Thursday, July 28, 2011

WARIOBA AROPOKA NA KUTAMANI KUTURUDISHA KTK ENZI ZA UDIKTETA WA NYERERE

WAZIRI Mkuu mstaafu, Joseph Warioba, amesema tatizo la Muungano linasababishwa na mamlaka zinazogombea madaraka na si wananchi.
Warioba ambaye alikuwa akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa (TBC), alisema kuwa muungano uliopo bado ni imara lakini wanaohitaji madaraka ndiyo wanaoufanya uonekane na matatizo.
Alisema wale wanaogombea madaraka wanapaswa kuchukua hatua ili isifike sehemu matatizo hayo yakawaletea shida wananchi.Warioba alisema wapo baadhi yao wanatoa sababu kuwa kuanzishwa kwa serikali tatu kunaweza kumaliza kero ya muungano, jambo alilosema kuwa halina ukweli wowote.
Kwa mujibu wa Warioba, uwepo wa serikali mbili malalamiko yanaendelea kujitokeza kila kukicha, hivyo alishauri kuwa wanaohitaji serikali tatu wasijidanganye kuwa zikianzishwa kero za muungano hazitakuwepo tena.“Wapo wanaohitaji serikali tatu na kwamba wanaona hilo ndilo jawabu, hawajiulizi juu ya je serikali tatu hazitakuwa na changamoto zake? Na kama zikija, hizo changamoto zinamalizwaje,” alihoji Warioba.
Akizungumzia kuhusu Bunge, Warioba alisema Bunge la sasa limeanza vibaya na halitoi mfano mzuri, hata lugha inayotumiwa na viongozi hao alidai sio ya staha bali ni ya kukejeliana.Alisema Bunge limekuwa la fujo, hatua inayowafanya wananchi mitaani kuambiana kuwa iwapo unahitaji burudani basi ni bora uangalie Bunge.
“Wananchi wanaambiana kuwa kama unataka burudani angalia Bunge maana unakuta malumbano hata vyama vilivyopo huoni msimamo wake…sijui linaonyesha mfano gani, lazima wachukue hatua,” alieleza.
Warioba alisema kuwa anaamini wabunge watakuwa wamesikia maoni ya wananchi, hivyo wanachotakiwa ni kutumia vizuri kanuni ili kurudisha nidhamu iliyopotea.Alisema Bunge lazima lichukue maamuzi magumu pamoja na kufuata maadili na ikiwa watafanya hivyo, alisema watarudisha hamu kwa wananchi ya kulitazama Bunge hilo.Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema wakati wa chama kimoja wananchi walikuwa wanapenda kipindi cha Bunge kwani walitenga muda wao na kusikiliza kupitia redio, bali kwa sasa teknolojia imekuwa hivyo wanajua kinachoendelea.Alisema pamoja na kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi, lakini Bunge limeweza kufanyakazi nzuri, kwa madai kuwa matatizo ya nchi ni magumu lakini Bunge la mfumo huo limejitahidi.
HILI ZEREE LINAWACHA KUKA NYUMBANI NA WAJUKUU ZAKE LIMO KWENYE TV KUROPOKA MAMBO YASIYOKUWA NA MAANA ATI BUNGE LA ZAMANI HAPO ZAMANI WEWE MWENYEWE SIKUWAHI HATA SIKU MOJA KUKUSIKIA UKISAMA NYOTE MULIKUWA MUKIMUABUDU NYERERE NA NDIO MPAKA LEO NCHI IMEOZA SASA Z;BAR ITAJIKOMBOWA NA SIO VIONGOZI WANAOTAKA MUUNGANO UFE NI SISI RAI NA TUNASEMA KWA SAUTI HATUTAKI MUUNGANO NA NYINYI NA HUU SIO MUUNGANO IMARA KAMA UNAVYO FIKIRIA WEWE AU UNAMANISHA NI IMARA KWA KUWA KUNAMAJESHI WENGI MULIOWAJAZA Z;BAR UNAONA NI IMARA WAZENJI HATUJAA AMUWA BADO ILA TUKIAMUWA BASI MUJUWE HAKUNA CHA JESHI WALA POLISI NYOTE MUTAIYONA NCHI CHUNGU AU MUME SAHAU MULIVYOCHAPWA NA WAGANDA MPAKA MKAJA KUCHUKUWA JESHI LETU LA NYUKI ZENJI NDIO MUKANUSURIKA BASI FUNGA DOMO LAKO KAA NA WAJUKU ZAKO UCHEZE NAO USUBIRI SIKU YAKO YAKUFA UFE TUKUZIKE USIJITUMBUKIZE NDANI YA SIASA UMEPITWA NA WAKATI WARIOBA.

2 comments:

  1. Wazanzibari mnagonjea nini? Hakuna manufaa yoyote katika Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. ACHENI MBWEMBWE NYIE, KWANZA FANYENI KAZI KWA BIDII SIO MNAKESHA KUDISCUSS SIASA HAMIWEZI HATA KIDOGO. ANGALIA KWANZA HATA NYANYA ZA KUPIKIA MNAAGIZA KUTOKA BARA KAZI YA MIDOMO MIPANA TU KAMA WANAWAKE WASIFUNDWA. MSIWATEGEE WA-MAKUNDUCHI KUFANYA KAZI YA KUZARISHA WALE WANA-ASILI YA BARA. PINDENI MIGONGO MFANYE KAZI SIO KUONGEAONGEA VITU AMBAVYO HAMVIJUI, ACHENI USHABIKI WA KIBWEGE HUO.

    ReplyDelete