Monday, November 23, 2015

MAANDAMANO YA WAZANZIBARI WAISHIO NCHINI MAREKANI YAFANYIKA NA KUTAKA RAISI ALIYE SHINDA UCHAGUZI NCHINI ZANZIBAR ATANGAZWE


Mpenda amani na Demokrasia Bwana Thuweni akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia  Yussra Alkhary akionyesha bango Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Wanachama wa ZADIA kutoka majimbo tafauti Nchini Marekani wakionyesha mabango yao

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji, akiongea na moja waandishi wa habari.

Pichani ni Bango la waandamanaji wa Zadia nchini marekani

Wapenda amani na Demokrasia wakiwa na mabango yao Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)


Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)

Mpenda amani na Demokrasia wa (ZADIA) wakipata picha Njee ya makao makuu ya Ikulu ya Marekani (White House)

Na Mwandishi wetu aliyepo jijini Washington nchini Marekani

Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya nchi ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo ya Marekani ambayo ndio wanayo ishi katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati ya kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo ulio fanywa kwa makusudi ili kuikandamiza nchi ya Zanzibar.Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo ya kutafuta uingiliaji kati ya kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisiasa nchini Zanzibar.Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika.“Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema ‘.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma’..”, alikumbusha Bwana Ali.Aliongeza kuwa “Wananchi wa nchini Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa”

Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa nchini Zanzibar, Bwana Ali alisema “Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini ((Tanzania)) ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa nchi ya Zanzibar ulikuwa wa haki na huru” Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwenye Umoja wa Mataifa.Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile “Mshindi wa uchaguzi atangazwe”, “maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe”, “bila haki hakuna amani’ na mengineyo.

Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai “tunataka matokeo yetu ya uchaguzi..”
Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema “Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na nchi yetu ya Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao”Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)  Jecha Salum Jecha kwa ukereketwa wake na kutaka kuipendelea chama chake cha CCM akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu nchini humo Zanzibar, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya nchi ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa nchi ya Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa nchini humo Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchi humo Zanzibar.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani tafauti na nchi ya Tanganyika inavyotaka kumaliza mzozo huo kwa kutumia majeshi na fifaru ilivyo vipeleka nchini humo baada ya kuona chama chao cha CCM KIMESHINDWAAAAAAA.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment