SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar bado imekumbwa na kigugumizi kikubwa juu ya kuruhusu udhamini wa makampuni ya bia kuja kusaidia michezo ikiwemo mpira wa miguu visiwani Zanzibar.Akijibu maswali la wajumbe wa baraza la wawakilishi Naibu Waziri Habari, Utamduni, Utalii na Michezo, Bihindi Hamad Khamis alisema kwa kifupi sana kwamba serikali imesikia maoni ya wajumbe wa baraza la wawakilishi juu ya suala hilo la kuruhusi wadhamini wa pombe lakini ushauri huo umeuchukua na serikali itaufanyia kazi.
Awali Mwakilishi Jimbo la Rahaleo (CCM) Nassor Salim Ali alitaka kujua ni lini serikali itaondosha marufuku ya udhamini wa michezo wa makampuni ya bia kwa kuwa makampuni hayo hayamiliki pombe pekee bali haa vinywaji vyengine vibaridi ikiwemo malta .
“Mheshimiwa Spika ni kwa nini serikali haifikirii kuyaruhusu makampuni ya bia Tanzania kuja kudhamini michezo yetu wakati makampuni haya hayazalishi bia peke yake huwa wana vinywaji vyengine ambavyo sio pombe mfano kama malta na vinywaji vyengine ” alihoji mwakilishi huyo.
Suala la udhamini wa makampuni ya bia katika michezo limekuwa likijirudia kila mara ambapo baadhi ya wawakilishi wakiishauri serikali kuondosha marufuku hiyo ambayo haipo kisheria kwa kuwa michezo imekuwa ikidorora sana kwa kukosa wafadhili
.
BORA IDORORE KULIKO KUWA NA MAMBO HAYA ZANZIBAR
Hata hivyo serikali imekuwa ikijibu kwamba michezo inaweza kudhaminiwa na makampuni mengine yasiokuwa na biashara ya pombe kama vile simu za mikononi kama zantel ambayo imeshawahi kudhamini mipira wa miguu hapa zanzibar.
Aidha Mwakilishi huyo alihoji ni lini serikali itaona haja ya kuhamisha mchezo pete ambao huchezwa na idadi kubwa ya wanawake ambapo imekuwa ukileta usumbufu mkubwa kutokana na mchezo huo kuchezwa katika eneo la kiwanja cha Gymkhana ambapo huleta usumbufu kwa wananchi kwani kipo sehemu ya kuendesha biashara ya ulevi.
Mwakilishi huyo aliungwa mkono na baadhi ya wajumbe wengine wa baraza la wawakilishi ambao wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuondosha mchezo wa mpira wa pete katika eneo la Gymkhana ambalo hutumiwa kwa starehe ikiwemo vilabu vya uuzwaji wa pombe.
Naibu Waziri wa wizara hiyo Bihindi alikiri kuwepo kwa usumbufu kwani sehemu iliopo kiwanja hicho ni maarufu kwa biashara ya pombe hapo Gymkkana na hivyo haileti sura nzuri kwa utamaduni wa wananchi wa Zanzibar lakini alisema suala hilo litafikiriwa na kuamuliwa baadae.
“Mheshimiwa spika ni kweli kiwanja kile kipo katika eneo ambalo linaendesha biashara ya ulevi…..ni tatizo kubwa kwani ni kinyume na utamaduni na silka za wananchi wa visiwa hivi lakini suala hili tumelichukua na tutalifanyia kazi”alisema Bihindi.
Alisema Serikali inafanya juhudi za kutafuta eneo jengine la kujenga kiwanja cha mchezo wa mpira wa pete ili kuona unaondoka katika eneo hilo .
Bihindi alisema wananchi wengi ikiwemo vijana hufika katika eneo lile kwa ajili ya kuangalia mchezo huo lakini pia wakati ule ule hufanyika biashara ya ulevi
Kiwanja kikubwa cha mchezo wa mpira wa pete ambacho hufanyika michezo mbali mbali ya kimataifa kipo Gymkhana eneo Maisara Mjini Unguja ambalo ni maarufu na ni la muda mrefu katika uuzaji wa pombe.
Serikali ya Mapinduziya Zanzibar hadi sasa imepiga marufuku matangazo ya pombe pamoja na ufadhili wake katika vilabu vya soka vya hapa ikiwemo katika viwanja vya michezo kwa madai kwamba kufanya hivyo ni kwenda kinyume na maadili ya wananchi wa Zanzibar .
HIZI NDIO FAIDA ZA POMBE
FAIDA ZA POMBE BASI NYINYI KARIBISHENI MUTAONA MATHARA YAKE WATOTO WENU WAKIKE WATAANZA KULEWA WATAFIRIGISWA VIZURI MABARABARANI MAANA HAYO HAMUYAFIKIRI NYINYI MUNAFIKIRIA WATHAMINI TU NA MAPESA HASARA ZAKE HAMUZIANGALI SAWA
UKIKARIBISHA POMBE ZNZ HIZI NDIO FAIDA ZAKE
No comments:
Post a Comment