Wednesday, July 20, 2011

HOSPITAL YA RURARI MKOA WA MARA ILIOANZISHWA NA RAI WA TANG 1085 MPAKA LEO SEREKALI YA TANG IMESHINDWA KUIMALIZA MAJAMBAZI WAKUBWA CCM


             Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri

KITENDADAWILI cha kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali ya Rurani Mkoa wa Mara ulioanza mwaka 1085, kimeshindwa kuteguliwa baada ya serikali kushindwa kutoa jibu la moja kwa moja.
Hata hivyo, licha ya wananchi kuchangia ujenzi huo, serikali imewataka kuendelea na juhudi hizo na kwamba, kiwango kinachotakiwa kukamilisha ujenzi huo ni kikubwa na haina fedha hizo kwa mkupuo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Aggrey Mwanri, alisema fedha zinazotakiwa kukamilisha ujenzi huo ni zaidi ya Sh13 bilioni, ambazo serikali haiwezi kuzipata kwa mkupuo.
Mwanri alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere, aliyetaka kujua mpango wa serikali kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo ili kuunga mkono juhudi za wananchi.
Pia, mbunge huyo alitaka kujua kiwango cha fedha kilichotengwa mwaka huu na muda zitakapoanza kutumika.Mwanri alisema nia ya kuendeleza ujenzi wa hospitali hiyo bado ipo ili kuunga mkono hatua mbalimbali za wananchi walioanza kazi hiyo tangu mwaka 1985.Alisema kwa kuzingatia umuhimu wa hospitali hiyo, uongozi wa mkoa kwenye bajeti ya mwaka huu, umewasilisha maombi maalumu ya Sh13 bilioni kwa ajili kuendelea na ujenzi huo.Hata hivyo, Mwanri alisema ni nyingi na hakuna mahali zilipoandikwa katika vitabu vya bajeti ya mwaka huu kwa sababu Hazina hawajatoa majibu.

No comments:

Post a Comment