Thursday, November 26, 2015

RAISI MAGUFULI AMERITHI NCHI AMBAYO RUSHWA NI SEHEMU YA SHERIA NA KATIBA YA NCHI KWA SASA INAYO WAONGEZA VIONGOZI UTAJIRI NA KUWAUMIZA NA KUWAUWA WANANCHI

Ulimwengu wa sasa umefikishwa pahali pabaya sana sana na tawala luluki za kifisadi zilizopita. Tawala ambazo, kwa hakika zimeleta ufujifu mkubwa wa amani na utulivu kwa matumizi mabaya ya dola na fedha za umma. Tawala zilizotawaliwa na viongozi waroho wa madaraka, walafi, wachoyo, wabinafsi na wasiojali wanyonge wala wanaowaongoza kama ilivyo nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar pia Pombe Magufuli leo.Taifa lolote linapofikia hatua ya kifisadi kama hiyo mungu huwashushushia nakama ya njaa, vita, na kila aina ya uonevu ambayo inawafanya wote, wanaonyonya na wanaonyonywa wapate shida na mateso yasiyomithilika. Hali hii husababishwa na kushindwa kwa mfumo sahihi wa maisha uliolengwa kuwasaidia watu kufikia malengo yao baada ya ufisadi kushika hatamu. Rais Pombe Magufuli, rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Tanganyika, ameingia madarakani hivi juzi na kurithi Tanganyika iliyo mahututi kwa ufisadi na ubadharifu katika Nyanja zote za nchi hii ya Tanganyika. Magufuli anarithi Tanganyika yenye viongozi mafisadi waliofurutu ada wala hawasiki wala hawaoni wala hawajali wala hawana hata hurumu wamekuwa kama familia za utawala wa Kiroma ni wao na familia zao na mahawara wao na watoto wao wa nje na rafiki zao walio baki kufeni na njaa na maaradhi pia wao hawajali. Magufuli anarithi Tanganyika ambayo viongozi wakuu wa nchi wanatumia madaraka yao kujitajirisha wao na familia zao.Magufuli anaingia madarakani katika nchi ambayo Serikali imo kiganjani mwa wafanya biashara na wala rushwa na pia rushwa imekuwa ni sehemu ya sheria na katiba ya nchi kwa sasa katika nchi hii ya Tanganyika. Magufuli anarithi nchi iliyokufa katika mfumo wa sheria na mahakama, miundo mbinu, nishati, madini, haki za binadamu, uchumi, kilimo, utalii na kila nyanja ya uchumi imekufa fofofo!!! na rushwa imetawala katika kila nyanja za hayo yote.


