Balozi Mkazi aliwahakikishia Viongozi hao wa Dini kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga vizuri kupitia vyombo vyake vya ulinzi kwa kupiga Doria maeneo yote katika kuona atii amani ya nchi inaendelea kudumu. Aliwapongeza Viongozi hao wa Dini kwa jitihada zao wanazochukuwa za kutumia busara zao kwa kukutana na Viongozi wa pande mbali mbali za Kisiasa wakilenga kusaidia kutuliza mumkari na machungu ya waumini wao ambao takriban wote ni wafuasi wa vyama vya Kisiasa vilivyopo hapa Nchini. Alivilaumu baadhi ya vyombo vya Habari hasa vile vya Nchi za Magharibi jinsi vilivyoonyesha wazi Taarifa zao nyingi wanazotowa za zoezi zima la uchaguzi Mkuu wa Zanzibar zikionyesha kuegemea upande mmoja tu. Balozi Mkazi huyo alielezea atii masikitiko yake juu ya wangalizi wa Kimataifa walioamua kufuatilia uchaguzi Mkuu wa Zanzibar kwamba hawakwenda Kisiwani Pemba muda wote wa zoezi la kupiga kura kufuatilia changamoto zilizojitokeza katika majimbo ya Pemba. ” Nimesikitishwa na waangalizi wa Kimataifa waliokuwepo Zanzibar kwa karibu mwezi mmoja kufuatilia kampeni na uchaguzi wake wameshindwa kwenda Pemba wakati wa zoezi la kupiga kura na kuonekana zaidi katika majimbo ya Kisiwa cha Unguja. Balozi Seif aliishauri Idara ya Habari Maelezo kuendelea kufuatilia Taarifa zinazotolewa na vyombo mbali mbali vya Habari ndani na nje ya Nchini na kukemea au kutoa Taarifa dhidi ya uchochezi unaotolewa na vyombo hivyo.
Huyu Balozi Mkazi na Shein na Jecha wote ni watumwa wa Mkoloni Mweusi Tanganyika wapo hapa kwa kzi maalum na ndio sasa wanaitimiza kwa guvu zote walianza na Masheikh na sasa watajidai kila aliye simamia uchaguzi pia nae aende jela watawafunga watu na kuwatesa watu ndani ya jela ili watu waingiwe na woga wanyamaze wao waendelea kuwa madarakani na huku wanaendelea na jitihada zao za kufanya Zanzibar iwe wilaya katika wilaya za nchi ya Mkoloni Mweusi Tanganyika Wazanzibari kaeni mkao wa kula ukisikia mumeo ashachukuliwa na polisi usistajabu ujuwe na yeye ashakubwa na mkono wa Wakoloni Weusi Tanganyika kwa kutumia wahafidhina wake hapa nchini Zanzibar Shein,Balozi Mkazi,Kificho,Vuai ali Vuai,Nahodha,Samia.Borafya,Jecha firauni jecha, N.K. kisha atii Balozi Mkazi anajidai kuwa serekali itawashughulikia wale wote walio chafua uchaguzi serekali ipi hiyo...? ya majeshi ya Mkoloni Mweusi Tanganyika yalio jazwa hapa nchini Zanzibar..? serekali ya Shein aliyejifungia ikulu kimya huku akilia usiku kucha ili itoke sababu mbaya ambayo itamfanya abakiye....? serekali ya jimbo lako ulilifanya kila ukiritibwa ili ushinde na ukae ukijuwa tukipata serekali tunakushtaki ili jimbo la mahonda uliteme maana hukushinda,serekali ya jecha ya kufuta uchaguzi.....?
No comments:
Post a Comment