linalotumika kwa muda mrefu bila kuhojiwa uhalali wake huwa ni halali kutokana na uwepo wake.
“Muungano ni halali kwa sababu mkataba wa Muungano ulipitishwa na wabunge wakiwemo wa pande zote kwa utaratibu uliowekwa na katiba katika kupitisha mambo ya Muungano,” alisema.
Aidha, alisema kwamba mambo yaliyoorodheshwa ya Muungano hivi sasa yamefikia 22 kutoka 11 na sio zaidi ya 30 kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Hata hivyo, alisema kwamba kwa mujibu wa katiba mambo ya Muungano hayawezi kuongezwa au kupunguzwa hadi ipatikane theluthi mbili ya wabunge kutoka Tanzania Zanzibar na Bara.
Awali, Sheha alitaka kujua taratibu gani za kikatiba zimezingatiwa kabla ya mambo ya Muungano kuongezwa kutoka 11 tangu kufikiwa kwa Muungano huo mwaka 1964.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa (Viti Maalum-CCM), Raya Suleiman Hamad, alisema Muungano wa Tnganyika na Zanzibar umeleta faida kubwa ikiwemo kujenga umoja wa kitaifa kwa wananchi wake “Leo Ndugu zetu wapo Tanzania Bara ukivunjika waende wapi, jambo la msingi ni kurekebisha kasoro za Muungano kwa sababu umeleta faida kubwa kwa wananchi,” alisema mwakilishi huyo.
Akifunga Mjadala, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alisema Muungano umeleta faida kubwa na tayari kero mbalimbali zimepatiwa ufumbuzi kupitia Kamati ya pamoja ya kujadili kero za Muungano.
Kuhusu utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar, Balozi Iddi alisema suala hilo haliwezi kutekelezwa kabla ya kufanyika marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kuwataka Wajumbe wa Baraza hilo kuwa na subira wakati serikali ikiendelea kulitafutia ufumbuzi

huyu koko Abubakari Khamisi Bakari anauhalalisha muungano ati ndio mwanasheria huyu mnafki ni mnafki tu na wewe Raya Suleiman Hamad ushashiba batata za urojo nini sasa hujuwi wasema nini sio.ati dungu zetu bara watakwenda wapi kwani walikuwa wapi..?na kuvunjwa kwa muungano sio kufukuzwa watu kwenye nchi wacheni ujinga mimi nauliza haswa hawa majuha nani anawapa uwaziri hawa watu hawajuwi lolote.ati waziri hahahaahah ulaya kabla haijaungana kuna wajerumani wanaishi ubeligiji na kuna wabeligiji wanaishi ufarasa na hawakufukuzwa na sasa nchi zao zimeungana wanaendeleya kuishi na ukivunjika wataendeleya kuishi sio kuwa muungano ukivunjika ndio kila mtu afunge begi lake arudi kwa sio hivyo wewe zoba raya suleiman hamad dungu zetu wakitaka kuridi poa ndio kwao hawataki watakuwa na paspoti za kitanganyika na wakitaka kuja nyumbani watatambulika kama watanganyika watakuwa na urai wa tanganyika kama dungu zetu wenye urai wa U.K,UHOLANZI,UBELIGIJI,OMAN,U.A.E. NK na wao watakuwa kama hivyo kasoma tena ndio uwe waziri wewe balozi iddi huna mpango wowote sisi tunakujuwa wewe umeletwa znz ili kuzuwi muungano ila sisi tutapingania muungano na ukivunjika basi wewe uweko bara kwenu ikiwa hapa z;bar ili jela ya kilimani ndio nyumba yako ya mwisho usitulete mambo ya katiba wala ukwaju hapa katiba katiba unaijuwa katiba wewe..?

ABUBAKARA KHAMIS BAKARI MNAFKI TU NA MNAFKI NI MNAFKI TU HATA AJIFICHE UTAMJUWA TU.