Leo hii Magufuli anaingia Ikulu huku Hospitali zetu zikijaa wagonjwa wasioshughulikiwa hadi kufa huko. Wagonjwa ambao hulala chini kwenye wodi zinazonuka kuliko machinjio ya ng’ombe. Haya yote yapo nchi nzima ya Tanganyika. Magufuli anaingia Ikulu akiwa na mkururo wa viongozi mafisadi ambao wao na aila zao ndio wanaomiliki uchumi wa nchi bila hata kulipa kodi hata chembe. Magufuli, ukiachilia mbali mzozo wa nchi ya Zanzibar ambao anaonekana haumshuhulishi sana na kujitia hamnazo, anakabiliwa na changa moto kubwa ya kurudisha hela ya kuurudisha tena uchumi wa nchi ya Tanganyika kuwa katika hali ilivyo sasa. Magufuli anakuja wakati ambao watu kama Kingunge na familia yake wanaweza kukodoshwa kituo kizima cha mabasi ya Ubungo kwa kodi ya milioni mbili kwa mwaka. Magufuli anakuja wakati ambapo watoto wa Viongozi kama Ridhiwani Kikwete wanamiliki mabasi karibu yote ya UDA hapa Dar Es Salaam ilhali hata kodi hata chembe hawalipi na ikiwa zitalipwa basi zinavyolipwa ni mushkeli mtupu na vichekesho. Magufuli anakuja katika Uongozi ambapo umasikini wa nchi ya Tanganyika umezidi kipimo kuliko miaka ile ya 1970 na hata baada ya vita vya Uganda vya 1978-79. Kwa ufupi, Magufuli amekuja katika Tanganyika ambayo imeshakufa dungu msokoni. Imekufa kwa sababu amerithishwa Serikali yenye matatizo kadhaa wa kadha na Viongozi waliomtangulia na kumuachia Tanganyika ikiwa kama mzoga wa Tembo aliyekwishang’olewa vipusa. Haya yote yamefanyika na kwa miaka 54 sasa, unaweza kuona kuwa kuna kila sababu ya nchi ya Tanganyika kupata Rais aina ya Magufuli.nchi ya Tanganyika kwa hakika inahitaji Kiongozi mfano wa Magufuli. Rais ambaye badala ya kutumia mamilioni ya fedha kuandaa sherehe za Uhuru wa Tanganyika, sasa anaokoa mamilioni ya fedha kwa kuwataka viongozi nchi nzima wafanye usafi pesa za kufanya shrehe hizo kwend kwa wanao hitaji kama maji safi nchi nzima tena sio mfereji moja kijiji kizima laa maji yatoke katika kila mbomba ndani ya nyumba,umeme wa uhakika sio zima washa zima washa kama tuko disco,dawa hospitalini n.k.
Rais ambaye, badala ya kuyafumbia macho makosa ya uzembe wa utendaji katika Hospitali zetu, amevaa njuga na kuyafanyia kazi na kuyapatia utatuzi haraka sana. Kiongozi ambaye wakati viongozi waliotangulia wakitumia mamilioni ya fedha kwa safari za nje kwenda kuinjoi na wake zao au mahawara wao, yeye ameamua kuzifungia safari hizo na kutaka fedha zitumike katika shughuli za kimaendeleo. Rais ambaye, badala ya kutumia mamilioni kwa vikao vya Serikali, huamuru watumishi waishie kula njugu (karanga) na juisi ya ukwaju huku akiamini kuwa hapana haja ya kulipwa posho kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kazi zao good one au ni seme Sadakta. Hatua hii ya Rais Mgufuli kufanya marekebisho makubwa ya mambo ambayo hatujapata kuyaona yakifanywa na kiongozi yeyote, hata huyo Nyerere wana muita baba yao wa taifa la Tanganyika, tunaweza kuiita ‘MAGUFULICATION’ of TANGANYIKA na falsafa inayosimama juu ya mchakato huu inaitwa ‘MAGUFULISM’. Hatua ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko haya ya kurudisha heshima katika utumishi wa Umma na kuimarisha utendaji wa Serikali (Magufulication) na Imani yake kuwa atahakikisha kila kitu kinakuwa sawa na Watanganyika kwa mara ya kwanza katika maisha yao wanapata nchi yao ya Tanganyika iliyo bora kabisa (Magufulism) ni hatua nzuri ya kupigiwa mfano kwa kweli na ndio maana nchi jerani kama Kenya nao washanza kushughulikia Viongozi mafisadi baada ya kuona ((Magufulism is working)). Hoja yangu lakini inakuja kuwa, pamoja na kuwa Magufuli amekuja kufichua uoza ulioachwa na waliomtangulia, nahisi Magufuli amekuja mwisho wa karamu. Ujio wake na sera zake za ‘Magufulism’ ni nzuri lakini nina uhakika akiwa amezungukwa na jopo la JUJA wa MAJUJA na masihi Dajjal ndani ya Serikali yake, hafiki mbali. Na iwapo atashinda vita hii, itakuwa ndio mwisho wa dunia maana wenye nchi wapo na wanatizama tu anavyo fanya na hawatamuachia afanye Umagufulism wake na kuwaathiri katika maslahi yao na yawatoto wao na ya mahawara wao. Kwa maana hiyo, licha ya uzuri wa sera zake za ‘Kimagufulism’ na hatua zake murwa za kurejesha hadhi ya uchumi wa nchi ‘Magufulication’ , bado naamini kuwa amechelewa sana. Tumeona hapo awali, wenziwe waliomtangulia, walikuja na Ari Mpya kifyofyoko, Nguvu Mpya kinyokonyoko na Kasi Mpya kifyokokifokoke, Watanganyika wakaishia na Tanganyika yenye uchumi mbovu unaokaribiana na ule wa Zimbabwe!!! na mipesa mingi isiyo na thamani utafikiri tuko somalia!!! Na licha ya uthabiti wa nia yake, nionavyo ni kama vile anakazania kulifunga banda wakati farasi kashatoka!!! si Wazanzibari yetu machooooooooooooooooooooooooooo.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment