Mawaziri walioshinda uchguzi wa 2015 katika uchguzi wa nchi ya Zanzibar wakionyesha shahada zao kuwa walishashinda uchaguzi na kukadhibiwa shahada sasa ZEC inatafuta ukereketwa wao usio na maana yoyote katika nchi ya Zanzibar.
9 Novemba 2015
Bw Khamis amesema kikatiba hakuna mawaziri Zanzibar
Utata umezingira hatima ya mawaziri katika serikali ya Zanzibar baada ya kuongezewa muda Shein kinyume cha sheria na katiba kuendelea kubaki madarakani kutokana na atii utata kuhusu matokeo ya uchaguzi kama wanavyo sema wenyewe CCM.
Chama cha Wananchi (CUF) kimepinga hatua ya kumuongezea muda wa kuhudumu Rais Shein anayetoka Chama cha Mapinduzi (CCM) wakisema hatua hiyo haikufuata katiba. Shein aliongezewa muda kinyume cha sheria na katiba ya nchi ya Zanzibar baada ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa nchi ya Zanzibar atii akisema ulijaa udanganyifu huku hakuna sheria wala katiba iliyo mpa yeye wala tume hiyo kufuta uchaguzi bali alifanya kwa utashiwake au kutishwa au kwa ukereketwa wake wa KiCCM.
Lakini chama cha wananchi CUF kinasema uchaguzi huo ulikuwa halali na mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad anafaa kutangazwa mshindi.Mawaziri waliotoka chama cha CUF kwenye serikali iliyofaa kukamilisha muda wake mwanzoni mwa Novemba wamesema kisheria hawamo uongozini.“Si kwamba tumejiuzulu lakini kisheria na kikatiba muda wetu wa kuhudumu ulimalizika Novemba 2,” amesema Nasor Abubakar Khamis Bakari, aliyekuwa waziri wa haki na masuala ya kikatiba.
“ZEC inafaa kutangaza CUF kuwa mshindi wa uchaguzi kwani hata katika majimbo tayari walitangaza washindi huko.”
Naibu katibu mkuu wa CUF Nassor Ahmed Mazrui, akihutubia kikao cha wanahabari mapema leo mjini Dar es Saaam huko nchini Tanganyika amesema chama hicho hakijafurahishwa na shughuli inayoendelezwa kwa sasa na Zec.
No comments:
Post a Comment