Sunday, November 15, 2015

SHAKA USISAHAU KUMUAMBIYA NA POMBE MAGUFULI KUWA KURA ZAKE PIA ZANZIBAR ZEMEFUTWA NA UCHAGUZI UNARUDIWA KWA HIYO NA POMBE MAGUFULI AJIANDAE NA UCHAGUZI MPYA ZEC ITAKAPO TANGAZA


SHAKA UMESOMA SHERIA...? HAYA BASI BISHANA NA HAWA WANASHERIA WENZIO BASI UZIDISHE UHONDO
IMG-20151115-WA0000
Umoja wa Vijana wenye njaa wenyekutafuta ruzuku kwa kutumia Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),atii umewataka vijana Zanzibar kutobabaishwa na kuendelea kwa mjadala au mazungumzo ya viongozi wa kisiasa kuhusu matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ambao umefutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).((wambiye basi watu umefutwa kwa sheria ipi au kipengele kipi cha katiba kilicho mpaa uwezo jecha kufuta usiseme domo tupu.
UVCCM imesema mazungumzo hayo ni sehemu ya harakati za kuhakikisha amani inaendelea kuwepo nchini na kwamba hayawezi kubadilisha uamuzi wa ZEC katika uchaguzi huo.Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema hayo jana katika mkutano wake na wajumbe wa umoja huo na viongozi wengine wa CCM ngazi za kata, majimbo na wilaya kwenye ukumbi wa CCM Dimani, katika Mkoa wa Magharibi Unguja.Alisema Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar ni mchakato unaosimamiwa na Sheria ya Uchaguzi, hivyo hakuna yeyote mwenye mamlaka wala madaraka ya kuiingilia ZEC, kuipangia au kulazimisha ipindishe sheria kwa maslahi ya wachache. ((je ZEC imepewa mamlaka na nani kuvunja katiba ya Zanzibar au imefanya hivyo kwa maslahi ya Mr and Mrs BT...?))

“Kukaa kwetu kimya haimaanishi kwamba sisi si weledi wa kusema na kujipamba kwa sifa na majigambo yasiyo na maana katika jamii, tunataka tutofautishwe kati ya wanaojua na kuheshimu nguvu ya sheria na wale wanaoropoka hovyo bila kujali maslahi ya nchi,” alisema.((wewe kweli sumuni,bukmuni,umiyuni.))

Katibu Mkuu huyo aliwaeleza wanachama hao wa CCM kwamba, tangu ZEC itangaze kufuta matokeo ya uchaguzi huo, kumekuwa na kauli mbalimbali za kibabaishaji kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani, akiwemo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

“Hatushindwi kumjibu Maalim Seif, chama chake na wote wanaomuunga mkono, tunachelea kuonekana mbumbumbu mbele ya waerevu,” alisema Shaka.((si haba kuwa mnajijuwa kuwa ni maa MBUMBUMBU.))
  
Alisema sheria inampa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi kama alivyofanya.((tuambiyeni basi ni sheria ipi iko wapi kifungu kipi katika katiba ya Zanzibar pahali gani panapo mpaa haki jecha kufuta uchaguzi uliokwisha kamilika sio mnasema tu sheria sheria na mkae mkijuwa kama uchaguzi wa Zanzibar umefutwa basi na Pombe Magufuli atakuwa sio rais halali maana kura zimepigwa siku moja zikahisabiwa siku moja sasa itakuwaje Pombe Magufuli kura zake ziwe halali na zengine ziwe sio halali na kufutwa wakati zimepigwa siku moja mutupe jibu...?)) baada ya kugundua kukiukwa kwa taratibu.Kwa mujibu wa Shaka, baada ya uamuzi huo anaepita mitaani na kusema anasubiri aapishwe awe Rais wa Zanzibar wakati Ikulu ipo chini ya rais halali kisheria,((sheria ipi basi shaka iliyo mpaa uhalali rais abaki ikulu mbona huzitaji hizo sheria umegangana tu sheria sheria maskini hujuwi mbele ni wapi wala nyuma ni wapi upo na maradhi ya BT yanakusumbuwa.)) huyo anaota mchana na anajiweka wazi jinsi alivyo na uchu wa madaraka.((na wewe shaka unajiweka wazi kuwa unawazimu wa akili na pia unaungwonjwa wa BT unakusumbuwa.))

Aidha, alisema mivutano itokanayo na utata wa kisheria haitamalizwa na vinywa vya wanasiasa wenye tabia ya kukanyaga sheria au kubeza matakwa ya katiba. ((alaa shaka pia wewe wajuwa kuwa kuna katiba jitahi baba utaelewa tu.))Kwa mujibu wa shaka, sehemu yoyote inayohitaji msaada wa mazungumzo, ni jambo la kawaida kwa wanasiasa na viongozi kukutana, ingawa hatua hiyo haihalalishi kuvunjwa kwa sheria na katiba ya nchi.Shaka alisema uendeshaji wa nchi yoyote duniani, husimamiwa na kulindwa kisheria na katiba, hivyo kinaweza kuwa kituko iwapo mwanasiasa atadhani kwa kushinikiza jambo, anaweza kupewa nafasi ya uongozi wa juu wa nchi.

“Iwapo ZEC imefuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu kutokana na uwezo wa kisheria walionao,((habu tusaidiye basi sheria gani hiyo iliyo mpaa jecha kufuta uchaguzi sio ZEC haijafuta uchaguzi aliyefuta ni jecha sasa tupe hiyo sheria iliyo mpa uwezo jecha au hata hiyo ZEC kufuta uchaguzi na kama hakuna ole wako)) sasa ni wajibu wao tena kuwaeleza wananchi ni lini watapiga kura tena. ((usisahau kumuambia na Pombe Magufuli pia ajiandae pia basi uchaguzi kurundiwa shaka na kukumbusha tena usisahau kumuambiya na Pombe Magufuli kuwa Zanzibar CCM na jecha wenu mumefuta uchaguz kwa hiyo kura zake pia bye bye kwa hiyo ajiandae tena uchaguzi mwengine utakapo tangwazwa na ZEC,)) ili watimize haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa kidemokrasia,” alisisitiza shaka.

Aliwataka vijana wa CCM kuwa makini, wavumilivu na wenye ari ya kudumisha mapinduzi yao, huku akiwataka kusahau wale wote wenye mawazo ya kutaka kuyazika kwa kuwa hilo halitawezekana milele.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment