Monday, November 9, 2015

NCHINI ZANZIBAR MAWAZIRI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF WAMERUDISHA MAGARI YA SEREKALI


Mwanasheria gwiji nchini aliyeongoza timu iliyoandika Katiba ya Zanzibar mwaka 1980, Aboubakar Khamis Bakary ametangaza rasmi kuwa mawaziri wote katika serikali ya Dk. Ali Mohamed Shein wanaotoka CUF wameshakabidhi ofisi na gari serikalini.Aboubakar ambaye alikuwa akiongoza wizara ya Katiba na Sheria, amesema wametekeleza hatua hiyo ya kisheria baada ya uongozi wa serikali ya Dk. Shein kumaliza muda wake rasmi ilipofika Novemba 2 mwaka huu.Alisema kwa mujibu wa Kif. 28 cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais Dk. Shein alikamilisha muhula wa miaka mitano tarehe hiyo na mtu yeyote anayetafsiri vinginevyo katiba, anafaa kuitwa “mbumbumbu wa sheria.”
“Mimi ni mwanasheria na mtaalamu hasa wa masuala ya katiba na hakuna wa kunidanganya. Wanaosema rais Dk. Shein anaongoza kihalali eti kwa kuzingatia kifungu cha 28, hawajui wanachokifanya, au wanapotosha makusudi ukweli ili kukidhi matakwa yao binafsi,” amesema Aboubakar.Amemsihi Dk. Shein azingatie katiba badala ya kusikiliza viongozi wa CCM ambao alisema wanatafuta njia ya kutengeneza mgogoro mwingine wa kisiasa Zanzibar baada ya kushindwa uchaguzi. “Lazima tufike mahali tuithamini demokrasia tuliyoamua kuijenga. Haikubaliki kuwasumbua wananchi wa Zanzibar kwa uchaguzi ambao baadhi yetu wanasiasa hatuko tayari kupoteza madaraka, hii si sahihi hata kidogo,” amesema gwiji huyo wa sheria aliyekuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Zanzibar baada ya Zanzibar kupata katiba yake ya kwanza tangu ile iliyovunjwa na Mzee Abeid Amani Karume mwaka 1964 yalipofanyika mapinduzi.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment