Saturday, November 7, 2015

VIDEO-NCHINI ZANZIBAR UKUMBUSHO KWA SHEIN KABLA YA SIKU YA MALAIKATU MAUTI HAJAKUTEMBELEA NA KUKUTANA NA M.MUNGUAmesema Mtume wetu Karim (SAW) huku akiwauliza Masahaba zake Jaliil ” Jee mnamjuwa nani ni muflis....???”
Masahaba wakamjibu ,” Ewe Mjumbe wa Allah, muflis ni yule asiye na dirham wala dinaar (yaani kafilisika kipesa na kimapato)”
Mtume (SAW) akwajibu Masahaba zake,”Hapana… muflis ni yule atakaeletwa mbele ya Mahkma ya Allah (SWT) akiwa na thawabu zinafurutu ukubwa Jabal Uhud. Lakini kamtukana huyu, kamuudhi huyu,kamsengenya huyu,kamzini mke wa huyu, kadhulumu haki ya huyu nk…nk… Kisha watahudhurishwa wale waliodhulumiwa na atanyang’anywa yule dhalim thawabu zake kwa kiwango cha dhulma aliyoifanya kwa kila mmoja na kupewa wale waliodhulumiwa. Hadi kufika thawabu zake zote zimekwisha kulipa dhulma zile, lakini inakuwa bado hazitoshi anadaiwa kwa hivyo huchukuliwa madhambi ya waliyodhulumiwa akabandikwa nayo kisha akatoswa kwenye Jahannam milele.” Sadaqa Rasulu’Allah (SAW). Au kama Qaal.
Sasa Shein unajuwa wangapi uliowadhulumu...?? Umma Mzima wa nchi ya Zanzibar mbali ya dhulma zako nyengine za kudhalilisha kuwasulubu Wazanzibari kwa mateso na mitutu ya bunduki. Mbali ya Masheke waliongali wanasononeka jela za nchi ya Tanganyika. Ukiwa wewe unajiona jabari,jee uko tayari kujibu mbele ya Jabbaru Samawati Wal ardhi...?? Jabbari wa Majabbari SWT. Jee unaeweza kufurutu aliyoyafanya Hajjaaj Bin Yusuf Athaqafii? Kauwa Waislamu 63,000 akiwemo mtoto wa Asmaa bint Abuubakr. Leo yuko wapi....??
Shein wewe na sisi mipito yetu hapa duniani ni kufumba na kufumbuwa. Usighurike na cheo au nguvu za dola, ukafanya kibri, ari na ghera na kukataa kushindwa. Vyote hivyo ni amana na dhamana uliopewa na Allah SWT na atakuliza ulivitumia vipi.
Shein mche Allah SWT wakati unayo fursa kutasamaha na Wazanzibari wenzio na wakakusameh.
Ukiwaendekeza Seif Balozi, Shaka, Hamza, Vuai, Jecha,Kificho, Borafya Shamte Nahodha,samia & company, wote watakuruka hawa!!!! wewe na khiyari yako. Natarjiya kuwa wewe ni Muislamu Muumin. Ndugu yangu Kesho haina msalie. Utabaki “Yaa laitani kuntu turaba”


Yupo kiongozi mmoja wa ASP. Simtaji kwa jina. Kifo chake kina mazingatio kwako wewe Shein.
Kwa miaka kabla ya kifo chake, alikuwa akiingia kwenye COMA na kutoka. Yaani akiugulia maumivu makali sana hadi kupoteza fahamu na baadae kuja juu tena. Hali ilizidi kuwa mbaya kila siku zikisonga. La kutisha, wakati ulipokaribia kutoka roho yake, alipoteza fahamu kipindi kirefu sana kiasi kuwapa wasiwasi manesi. Kudhani kuwa tayari mzee ashakabidhi amana. Lakini yule nesi alopangiwa hakuwa na wasiwasi. Akiwambia wenzake “mzee atarudi”lakini siku zake zilifika.
Siku ya kutoka roho ilikuwa jumapili, alfajiri ghafla alizinduka. Alianza kusema kwa sauti maneno ya ajabu. Akisema kwa kelele “jamaniii siasa mbaya,” “siasa mbaya wanangu,” “siasa mbayaaaa ah najuta,”
Yule nesi kumsikia mzee akawakimbilia wenzake waje kumuona mzee karudi. Lakini walipoingia ajabu hawakumkuta mzee kitandani. Kusachi wakamuona mvinguni mwaa kitanda ameshakufa mweusiiii kama mkaa.

ZINGATIA SHENI


KILA MZANZIBARI ALIYE IPIGIA KURA CCM AU MPAKA WAKATI HUU BADO ANAISAPOTI CCM ILI IBAKI MADARAKANI JAPO KUWA CCM IMESHINDWA UCHAGUZI AJUWE NA YEYE ANACHANGIA KUENDELEZA DHULMA NA KUFUNGWA KWA MASHEIKH NA KUTHALILISHWA KWAO NA KUENDELEZA DHULMA KATIKA NCHI YA ZANZIBAR UKAE UKIJUWA UTAULIZWA SIKU YA KIYAMA NA MWENYEZI MUNGU ULIPOSIKIA WAZANZIBARI WENZIO WANADHALILISHWA,KUDHULUMIWA NA KULAWITIWA NA HAWA JE ULIFANYA NINI TAFUTA JIBU LAKO MAPEMA KWA SIKU HIYO YA KIYAMA SIKU AMBAYO MALI NA WATOTO WAKO WALA CHEO CHAKO HAVITAKUFAA SIKU HIYO.

No comments:

Post a Comment