Walichosema ZLS
Kwa mujibu wa Rais wa ZLS, maudhui ya Ibara 28 (1) hiyo ni kumpa uwezo wa kikatiba Rais kuendelea ili kutoa nafasi ya maandalizi ya kula kiapo kwa Rais anayefuata tu na si kuendelea kukaa madarakani bila ya kufanyika kwa uchaguzi au kwa sababu ya Uchaguzi kufutwa. Hata hivyo Said alisema nchi kuendeshwa muda mrefu bila ya Baraza la Wawakilishi (MBW) kama mazingira yaliyopo yanavyoonyesha ni tatizo. Alisema Katiba ya nchi ya Zanzibar imeruhusu hali ya kuendesha nchi bila ya BLW kwa muda usiozidi siku tisini (90) tu kuanzia siku Baraza lilipovunjwa. “Kwa mazingira tuliyonayo, siku tisini (90) zinazokubalika kikatiba zinaishia Novemba 12, 2015 kwa kuwa BLW lilivunjwa Agosti 13, 2015,” alisema.
Rais huyo wa TLS alionyesha pia hatari ya kuwa na rais ambaye yuko juu ya Sheria na Katiba, akibainisha Ibara ya 37 ya Katiba ya Zanzibar ya 1984 inayoipa Mamlaka Baraza la Wawakilishi kuondoa kinga ya Rais kutoshtakiwa anapokuwa madarakani kama inavyotolewa na Ibara ya 36 ya Katiba.Alisema katika mazingira yaliyopo hivi sasa ambapo ifikapo tarehe 12 Novemba, 2015, Baraza la Wawakilishi halitakuwapo na haliwezi kuitishwa kikatiba, ni wazi kuwa ikiwa Rais atafanya matendo yoyote yenye kuvunja katiba ya nchi na kukiuka kiapo chake, hakutakuwa na mamlaka nyingine yoyote yenye uwezo wa kuhoji matendo ya Rais.
Alidai hii inatoa fursa na inatengeneza hatari ya kuwa na Serikali inayoongozwa na ‘dikteta’.
No comments:
Post a Comment