Monday, July 4, 2011

TANU-AMBAYO NI CCM SASA INAJIANDAA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WAO NA MAFANIKIO YA UKOLONI WAO JUU YA ZANZIBAR


Hapa ndipo chanzo cha miaka 50 ya Uhuru.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mwaka huu Sehemu ya nchi, yaani TANGANYIKA  itaadhimisha miaka hamsini ya Uhuru  toka kwa Wakoloni.wakati wao wenyewe ni wakoloni wanaisulubu NCHI YA ZANZIBAR  katika kila hali na kila binu.  Uhuru huu uliopatikana miaka hamsini iliyopita ni kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na Chama cha TANU.kuimeza NCHI ZANZIBAR na kuhakikisha inafuta utaifa wa NCHI YA ZANZIBAR na kutubatiza kuwa WATANGANYIKA  wa mkoa wa pwani
Chama Cha TANU katika kukumbuka kazi  nzuri ya kutafuta Uhuru wa nchi  ya TANGANYIKA kimeamua kufanya shughuli mbalimbali za kukumbuka kuzaliwa kwa chama kilicholeta Uhuru wa TANGANYIKA yaani TANU.
TANU ilizaliwa tarehe 7/7/1954 jijini Dar es salaam katika mtaa wa New street ambao kwa sasa unafahamika kama mtaa wa Lumumba mahali ambapo sasa ni  Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu, Na Huo ulikuwa ni moja ktk kupata uhuru wa TANGANYIKA maana chama kilicho anza kudai uhuru ni cha cha TAA ambacho kwa sasa hakitajwi na kimefukiwa ukweli wake na watu wanapakwa uwongo tu kuanzia maskuli hata majumbani,huu ndio ukweli,Utu na Heshima ya Mwafrika ikiwa patasemwa kweli lakini hapasemwi kweli ni uwongo,ufisadi na unafiki.
Kwa kuienzi historia na kazi nzuri na ya Kizalendo iliyofanywa na TANU,kwa kuimeza ZANZIBAR na hata sasa kuna umoja wa AFRIKA MASHARIKI pia wanataka watumeze na tusionekane kama kuna NCHI INAITWA ZANZIBAR ktk NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.chama cha TANU ambacho sasa ni CCM kimeamua katika kuadhimisha miaka hamsini ya Uhuru wa TANGANYIKA kwa kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii zikiwa na kauli mbiu Uhuru na Kazi, kauli maarufu katika miaka ya nyuma ambayo Baba wa Taifa LA TANGANYIKA Mwalimu J. K. Nyerere aliitoa katika hotuba yake ya kusisimua siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Mwalimu Nyerere aliitumia hotuba hiyo kuwaeleza wananchi wajiandae kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea  wenyewe na nchi yao ya TANGANYIKA maende ya sasa. Maadhimisho haya yatafanyika nchi nzima kuanzia ngazi za matawi na kuwashirikisha wanachama wa CCM na wananchi wote kwa ujumla na nifuraha kubwa kuwa sasa ndio wanaimaliza NCHI YA ZANZIBAR maana kutakuwa na KATIBA MOJA NCHI MOJA ZANZIBAR ITATABULIKA KUWA NI MKOA WA PWANI ZANZIBAR.
TUMEKWISHA KABISA.

No comments:

Post a Comment