Wednesday, July 20, 2011

SERIKALI YA TANGANYIKA YA ONYWA NA RAI KWA KUWAPA WANYARWANDA ARDHI NA URAIA WA KITANGANYIKA


 
HAYA NI MAFUVU YA VICHWA VYA WATU  NA MAITI ZA WATU WALIO ULIWA KWA MAPANGA KATIKA VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE NCHINI RWANDA SIJENGI CHUKI ILA TUNATAHATHIRISHANA NAMAPEMA MAANA WAKIPEWA URAI NA RDHI TANGANYIKA BASI NA ZNZ WATAFIKA MAANA TUNAO WABURUNDI NA VITAMBULISHO VYA KIZENJI HAYA BASI SASA NA WARWANDA HAO.
Serikali ya tanganyika inafanya hivyo ati ikiwa ni kuimarisha udugu wa kiafrika mashariki na kati kwa kuwa warwanda ardhi, uraia (EAC) Serikali imeshauriwa kuzingatia maoni ya wadau waliyoyatoa wakati wa mchakato wa kutafuta jinsi ya matumizi ya ardhi katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika suala la kutoa ardhi na uraia kwa wananchi wa Rwanda .Aidha serikali imetakiwa kuepuka kutoa maamuzi kwa wepesi katika masuala mazito, hasa yanayohusu kulinda maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.Hayo yalielezwa na mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu mkoa wa Tanga, Asseli Shewally, wakati akisisitiza umuhimu wa serikali kufuata maoni ya wadau waliyoyatoa kupinga matumizi ya pamoja ya ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Shewally, alisema kuridhia kutoa ardhi na uraia kwa wananchi wa Rwanda inaonyesha kwamba serikali haikuelewa maana ya wananchi kupinga matumizi ya pamoja ya ardhi ndani ya ushirikiano wa nchi EAC.“Suala hili la ardhi na kutoa uraia si la kunong’onezana ni la kitaifa na kulifanya siri ni makosa. Serikali inaonekana kufanya maamuzi kuwa wepesi katika masuala mazito kama haya, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shewally.Alisema lengo la wadau kupinga matumizi ya ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuilinda isichukuliwe na mtu na badala yake itumike kwa manufaa ya wote na vizazi vijavyo na kwamba kuwakabidhi raia wa Rwanda ni sawa na serikali kutoa ardhi kwa mlango wa nyuma.Alitahadharisha kwamba, endapo serikali haitakuwa makini na suala la ardhi na ikaendelea kuitoa kama zawadi kwa nchi marafiki athari zake zinaweza kujitokeza miaka 35 ijayo, ambapo maamuzi hayo yataweza kusababisha kuzuka migogoro mikubwa ya kugombea ardhi baina ya wazawa na raia wa kigeni.Hata hivyo alimtaka Rais Jakaya Kikwete na serikali kwa ujumla kutambua kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaimezea mate Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo ardhi na kuwasisitiza Wabunge kuwa wawakilishi wazuri wa wananchi katika kupinga suala hilo.
WATU WALIO UWAWA KTK VITA YA RWANDA
 

HAYA ZANZIBAR TUKAE MKAO WA KULA MAANA JUZI JUZI BILAL ALISEMA WALIOCHOMEWA VIBANDA ZENJI WAPEWE ARDHI SASA WARWANDA NA NCHI NYENGINE WASHAUNGANA NA TANGANYIKA KTK AFRIKA MASHARIKI NA KATI TUSISTAJABU TUKIAMBIWA KUWA SASA MICHEZANI WANAPEWA WARWANDA MAANA WANAJUWA 2015 WAKIWAMBIYA PIGENI KURA HAPA WATAPINGA MAANA WASHAONA ZENJI WATU WOTE WAMESHIKANA HAKUNA TENA MAMBO YA VYAMA NI ZENJI KWANZA KISHA NDIO MAMBO MENGINE SASA HII NDIO KAMPENI YAO MPYA KUTUJAZIYA WAGENI WAKUTOKA NCHI NYENGINE ILI 2015 WAPATE WATU WAKUWAPINGIA KURA BASI TUWE MACHO WAZENJI.

No comments:

Post a Comment