KUMBUKA UME APAA NA MSAHAFU UKASHIKA KUWA UTASEMA KWELI NA SASA UNASEMA MUUNGANO NI HALALI NA UNAJUWA KAMA SIO HALALI CHEO TU HICHI LEO UNACHO KESHO HUNA AU KABURINI

Alivyo sema kuwa aliposema Maali Seif kuwa hajaona mrisi ktk walomzungumko kumbe kweli alikwisha washtukizia kuwa harakati za wenzake ni kwenda mbio na mloo tu.
Wzanzibar wengi wamepigwa na butwaa bada ya kumuona  Abubakar Khamis
Bakari kuwambia Wzanzibar ktk BLW kuwa kisheria Muungano ni halali kwa
vile Baraza la Mapinduzi limekubaliana.
Sasa mimi sio mwana sheria kama Abuu? lakini ni Mzanzibar jee kama
Muungano Abuu ni halani kwa makubaliano ya Baraza la Mapinduzi wakati
huo? Swala ni hili misingi yakuunganishwa haikuwashirikisha wananchi wa
Zanzibar.
Jee Wzanzibar kisheria sasa hivi wakiamuwa kuuvunja ni halali au mpaka
Baraza la Sasa la Uwakilishi likubali? swali la pili znz wakati wa karume haikuwa na katiba sasa nchi mbili zitaunganishwa vipi wakati moja inakatiba na nyengine haina..? Maana naona hivi sasa
tushanyaganywa akili na viongozi wetu tena wa CUF akina Abuu.
Juzi alipokuwa njee ya Serekali alikuwa msemaji mkubwa wa Wzanzibar na
tulipo mwaga damu na kupoteza watoto wetu wabichi 26/27 ili tupate
watetezi wa kizazi cha Zanzibar tukapapatuwa mpaka  Abuu ukaingia ktk
uliongo? lakini leo ametugeuka na kuhalalisha batli ili tu awarithishe mabwana wake
Tanganyika nao   kwa kumsifu kuwa abuu abuu wewe ni Goodboy?.
Hii ndio inayo turudisha nyuma Wzanzibar, tumesha poteza watoto wetu na
nguvu zetu leo kibaraka Abuu katuacha mkono anasema Muungano ni Halali , mimi
naona koko Abuu unatuchanganya hujatwambia ukweli halisi na kama Muungano
ni halali mbona kuna maswali mengi yasio na majibu?.
Mh mkuu wa Zanzibar ktk kesi ya Muungano kasibitisha wazi kuwa Hakuna
mkataba wa Muungano ofisini kwake Jee unasemaje haya kitumwa cha watanganyika  Abuu niuongo au kweli? kama sio kweli kitumishi Abuu wewe binafsi unao ushahidi wowote unao halalisha Muungano kuwa Halali?.
Sio utwambie kuwa ooh nihalali kutokana na kuwa upo muda mrefu bila
manuguniko au ni halali kwa vile ni muda mrefu na watu wako kimya, mimi
sikubaliani na wewe kwa hili na umejivunjia hishema kwa waz;bar  abuu usituchafuwe,
miaka 47 sasa Wzanzibar wana-struggle kunugunikia Muungano
tume-sacrifice  kila kilicho chetu mpaka ukaweza kuingia hapo kwenye
ulingo leo unatuletea maneno ya kejeli na uchale.
Hatuko radhi na wewe na tunakuisabu kuwa ni miongoni mwa wanafiki wasio
ipendelea  Zanzibar kuwa huru nchi huru bila ya kutawaliwa na mkoloni mweusi na wewe nikatika waliokuwa tayari wamesha kula
hasara kama wale wanao pewa Viwanja na Wake Bara wakaukana Uzanzibar na
wakashirikiana na Shetani.
Hivi ndivyo tunavyo jimaliza wenyewe Wzanzibar mtu akiwepo nje hutetea
Zanzibar na huwa ktk Shangwe la wananchi akisha kamata tawi basi sio
tena mwenzako shame on you Abuu kifu tundu.

ZOP YAISAIDIYA VITANDA HOSPITALI YA MNAZI MOJA


Ahsanteni kwa msaada




Hoteli ya Serena Inn ya Zanzibar kupitia Jumuiya isiyo ya
kiserikali, Zanzibar Outreach Program (ZOP) inayojishughulisha
 na huduma za jamii,
imekabidhi msaada wa vitanda 14, magodoro na vifaa vingine
 vyenye thamani ya shlinngi milioni 55 vilivyotolewa msaada
 kutoka Hospitali ya St. Jude ya Uingereza kwa ajili ya
Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ya Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar,
 Dk. Malik Abdallah Juma (wa pili kupia), Mwenekiti wa
 bodi ya wadhamini wa ZOP, Maalim Mohammed Idrissa,
 na Meneja wa Serena Inn Daniel Sambai na wafanyakati
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye sherehe ya
 makabidhiano iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena Inn
 Mjini Zanzibar
HOSPTALI ya Rufaa ya Mnazimoja leo ilipata vitanda
 maalum 14 vya wagonjwa ili kuongeza mahitaji ya
 vifaa hivyo kwa wagonjwa.
Vitanda vyenye thamani ya shilingi milioni 55.4 ni
msaada wa taasisi ya kiraia iitwayo
 Zanzibar Outreach Group (ZOP) kwa wagonjwa
wanaolazwa hospitalini hapo.
Mkurugenzi wa ZOP, Kuki Aggarwal, alisema wakati
wa makabidhiano ya vifaa hivyo kuwa, vitanda hivyo
 vimetolewa kwa taasisi yake na Hospitali ya
St Jude ya Uingereza, kupitia
Aga Khan Foundation huko Zanzibar.
Aggarwal alisema taasisi yake imeamua kutoa
vifaa hivyo kwa Hospitali ya Mnazimoja chini ya
utekelezaji wa mpango wake endelevu wakusaidia
sekta za huduma za afya, maji na elimu.
Msaada wa vitanda hivyo ulikabidhiwa kwa
 Mkurugenzi Mkuu wa Afya katika Wizara ya
Afya Zanzibar, Dk Malick Juma na Meneja wa
Hoteli ya Serena, Daniel Sambai.
Akiipongeza taasisi ya ZOP kwa msaada huo,
 Dk Malick alisema vitanda ni miongoni mwa
mahitaji muhimu kwa hospitali hiyo ya Mnazimoja
 yenye jumla ya vitanda 400.
Hata hivyo, Dk. Malick hakueleza kama
Hospitali ya Mnazimoja ina upungufu wa vitanda
 au imejitosheleza kwa mahitaji hayo, lakini
 hospitali hiyo hivi sasa inakabiliwa na ukosefu
wa vifaa muhimu katika chumba cha wagonjwa
 mahututi (ICU) bvaada ya mashine zote za tano za
 kusaidia wagonjwa kupumua kuharibika tangu mwaka jana
nivizuri kusaidiya maana hospitali ya mnazi moja
 sio hospitali ni gereji haswa na haya yote yanaletwa
 na mawaziri wasio na huruma wako wapi mawaziri
 wa afya na manaibu wake wanafanya nini...? kuiba
na kujaza matumbo yao toka bajeti itoke mbona hatujawasikia...?

Tuesday, June 28, 2011

MAMBO 11 WALIYOKUBALIANA SERAKALI YA Z;BAR NA TANGANYIKA 1964 NYERERE NA MZEE KARUME NI HAYA TU.


Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakar Khamis Bakari
ameyasema mambo kumi na moja waliyokubaliana serekali ya tanganyika na zanzibar ni

Abubakar aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba wananchi wengi hawaujuwi mkataba wa Muungano wa asili amabpo mwaka 1964 mkataba wa Muungano uliorodhesha mambo 11 ya awali ikiwemo katiba ya Jamhuri ya Muungano, mambo ya nje, ulinzi na usalama, polisi na mamlaka juu ya mambo yanayohusu hali ya hatari.
Mambo mengine ni uhamiaji, mikopo na biashara za nchi za nje, utumishi katika serikali ya Muungano, kodi ya mapato na ushuru wa forodha na bandari, usalama wa anga, posta na simu.
1)KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO.
2)MAMBO YA NJE.
3)ULINZI NA USALAMA.
4)POLISI NA MAMLAKA JUU YA MAMBO YANAYOHUSU HALI YA HATARI.
5)UHAMIAJI.
6)MIKOPO NA BIASHARA ZA NCHI ZA NJE.
7)UTUMISHI KATIKA SERIKALI YA MUUNGANO.
8)KODI YA MAPATO NA USHURU WA FORODHA NA BANDARI.
9)USALAMA WA ANGAA.
10)POSTA
11)SIMU
sasa haya ndio mambo tuliyokubaliana na serekali ya tanganyika na sio sisi tuliyokubaliana ni nyerere na mzee karume maana mzee karume hakuwashauri mawaziri wake wala hakuwauliza wananchi wake iliungana kwa uwonga wake na uroho wake wa madaraka ili asipinduliwe nyerere alikuwa akimtisha utapinduliwa wee utapinduliwa.sasa swali ni hili katiba ya jamhuri ya muungano sote tunajuwa ni katiba ile ile ya tanganyika ndio iliyogeuzwa na kuwa ya jamhuri ya muungano sasa muungano huwo vipi maana wakati wa mzee karume kama alikuwa na katiba yake kwanini haikuwekwa ktk ile ya tanganyika kisha ikaundwa katiba moja..?
mambo ya nje toka 1964 mpaka leo mambo ya nje yanafanywa na watanganyika ni nani na nani znz aliyekwenda nje nakusema mimi natokeya ktk serekali ya znz nimekuja kuiwakilisha ktk mambo ya nje nani...?
ulinzi na usalama ooooyee tunauwona ulinzi na usalama kila siku tunaingiliwa na majambazi,wizi,vibaka,na siku jeshi au polisi wakilewa wanapinga watu kama hawana akili vizuri na siku za chaguzi watu wanauliwa hatharani na wengine kisirisiri je ulinzi na usalama huo uko wapi..?
polisi na mamlaka juu ya mambo yanayohusu hali ya hatari naona hapa znz hakuna hata hali ya hatari zaidi ya kuingiliwa na majambazi na polisi hawawakamati hao majambazi wala wauza unga wameja kila kona na hao hao polisi ndio wanaopiga rai sasa wa ndio hatari au..?
uhamiaji kwanza hawatupi sisi rai wa znz paspoti mpaka uliwe millioni na usheya pili watu wanaingia znz kama danguroni hakuna lolote uhamiaji imeka kula pesa za haramu za paspoti na kuzuia mizingo ya wafanyabiashara masikini za mungu je ndio uhamiaji hiyo...?
mikopo na biashara za nchi za nje hakuna mkopo unaokoja znz wala znz haitambulika nchi za nje kama serekali sasa nani ataipa mikopo na biashara nchi za nje ni karafu na imethibitiwa na wajuku wa karume ZSTC mwananchi habuwi kitu mpaka asafirishe magendo karafu zake mwenye kuza kwa mangendo je ndio mikopo hio na biashara nchi za nje ilivyo...?
utumishi katika serekali ya muungano ahahaha bora nicheke maana wacha serekali ya muungano hata serekali ya zanzibar basi sio wazanzibar itakuwa serekali ya muungano kwali..?
kodi ya mapato na ushuru wa forotha na bandari ndio mukatuletea TRA-HIV/AIDS sio ijekutumaliza maana munakusanya mapato na kodi za bandari ya zanzibar ila pesa hazionekani zote zinaishia katika matumbo yenu watanganyika au munakata..?
usalama wa angaa hahaha sijaona hata siku moja znz kuwa na denge za kijeshi labda bara sasa ikiwa tutashambuliwa tuwapingiye simu nyinyi kwa vodacom kisha ndio muje na denge zenu mutuhami sio..?mumusikia wapi upumbavu huu..?
posta mawe unatuma baruwa dar mpaka znz inachukuwa miazi 3 na hio ikifika ni salama yako kwanza baruwa munazifunguwa na kuiba kila kilichomo ndani ya barua nani asiyeyejuwa haya munafikiri zanzibar wanahaja sana ya posta..?
simu na umeme ni sawa sawa unapiga dakika 3 unaletewa bili millioni moja nani mwenye haja ya simu ya nyumbani miaka hii ni komputa na simu za mkononi tu hakuna tena simu za ndani au munataka kusikiliza watu wanasema nini katika simu...?

mimi naona mambo yote 11 ni upumbavu mtupu haya znz tunaweza kufanya wenyewe bila ya muungano na wala hatuna haja ya muungano kwanza TRA ikiondoka vijana wengi watapata kazi polisi machogo na majeshi machongo wakirudi kwao wengi vijana znz watapata ajiri ya kuilinda nchi yao na kuihami nchi yao bandari itakuwa bandari huru znz itainuka na itakuwa watu wote wanakazi sio sasa vijana wote bangi,unga mtu hatuna haja ya muungano nauvunjwe nauvunjwe nauvunjwe

DODOMA KUNA MOTO UNAWAKA JE UTAENDELEYA KUWAKA AU NI WAKIFU TUNDU TUU..?



HILI NDIO BUNGE LA DODOMA LILIVYO KAA KTK NYOYO ZA WANANCHI NA NDIO NYOYO ZA WABUNGE ZILIVYO KAA KWA KUWADIDIMIZA RAI WA NCHI HIZI MBILI NA KULAZIMISHA MUUNGANO AMBAO TUSHAUKATA WAZANZIBAR WOTE HATUTAKI KAMA KUNA MTU ZNZ ANASEMA ANATAKA MUUNGANO NI MTU KUTOKA BARA TUNAWAJUWA MZANZIBAR HALISI HANA HAJA YA MUUNGANO FEKII ULIYOJA VIRAKA.
Mbunge ailipua Ikulu
AHOJI SABABU ZA KUTENGEWA MABILIONI KILA MWAKA, MUUNGANO NAO WATIKISA BUNGENI
Kizitto Noya, Dodoma
MBUNGE wa Chadema, Suzan Lyimo ameishangaa Serikali kwa kutenga mabilioni ya fedha kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam kila mwaka, huku Serikali hiyo hiyo ikiendelea kusisitiza mikakati ya kuhamia Dodoma.
Akichangia mjadala wa bajeti kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na ofisi zilizopo chini yake, kwa mwaka wa Fedha 2011/12 jana, Lyimo alisema haungi mkono hoja hiyo, mpaka apewe majibu ya kuridhisha ya sababu za Rais kushindwa kuhamia Dodoma na badala yake kuendelea kutenga kiasi kikubwa cha fedha kukarabati Ikulu ya Dar es Salaam.
Akitoa takwimu mbalimbali za bajeti ya Ikulu tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2011, Lyimo alisema kwa kipindi hicho cha miaka kumi, Ikulu imekwishatengewa zaidi ya Sh50 bilioni, fedha ambayo kwa maoni yake, zinatumika vibaya.
“Siungi mkono hoja hii kwa sababu tatu; moja ni ukubwa wa Baraza la Mawaziri, mbili uonevu wanaofanyiwa wanafunzi wa elimu ya juu na tatu Serikali kutokuwa na mpango wa dhati wa kuhamia Dodoma,” alisema Lyimo alipoanza kuchangia mjadala huo.
Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Viti Maalumu, kitendo cha Serikali kuendelea kuliomba Bunge liidhinishe matumizi ya Sh10 bilioni kwa ajili ya ukarabati wa Ikulu ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwaka 2011/2012, kinaonyesha kuwa haina nia ya dhati wala utashi wa kisiasa kutekeleza mpango wa kuhamia Dodoma.
“Tangu mwaka 2001 hadi 2011, Ikulu hiyo imetengewa Jumla ya Sh56 bilioni. Kila mwaka Serikali inaomba Sh2 bilioni, mwaka jana iliomba Sh7.2 bilioni na mwaka huu imeomba Sh10 bilioni,” alilalamika Lyimo na kuendelea:
“Hivi ni kweli mabilioni hayo yanatengeneza Ikulu ya Rais tu pale Dar es Salaam? Na kama kweli ni Ikulu, kwa nini isitengenezwe Ikulu ya Chamwino ili Rais ahamie Dodoma?” alihoji
Lyimo alisema haoni mantiki kwa Rais kuendelea kuishi Dar es Salaam wakati mpango wa kuhamia Dodoma ulianza tangu mwaka 1976 na kila mara Serikali imekuwa ikiendelea kusisitiza mpango huo.
“Mheshimiwa mmoja hapa alipendekeza Spika ahamie Dodoma, mimi nasema sio Spika ni Rais ndiye anayepaswa kuja Dodoma. Na kama Rais anahamia Dodoma hakuna waziri atakayebaki Dar es Salaam. Tunamtaka pia Waziri Mkuu kuja Dodoma,” alisema.
Baraza ni mzigo
Kuhusu Baraza la Mawaziri, Lyimo alisema ni kubwa kupita kiasi na kwamba Serikali inapaswa kulipunguza ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima serikalini.
Alisema mawaziri 54 waliopo sasa, ni wengi mno na wanaiongezea mzigo wananchi ambao ndio wanaobeba jukumu la kuigharimia Serikali yao.
“Baraza la Mawaziri ni kubwa mno, wako 54 ukimjulisha na Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar. Nchi tajiri kama Marekani ina mawaziri 15 tu, kwa nini Tanzania ambayo ni maskini iwe na mawaziri wote hao?” alihoji na kusisitiza, “tunaomba Serikali iliangalie upya baraza lake la mawaziri.”
Katika hoja ya uonevu aliodai unafanywa na Serikali kwa wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Lyimo alihoji sababu za wanafunzi kufukuzwa baada ya kufanya migomo na maandamano wakati kisheria, inaruhusiwa vyuoni.
Muungano watikisa
Katika hatua nyingine, hoja ya Muungano jana ilitawala mjadala huo unaoendelea bungeni baada ya wabunge kadhaa kutoka Zanzibar, kueleza kuwa bado una kero nyingi na hivyo kupendekeza uvunjwe.
Wakichangia mjadala huo kwa nyakati tofauti, wabunge hao walisema Muungano bado ni kero kwa Wazanzibari kwa kuwa kuna mambo mengi ya msingi ambayo yanatendeka bila kujali maslahi ya pande zote mbili.
Mbunge wa Mgogoni, Kombo Khamis Kombo alihoji namna haki inavyoweza kutendeka katika mazingira ya nchi hizi mbili kuungana kwenye wizara sita tu kati ya wizara 26 zinazounda Serikali ya Muungano.
“Seriklai hii ina wizara 26 na wizara za Muungano ni sita tu. Mambo yote yanayofanywa kwenye wizara ambazo sio za Muungano bajeti yake inapangwa na kutekelezwa na Serikali ya Muungano, sasa licha ya jambo hilo kuwa kikatiba, kutakuwa na usawa gani kati ya Zanzibar na Tanganyika?” alihoji.
Mbunge huyo alisema haamini kama Serikali ya Muungano ina nia ya dhati katika kutatua kero za muungano na kama ina nia ya kweli, iwajengee imani Wazanzibari kwa Waziri Mkuu kuzungumzia kero hizo wakati anajibu hoja za wabunge katika mjadala unaoendelea.
“Mheshimiwa Spika, katika mazingira haya, tunawahakikishia Wazanzibari kuamini kuwa Tanganyika (Tanzania Bara) inawadhalilisha. Zanzibar kuna mabalozi wanne tu tena wanapelekwa kwenye nchi za Kiarabu na sasa China amepaelekwa mheshimiwa Mapuri. Wazanzibari wana haki, uwezo na haki ya kupeleka wafanyakazi katika balozi,”alieleza.
Kombo alisema kitendo cha Serikali kupuuza mapendekezo ya kamati ya Nyalali, Shelukindo na Amina Salum Ally kuhusu kero za Muungano ni ishara tosha kwamba haina nia ya dhati kutatua kero hizo zinazolalamikiwa na Wazanzibari.
Maelezo hayo yaliungwa mkono na mbunge wa Micheweni (CUF), Haji Khamis Khai aliyeeleza kuwa Wazanzibari hawana imani na Muungano huo kwa kuwa wao ni maskini kuliko Tanzania Bara.
“Kama Zanzibari ni mzigo kwenu (Bara) tuvunje muungano huo, mtuache,” alisema.
Alisema inaudhi Wazanzibari kuzungumzia kero za Muungao kila siku na Serikali ya Muungnao ikiendelea kuwa kimya bila kutoa kauli inayotekelezeka.”Tunaomba Muungano uvunjwe na uundwe tena kama ni lazima,” alisema.
Hii ni mara ya pili kwa wabunge kujadili hoja ya Muungano katika Mkutano huu wa nne unaondelea sasa. Mara ya kwanza hoja hiyo iliibuliwia na mbunge wa Chwaka (CCM), Yahya Kassim Issa ambaye aliliambia Bunge kwamba Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar, bado una sintofahamu nyingi.
Akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Matumizi ya Fedha ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge ya mwaka 2011/2012 jana, mbunge huyo alisema suala la Muungano bado lina utata unaopashwa kushughulikiwa haraka.
“Mheshimiwa Spika, Wakati Rais akitolea ufafanuzi suala hilo la Muungano alieleza kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya nchi ya Tanzania lakini, Nje ya nchi, nchi ni Tanzania. Lakini mheshimiwa spika, mpaka leo vitabu hivi, bado vinaitambua Zanzibar kuwa ni mkoa kama ulivyo Kilimanjaro!”
“Mbona vitabu havitoki kubadilisha hilo ili Zanzibar isomeke kuwa ni nchi kama Rais alivyosema? Huu ni mzozo, Zanzibar kuonekana kama mkoa na sisi (Wazanzibari), hatutaki,” alisema mbunge huyo.
NCHI MASIKI ONA YALIVYOVIMBA KAMA MAKOBE MIMBA

