Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umezua hofu kubwa bungeni kutokana na hali ya kutangaza msimamo wao wa kutokukubaliana na Rais Pombe Magufuli kulihutubia Bunge.Jana umoja huo ulitangaza rasmi kwamba umemwandikia spika barua ya kuhoji uhalali wa Rais kulihutubua bunge wakati uchaguzi wa nchi ya Zanzibar umefutwa na kulifanya taifa la Zanzibar kutokuwa na rais.Hali hiyo imeifanya serikali kuwa na hofu kubwa ambayo inaonekana kuwatesa viongozi wa CCM siku ya leo iwapo msimamo wao utaendelea kuwa huo.
Ili kuonesha kuwa hofu ni kubwa leo kuanzia asubuhi, maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma hususani katika maeneo ya bunge kulikuwepo na magari ya polisi ya maji ya kuwasha.Mbali na magari ya polisi yenye maji ya kuwasha yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali ya bunge, magari mengine ya jeshi la polisi yalionekana kurandaranda huku yakiwa yamesheheni askari.Hali hiyo imetafsiriwa wananchi na baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma kuwa ni njia pekee serekali hii mpya ya kuwatishia watanganyika ((watanzania)) kwa ujumla wasidai haki yao bali wafuate amri tu na wakazi hao waliuliza jee nchi hii ni ya demokrasia au inatawaliwa kijeshi kutokana na tangazo la Ukawa la kutomtaka Rais John Magufuli kulihutubia Bunge.
No comments:
Post a Comment