Friday, November 20, 2015

NCHINI TANGANYIKA JOHN MAGUFULI MWANASHERIA ULIO MUAPISHA BORA AJIUZULU ASHAKUPAKA MAVI KWA KUSEMA UWONGO KUWA SHEIN NI RAIS HALILI NA KUJARIBU KUPINDISHA KATIBA KWA KUDANGANYA UMMA HAFAI NA AJIUZULU


MAGUFULI HUYU KICHWA CHA SAMAKI AMEANZA KUPOTOSHA KATIBA NA NDIO KWANZA HATA SIKU MIA ZAKO ZA KWANZA HAZIJAKAMILIA ANAKUPAKA MAVI
DADA WASOMESHE SHERIA HAWA MAJUHA
KAKA WASOMESHE SHERIA HAWA MAZEZETA
Jee Shein Rais Halali kama alivyo sema Mwenasheria wa nchi ya Tanganyika hebu tuitazama katiba ya nchi ya nchi ya Zanzibar inasemaje.....?
Kumekua na maoni tofauti kuhusu Kuendelea kwa Expire Raisi Shein na Uhalali wake. Mwana sheria mkuu wa Serikali ya Muungano feki wa Jamuhuri ya Tanganyika na Jamuhuri ya watu wa Zanzibar amesema Shein ni halali kwa mujibu wa kifungu 28-1(a) . Hapa amepotosha kwa makusudi ni jambo baya sana sana kuhalalisha batili katika sheria na hasa hasa katiba ya nchi ambayo sio nchi yako na hata ikiwa ni nchi yako huwezi kupindisha sheria kwa kujifurahisha au kukamilisha mipango ambayo na kwa manufa ya viongozi wachache kwa jili ya kubaki madarakani ni kosa kubwa sana.
Ukweli kuhusu kifungu hichi ni kuonesha namna gani rais atasita kuwa rais. Kifungu hichi sio kifungu kinacho toa ruhusa ya nyongeza ya muda au kumhalalishia Expire Raisi Shein kubaki madarakani bali kinaeleza sababu ya kuendelea kama tu kumefanyika uchaguzi na rais mteule amepatikana basi muda wake utakoma pale atakapo apishwa rais mteule. Kama hakuna uchaguzi basi kifungu hichi haki apply na hakina maana yoyote kwa suala la Zanzibar. Zanzibar uchaguzi umefutwa hivyo hakuna rais mteule na tukumbuke kuwa akiye futa hana madaraka hayo ya kufuta wala hana uwezo wakufuta kwa njia yoyote hana uwezo wa kufuta kisheria wala kikatiba ila amaefuta tu kwa kiukereketwa wake baada ya kuona chama chake kinashindwa na nikosa la kihaini alilolifanya ndio maana wakamficha huyo Jecha.
KATIBA YA ZANZIBAR INATUAMBIA NINI.
28.(1) Kufuatana na Katiba hii mtu ataendelea kuwa Rais mpaka:
(a) Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais; au
( HAPA HAKUNA RAIS ANAYEFUATA NAOMBA TUELEWANE VIZURI. WALA HAKUNA RAIS ANAESUBIRI KULA KIAPO TUSOME VIZURI SANA TUSIKUBALI KATIBA KUCHEZEWA KWA MASLAHI YA KICHAMA –TUNAJENGA BAD PRECEDENT AMBAYO MBELENI ITALETA MATATIZO SANA TUSIPOLISEMEA HILI NA HATA KULIFUNGULIA KESI YA KIKATIBA KATIKA MAHAKAMA YA KATIBA AMBAYO HAIPO LAKINI KATIBA YA JAMHURI INAITAMBUA KUWEPO KWAKE)
(b) afariki wakati akiwa Rais; au
(c) hapo atapojiuzulu; au
(d) iwapo amechaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania; au
(e) kwa sababu yoyote nyengine ameacha kuwa
Kiongozi kwa mujibu wa vifungu vyengine vya Katiba
hii.
Ukomo wa muda wa Urais unaelezwa vizuri katika kifungu cha 28-2 . Kifungu hichi kimeweka wazi namna ukomo wa rais unavomaliza . Expire Shein ukomo wake umemaliza kwa mujibu wa 28 – (a) …..kisome vizuri utaelewa.
Katiba hii wala haina mgogoro imeweka wazi kuwa ukomo wa rais ni miaka 5 tu Ukimaliza muda wa miaka 5 uongozi wako umefika mwisho. Hivyo ni wazi Expire Shein amemaliza muda wake. Ni jambo la kushangaza mwana sheria mkuu wa Serikali ya Tanganyika anapindisha kwa makusudi kabisa maana ya katiba ni jambo la aibu na hatari sana.
28 (2) Kufuatana na maelezo ya kijifungu (1) cha kifungu hiki,
Rais ataacha madaraka yake baada ya kumalizika miaka mitano
kuanzia tarehe, ambapo:
(a) kama yeye ni mtu ambaye ndiye mara ya kwanza
amechaguliwa kuwa Rais chini ya Katiba hii alipokula
kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais; na
(b) kwa sababu nyenginezo mtu wa mwisho kushika
madaraka hayo kwa mujibu wa Katiba hii alipokula
kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuwa Rais, au
pasingelikuwa na sababu ya kifo chake, basi angalikula
kiapo hicho.
(3) Bila ya kuathiri chochote kilichomo katika kifungu hiki
cha Katiba hii hakutakua na mtu yeyote ataechaguliwa kuwa Rais wa
Zanzibar kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja.
Jee wakati gani Rais ataongezewa muda wa kuongoza.....?? Expire Shein Urais wake umefikia ukomo jee anastahiki kuongezewa muda.....??
Katiba hii imeweka wazi wakati gani rais amaweza kuongezewa muda kama aya 29 chini inavoeleza. Sasa hatupo kwenye vita hivyo hakuna sababu ya Shein kuongezewa muda!!!!! au ndio mumeleta majeshi magusudi ili watu wanzishe vita kisha Expire Shein abaki madarakani...?? basi mumeula na chuya Wazanzibari wanajuwa siasa musifikiri ni wajinga majeshi yameja na vita hakuna munaendelea kuvunja katika na kuvunja sheria za nchi ya Zanzibar.
Kuongezwa kwa kipindi cha miaka mitano. Kif. 14 cha Sheria Nam. 9/ 2010.
29. Ikiwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imo katika vita na
ikiwa Rais anaona kuwa ni muhimu kuzuia uchaguzi, Baraza la
Wawakilishi linaweza kwa kupitisha Azimio, kuzidisha muda wa miaka
mitano uliotajwa kwenye kijifungu (2) cha kifungu cha 28 katika kipindi
hadi kipindi lakini hakutakuwa na kipindi kitakachozidi miezi sita
mfululizo.
Ukawa wapo sawa kabisa na Expire Shein yupo pale IKULU KACHUTAMA kinyume na katiba hivyo Expire Shein hastahili kualikwa bungeni kama rais wa nchi ya Zanzibar ila kama Bunge ni kundi la Mafia sawa munaweza kumualika. Kumualika kwa vile ccm wapo wengi bungeni ni ulimbukeni wa kupenda chama zaidi kuliko katiba yetu na ni hatari sana kwa utawala bora.

KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment