TUNAMUOGOPA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD, MAMLAKA YA NCHI TUMUACHEYE TANGANYIKA MASULTANI WETU WEUSI WATUTAWALE, NEEMA KWENYE MATUMBO YETU, WAZANZIBARI NA WAFE NA NJAA NA MAISHA MAGUMU KWA MIAKA MENGINE 50 IJAYO
Lazima sana kuanza kwa kumshukuru Mola wetu kwani bila yeye hapa leo tusingekutana kuongea,kunon’gonezana au kuambizana neno kupeyana ukweli wa mambo japo wengine hujitia hamnazo na kujitowa ufahamu.
Uchaguzi umekwisha kama tunavyojua na mshindi anajulikana ingawa hakutangazwa bado na wahusika na tunavyoambiwa kuwa ametenda dhambi mbaya sana iliyo juu ya uhaini kwa kuwa amejitangaza mwenyewe na hilo ni kosa kwa sheria za nchi yetu Zanzibar kama nchi, ZEC,polisi au ccm kwa ujumla,binafsi silioni kosa hapa kwa sababu halipo, mgombea wa urais Maalim Seif Sharrif Hammad wa chama cha CUF hakuvunja sheria yoyote na wala hajatamka kuwa yeye ndie RAIS wa nchi ya Zanzibar alichokisema na kudai ni kutaka chombo husika yaani ZEC wamtangaze yeye mshindi baada ya kuweka wazi au kuonyesha kura zake HALALI zilizothibitishwa na kuwekwa sahihi na mihuri na wahusika wote na vituo vyao vya tume ya uchaguzi ZEC hapa nchini Zanzibar na zile za mpinzani wake yaani za aliyekuwa rais wa nchi hii ya Zanzibar aliyekuwa maana sasa sio raisi tena kikatiba na kisheria za nchi ya Zanzibar wa kipindi kilichopita na kumaliza muda wake Shein,kuhusu Zanzibar kama nchi nafikiri tumeshawahi kupata jawabu la kitendawili hicho wakati wa ile kesi iliyowakabili watuhumiwa waliotaka kupindua nchi yetu hivi ya Zanzibar na kesi kufika mahakama ya kuu/rufaa ya Masultani WeusiTanganyika na ndipo tulipo pata jawabu ya kuwa hapa hakuna nchi kuna nini hilo mtanisaidia nyinyi mnao soma.
Kilichotendeka oktoba 25 siku ya uchaguzi ndio kile kile nilisema sana hapa kuwa chama changu yaani CCM kitashindwa vibaya kitashindwa vibaya nimeandika sana kuhusu hatma hii hapa na wengi mtakuwa mashahidi wangu kwa kuwa haya sio mageni kwetu sote hasa wale tunaotumia muda mrefu na kuumiza vichwa vyetu kwa kuitakia kheri nchi hii isiyotakiwa na Wakolini Weusi Tanganyika,nilifika kuweka wazi kuwa nitakuwa tayari kuja mbele yenu tena hapa kuwataka radhi ikiwa CCM chama changu kitashinda uchaguzi huu au tutashinda pia niliyajua zamani kuwa hapa hapana uchaguzi bali tujitayarishe na uchafuzi na ndio huu unaoendelea sasa baada ya mwenyekiti wa ZEC Mkereketwa Jecha kuamua kuufuta uchaguzi na kuanza machafuzi ya makusudi ili kukinusuru chama chetu baada ya kuona matokeo halali na halisi ya uchaguzi wenyewe.Ni vema tukayadhukuru yote ya nyuma ili tuweze kujua wapi tulikosea au wapi hakuhitaji marekebisho na nini la kufanya tuepukane na maafa tunayotengenezewa na viongozi wetu wa CCM hapa nchini kwetu Zanzibar na huko kwa Masultani Wetu Weusi Tanganyika waliopo madarakani na wale waliostaafu lakini bado wanafanya kazi za chama cha mapinduzi kwa malipo wanayoyajua wao wenyewe kwa sababu hakuna karatasi au vocha hata moja utakayo iona inayoidhinisha malipo ya viongozi hao akiwemo Ali Hassan Mwinyi,sasa la kujiuliza safari zote hizi za kuja hapa nchini Zanzbar/kurudi Dar nchini Tanganyika za kila kukicha zinafanywa kwa mapenzi ya nchi peke yake...?? au chama peke yake....??au kuna tija gani ndani yake....??
Sababu kubwa ya mwenyekiti wa ZEC kufuta uchaguzi inayopewa kipa umbele hapa nchini Zanzibar na watetezi wengi kama si wote wa chama changu cha CCM isipokuwa mimi au baadhi yetu tusiopenda au kufarijka kwa kujidanganya nafsi zetu kwa makusudi kwa sababu kuna uwezekano mtu ukajidanganya kwa bahati mbaya,ni kule kusema kuwa PEMBA ndio kumetokea uchafuzi wa hali ya juu na huko ni sawa na kusema kuwa hakukuwa na wasimamizi wala ukaguzi wa kura hata uhesabuji wa kura pia ulifanyika chini ya miti kwa kuwa ofisi zilikuwa zinavuja maji na viti vinawasha kama upupu pia nambari za uhakiki wa kura na vitambulisho zilifutwa na kuandikwa kwa wino baada ya kukarabatiwa,huu ni uongo uliojaa uzandiki Pemba hawana bahati siku zote kwa sababu wameamua kwa kujua tena kwa ridhaa yao na kwa makusudi matupu kuikataa CCM miaka yote na kuinyima kura hata ya balozi wa nyumba kumi kumi kwa sababu wametumia haki yao ya kidemokrasia ya kukichagua chama wanachokitaka hata kama hakitowafaa huko usoni lakini huo ni uamuzi wao na ni lazima hatuna hiari tuuheshimu na kuulinda uamuzi wao huo sio kuwatisha na kuwapelekea majeshi au kuwabaguwa na kuwafanyia vitimbi au kuwandika kwenye mabao kisonge haitosaidi haijasaidi na wala haitatokea kusaidia.
Sio rahisi kwa chama changu kupata usingizi na kuukubali ukweli huu,tutawasingizia PEMBA miaka yote tukipenda kwa raha zetu lakini kamwe hautokuwa ukweli wa hali halisi,hali halisi CCM hatutakiwi tena hapa nchini Zanzibar na wengi wa wananchi wetu hii sio siri tena kwa nini tumekuwa wakaidi na vipofu juu,shemeji yangu alikuwa mmoja ya wasimamizi wa uchaguzi pale kibanda maiti alichokuja kunihadithia yeye kilimshitua mimi kilinichekesha chumba alichopangiwa kukisimamia ilikuwa ni cha waajiriwa wa JINA KAPONI peke yao au niseme wengi nitakuwa niko sahihi wakati ulipofika wa kuhesabu kura ulipofika waligundua yeye na wenziwe waajiriwa hao wapya na wakongwe wa JINA KAPUNI nusu yao wamempigia kura mgombea wa CUF yaani Maalim Seif juu ya kutishwa kufukuzwa kazi kulikofanywa na viongozi wa CCM na makamanda wao sasa bado tutazituma lawama zetu PEMBA wakati kura za urais zilizo mpa ushindi Maalim karibu zote zimetoka hapa unguja.
Nirudi kwenye katiba iliyotuletea balaa sisi CCM tulipojikusanya pale Dodoma na kumtukana Warioba na rasimu zake mbili alizoziandika akishirikiana na mwana diplomasia Mohamad Yussuf Mshamba {black} pamoja na wasomi wengine waliobobea katika sheria na lugha tulijiona tuko juu ya ulimwengu wa siasa na Tanganyika na Zanzibar na ni shamba la shemeji yetu na hati miliki ya eka hizi anazo dada yetu chini ya mto kwa amani kabisa hatukuwa na budi kulala usingizi mnono kwa sababu shemeji hawezi kuipata hati miliki ya shamba hili bila kumuamsha dada yetu,kitu ambacho hatukijua hati miliki haikuwepo uchagoni kama tulivyodhani wenye nchi walikuwa nayo mikononi siku nyingi wala hawakulala usingizi siku imefika wanataka nchi yao siku za kucheza na kuimba mguu mbele mguu nyuma zimekwisha, sisi ndio tunataka uchaguzi urudiwe ili tuendelee kuburudika na muzeka wapi haya tumeyakaanga wenyewe kwa miaka yote hii tuliyoifanya dhulma kwa viumbe hawa wa kila rangi wanaopumua hapa nchini Zanzibar na wale waliotangulia,tumehutubia ubaguzi wakati wote wa kampeni tukiongozwa na Balozi seif na Borafya huku viongozi wa juu wakiwa nyuma ya majukwaa wakitoa baraka zao leo tunavuna matunda ya ubaguzi tuliyo yapigia debe kama wendawazimu kwa kuwahofia waislamu wenzetu sijui wangelikuwa makafiri tunge liwasherehekea vipi.....??
Nchi yetu ya Zanzibar kwa sasa hakuna rais wala kiongozi yoyote kikatiba kuna watu tu wanalindwa na polisi na jeshi la Mkoloni Mweusi Tanganyika na mabunduki na kupelekwa safari zao na tunaenda kama mv jamhuri kwa wale wanao ikumbuka yaani bega moja,viburi vilivyojaa mauti ndio vinavyoongoza hapa nchini kwetu Zanzibar hivi kwa sasa tumechoka na amani ya miaka mingi hatuna budi kuitafuta shari kwa bei yoyote hayo ndio yaliyomo ndani ya mioyo ya watawala wetu ambao kwa sasa neno watawala ndio neno sahihi kabisa kwa kuwa hawana ridhaa yetu kutongoza na hatutaki kuongozwa kwa nguvu au mabavu,niliwahi kusema nchi itajiinamia nililitumia hilo neno kwa kuwa ndilo nililoliona linafaa kwa hali hii leo hii nchi ya Zanzibar imegeuka bosnia au palestina maaskari na bunduki,vifaru na zana zote za kijeshi zimeletwa hapa kutulinda tusilaumiane....??kwa kweli inasikitisha sana kuona nchi ya Zanzibar ijulikanayo kama Visiwa vya marashi ya karafuu kwa sasa vinakaribia kunukia baruti,mabomu,risasi na damu za watu wasio na hatia yoyote kwa kukata viongozi wasi wataka na wao hao viongozi kulazimisha kubaki madarakani kwa lazima na sasa kinachosubiriwa ni ama askari mmoja aliye taahira afyatue risasi ovyo au wenye haki wadai haki yao kwa amani au fujo tena itakuwa tumeshapata sababu ya kuhalalisha “UCHAGUZI URIDIWE” kwa sababu tunachohitaji kwa bahati mbaya sana ni tone la damu limwagike ili watawala waendelee kula nchi au kututawala tukitaka tusitake.
Kumuapisha Maalim Seif Shariff Hamad kuwa rais ndio mtihani mkubwa kwa chama changu CCM kwa sasa matokeo wameshayakubali siku nyingi tatizo ni kiongozi mwenyewe sijui anaogopwa nini bwana huyu na utu uzima huu alio nao sasa,kuna wakati hata mimi nikimuogopa huyu muungwana ukweli niseme lakini sio leo hekima tupu imejaa kichwani mwake mengi yamemkuta katika uhai wake hasa wa siasa,mandela alitegemewa na wengi aje na kuna waliomtaka na kumlazimisha alipize kisasi kwa yote aliyofanyiwa binafsi na watu wake weusi kwa weupe lakini alikataa na alikuja na busara za kiongozi mpevu mpaka leo afrika ya kusini iko shwari,uholanzi wanakotoka wadachi kiasili walijenga miji maalum kwa kuwapokea wazungu wenzao kutoka huko afrika ya kusini walidhani Mandela atawafukuza na kuwabaguwa badala yake hakuwafukuza baada ya kupata uhuru na majengo walio jenga wadachi kuwapokea ndugu zao kutoka afrika ya kusini huko hivi sasa wanajaza wakimbizi toka duniani kote kwa kuwa wale wazungu walio watarajia hawakupatikana,tuondoe viburi mauti kwa kuogopana kusiko kuwa na tija tuna jitia vijiti vya macho kwa kudhania tunajipura kwa wanja,tusisubiri upofu ndio tujifunze kuona.naona kwa leo niishie hapa naomba radhi kwa makosa yatakayojitokeza ya uchapaji,nina mengi sikuwahi au kujaaliwa kunena leo inshalah nitapata muda nitajaribu tena kuelezea kilichojiri,kinachojiri na kitakachojiri hapa kwetu tusisite kuomba salama visiwa au nchi yetu ya Zanzibar hivi sasa inafukuta moshi mtupu kwa sasa wapulizaji wako wengi magari ya zima moto tunayo mawili tu na moja bovu kwa maana hiyo limebaki moja nalo kongwe kwa ufupi moto una kila sababu ya kuwaka na utushinde kuuzima sasa wakati umefika wa kuachana na “viburi mauti”
ASANTENI.
No comments:
Post a Comment