Wednesday, July 27, 2011

WABUNGE WA Z;BAR WANGURUMA NA KUWAKOMESHA WABUNGE WA TANG KWA KUIFANANISHA NCHI YA Z;BAR KAMA WILAYA.

HILI NDIO JUMBA LA WACHAWI WA TANGANYIKA KUWAROGA WAZENJI ILA MWAKA HUU UCHAWI WAO UMEPIGWA NA MZIZI WA MUARBAINI HAUFANYI KAZI TENA HAHAH

Bunge la la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeambiwa kuwa
Zanzibar ni nchi kwa kuwa ina Rais wake, katiba na bendera yake na isifananishwe  na wilaya yoyote yaTanzania Bara (Tanganyika) kwa sababu ya udogo wake.Kauli hiyo imetolewa jana mjini Dodoma na Mbunge wa jimbo la Ole Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohamed (CUF) alipomjia juu Mbunge wa Geita Donald Max (CCM) kwa kuifananisha Zanzibar kama Wilaya.Wakati akichangia hotuba ya wizara ya kilimo, chakula naushirika Max alisema kuwa wilaya ya Geita ina ofisa kilimo mmoja, wakati wilaya hiyo ni kubwa kuliko Kilwa na Zanzibar.Baada ya Mbunge  huyo kumaliza kuchangia hotuba hiyo, ndipo Mbunge wa Ole alipoomba kutoa taarifa kwaMwenyekiti wa Bunge Jenista Mhagama,  nakusema kuwa Mbunge aliyemaliza kuchangia ameitaja Zanzibar kama wilaya. Kauli ambayo ni ya kupotosha.“Mheshimiwa Mwenyekiti naomba kutoa taarifa, mchangiaji aliyemaliza ameitaja Zanzibar kama wilaya”, alisema Mohamed na kuongeza  “naomba kumpa taarifa kwamba Zanzibar ni nchi  ina mipaka yake, ina Rais, Katiba na Bendera yake. Tunataka hili suala likome”, alisisitiza mbunge huyo.Akiunga mkono hoja hiyo, Mwenyekiti  wa Bunge Jenista Mhagama alisema kuwa taarifa hiyo imezingatiwa na itaingizwa kwenye “hansard”, kwani inafahamika kwamba Zanzibar ni nchi.

No comments:

Post a Comment