LEFT BEHIND- a fathe hold his baby after wife died in childbirth in moshi,Too many die,too young,said a doctor worried about maternal deaths.
KIKWETE IWACHE Z;BAR USHUGHULIKIYE WANANCHI WAKO WA
TANGANYIKA
FAIDA ZA BONGE LA DODOMA SASA TUNAJENGA NYUMBA ZA GHOROFA
DODOMA HIYOOOOOOOOOOO
HAWA BATHI YA WABUNGE WETU WANAWAOGOPA HAWA WANYE MASHATI YA KIJANI KAMA WAKULIMA WA MACHAKOS
IKISHA WANANCHI WANAULIZA PESA ZA NCHI ZINAKWENDA WAPI WANGALIYE WALIVYO NDIO JAWABU LAKO WAPI PESA ZINAKWENDA
DODOMA OYEEEE DODOMA OYEEE  OYEEEE
KILA MOJA ANAJARIBU KUMZIDI MWENZAKE ILI ATAWALE APATE KUIBA ZAIDI
ONA ILIVYO VIMBA KISHA ATI NCHI MASIKINI MAWEEEEE
WENGINE WASHALICHUNGULIA KABURI LAKINI BADO WAMO
WAKIJADILIYANA JINSI GANI WATAIMALIZA ZANZIBAR
MOJA KTK VIONGOZI WA Z;BAR MAKOKO WA KUJITAWALA WANYEWE WANATAKA KUTAWALIWA MPAKA KIYAMA KISHUKE NDIYE HUYU KOKO OMAR MZEE
WOTE WANAMIMBA ONA MATUBO YALIVYOWAKOBOKA