WANASIASA wawili wanaogombania kutwaa urais katika uchaguzi mkuu wa nchi ya Zanzibar wa Oktoba 25, walikutana mjini hapa jana na kuamsha upya “imani” miongoni mwa wananchi kwa vile huo ni mkutano wa kwanza kwao tangu uchaguzi huo ulipofutwa kinyemela Oktoba 28, mwaka huu na mfurukutwa wa CCM.Dk. Shein aliyegombea tena urais kwa tiketi ya Chama Cha Maponduzi (CCM), na Maalim Seif Shariff Hamad, aliyegombea kwa mara ya tano mfululizo huku mara zote nne wakimuibia kura au kufanya vitimbi mpaka anawachia, walikutana Ikulu ya hapa nchini Zanzibar.Hakuna upande wowote kati ya viongozi hao uliotoa maelezo baada ya kukutana kwao, ingawa vyanzo vya ndani ya serikali, Chama Cha Mapinduzi na Chama cha Wananchi (CUF), vimethibitisha mazungumzo ya viongozi hao yalichukua karibu saa nne kumalizika katika mazungumzo yao.Mwandishi wa habari hizi za siri aliye Ikulu ya Zanzibar alipata taarifa awali kuwa ratiba ya kikoa cha viongozi hao ilikuwa kuanzia saa 4 asubuhi hiyo jana, lakini inasemekana kilichelewa kidogo kuanza.Katika hatua nyingine, imeelezwa kwamba kikao cha viongozi hao, pia kilimshirikisha Balozi Mkazi, Balozi Seif Ali Iddi, ambaye mwenyewe aligombea kiti cha uwakilishi, jimbo jipya la Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.Taarifa zaidi zimesema kwamba marais wawili wastaafu wa Zanzibar, Ali Hassan Mwinyi aliyeongoza mwaka mmoja tu kufikia mwaka 1985 alipohamishiwa Tanganyika na kuchaguliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika, na Amani Abeid Amani Karume, aliyeingia Ikulu Novemba 2000 na kutoka Novemba 2010 baada ya kufanikisha mkataba wa kihistoria wa maridhiano na Maalim Seif uliowezesha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) baada ya uchaguzi mkuu.
Haifahamiki ni katika mazingira gani aliitwa Mzee Mwinyi lakini akaachwa Dk. Salmin Amour Juma ambaye aliongoza vipindi viwili kufikia 2000 ulipofanyika uchaguzi mkuu.Maofisa wa Ikulu ya nchi ya Zanzibar hawakuwa tayari kueleza undani wa kikao cha viongozi hao, lakini wale wa CUF walithibitisha kuwa majadiliano yalikuwa “ni mema kwa maslahi ya nchi ya Zanzibar na Wazanzibari.”Zipo taarifa kwamba ni Maalim Seif aliyetaka Mzee Mwinyi ashiriki kikao hicho, lakini hakuna aliyethibitisha taarifa hizo, na wala haikuelezwa sababu ya kualikwa kiongozi mstaafu huyo ambaye kwa Wazanzibari wapenda mabadiliko, anaonekana kama “adui” wa maendeleo ya nchi ya Zanzibar.Tangu kustaafu uongozi mwaka 2000, Dk. Salmin amekuwa haonekani mara kwa mara hadharani kutokana na hali yake ya afya. Hata kabla ya kustaafu, alipata upofu wa macho, na mara ya mwisho alipokutana na waandishi wa habari nyumbani kwake Migombani, mjini hapo, alisema, “sasa hivi angalau naweza kusoma magazeti, sijambo alhamdulillahi.”Hata hivyo, hali yake ilionekana wazi kuwa macho yake hayakuwa na uwezo tena wa kusoma chochote, na kwa jumla kuona.Ingawa hakuna maelezo ya undani wa mazungumzo yalivyokuwa, kule kukutana kwa Shein na Maalim Seif wakati huu, kunaweza kurudisha imani kwamba utatuzi wa mgogoro uko nchani kupatikana.Kikao kilichowakutanisha Shein na Maalim Seif kimefanyika ndani ya hali isiyoeleweka kwa sasa, kwa vile nchi imeganda baada ya kuingizwa kwenye mgogoro wa uchaguzi mkuu.Mgogoro huo umetokana na hatua ya Mpumbavu moja tu anae jali tumbo Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Firauni Jecha, kutangaza uamuzi wa “peke yake” wa kufuta uchaguzi wote nchi nzima huku akiwa ameshatangaza matokeo ya urais kwa majimbo 31 kati ya 54 yote ya nchi ya Zanzibar.Uamuzi huo unatambuliwa kuwa ni wa peke yake, kwa sababu umethibitishwa kutokana na majadiliano ya ndani ya Tume hiyo, na kwa kuwa si yeye mwenyekiti wala Tume, yenye mamlaka ya kisheria au kikatiba ya kufanya hivyo.
Hakuna kifungu cha sheria katika Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, Na. 11 ya mwaka 1984, wala katika Katiba ya nchi ya Zanzibar ya Mwaka 1984, kinachotoa mamlaka hayo kwa namna yoyote ile.Hii imethibitishwa na tamko lake mwenyewe Jecha ambalo pamoja na kuwa alilisaini, hakueleza amepewa mamlaka hayo na kifungu gani cha sheria.Jecha alitangaza uamuzi huo Oktoba 28, siku ya pili, makamishna wawili wa Tume hiyo kutoka CUF, Nassor Khamis Mohamed, na Ayub Bakari, walimkana wakieleza kuwa alichokifanya si halali kwani hakuna mamlaka yaliyompa nguvu, na hakuna kikao cha Tume kilichofanyika hata kufikia uamuzi wa kumtuma kufanya hivyo.Aidha, Jecha alitoa tangazo hilo siku mbili baada ya Maalim Seif kueleza kwamba mwelekeo wa kura ulikuwa wa kumpatia ushindi wa asilimia 52.87 dhidi ya asilimia 47.13 za Dk. Shein.Maalim Seif aliyetoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari, kwenye makao makuu ya CUF, alisema alitarajia Tume itangaze matokeo pasina kuchelewesha na kumtaka Dk. Shein akubali amepoteza mamlaka na kutangaza rasmi kama alivyofanya yeye mwaka 2010.Kukutana kwa viongozi hao kunachukuliwa kama hatua muhimu katika kurudisha “wanasiasa wahafidhina wa CCM” katika ufahamu wao wa akili kwa vile dunia inauhakika kuwa wao ndio tatizo.Matokeo ya uchaguzi yalikuwa tayari yamesainiwa na wasimamizi wa vituo vya uchaguzi nchi nzima katika majimbo yote 54, na hata wakala mkuu wa Shein, Balozi Mohamed Ramiya Abdiwawa, alisharidhia na ikaelezwa “aliharakia kumpa taarifa ya kushindwa Shein.”“Ukweli Shein ameingizwa tu katika mgogoro ili aonekane tatizo, lakini aliharakia kukubali kushindwa na kusema, ‘siwezi kubadilisha uamuzi wa wananchi.”Viongozi wanaotajwa kuchimba mgogoro ni wale watatu walioonekana kwenye vyombo vya habari Oktoba 29, wakitoa malalamiko kuwa CCM ilihujumiwa.Hao ni Spika Pandu Ameir Kificho,Waziri Kiongozi mstaafu Shamsi Vuai Nahodha na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai ambao duru ndani ya CCM zinasema wanaungwa mkono na Balozi Seif na Mpambe wa Balozi Mkazi Mohammed aboud.
No comments:
Post a Comment