Wednesday, July 6, 2011

TANG-WAMESHIBA HAWAMJUWI-MZ;BAR-MWENYE NJAAA






Mimi nimefuatilia sana ktk vikao vyetu vya ndani vya Baraza la wajumbe wa Uwakilishi na kumalizia mkutana wa 3/7/11 wa Kibanda maiti alio elezea mengi Mh Makamo wakwanza wa Rais na katibu mkuu wa Chama cha Wananchi Cuf Maalim Seif shariff Hamadi.
Ndugu waugwana wa kizazi cha Wzanzibar, kifupi tu alio zungumza Mh Maalim Seif nikweli na viongozi wingi wanaonyesha imani hio hio ya kutafuta rai na mbinu za kufufua na kukuza uchumi wa Zanzibar ili Wzanzibar watokane na umaskini ulio kithiri na maisha magumu yalioko Zanzibar.
Hii imetokana ktik vikao vya ma-Baraza yetu mawili yani Bunge na Baraza la Uwakilishi ambalo ndio Baraza letu la Ndani na lina (Fluency) kubwa na ndio uti wa mgongo wa Zanzibar na tunaweza kusema kuwa Baraza letu la Uwakilishi ni Bora lenye nguvu kwa hatma ya mustakbali wa Zanzibar kuliko Bunge lenye pasentege ndogo ya Wabunge kutoka Zanzibar.
Hivi sasa tokea kundwa kwa Serekali ya Umoja wa kitaifa (SUK) kumejitokeza matumaini makubwa kwa Wzanzibar ya kuweka pembeni tafauti zetu za kisiasa na mivutano na zarau ktk Baraza, haya yote yalikuwa haimnufaishi mtu isipokuwa ni kuiteketeza Zanzibar na kuzidisha migawano na tafrani kwa raia wetu wa Kizanzibar. hili nijambo kubwa la kushukuru mola na Baraza letu la sasa.
Sasa tuje katika maswali na mikakati ya rai ya kukuza uchumi wa Zanzibar? vipi uchumi wa Zanzibar unaweza kukuwa na kuimarika? na nikizingiti gani kinacho zuia uchumi wa Zanzibar usikuwe hali yakuwa huko nyuma maisha yalikuwa afathali kuliko maisha ya sasa tunayo kwenda nayo siku hadi siku?.
Wzanzibar wengi wamesha baini kuwa kinacho uwa uchumi wa Zanzibar usikuwe au kunawirika, nimfumo huu wa Muungano tulio nao haupi fursa Zanzibar kushughulikia mambo yake ya umuhimu kwa kuimarisha uchumi bila kupata ticket kutoka Tanzania Bara, hii ni kubana kila sehemu yenye kuvuta punzi Zanzibar imeekewa kizibo malum cha kukisia hewa ingiayo na itokayo.
Na swala hili ndio kero kubwa sana la Muungano kwa Wzanzibar kutaka uvunjike na usirudi tena, Zanzibar inaweza kupiga hatuwa kubwa zaidi kuliko Tanzania Bara kwanza wananchi wake ni kidogo na Zanzibar kuwa na sehemu nyingi tu za vivutio vya uchumi bila kutegemea hata hayo mafuta?. mfano
Ikiwa Zanzibar itajitegemea wenyewe ktk kuekeza maswala ya Free-port, Utalii, Uvuvi na kilimo cha kisasa Basi Zanzibar inaweza kupiga hatuwa za haraka mno, lakini hii inahitaji Zanzibar wenyewe waweze kuwa huru kwa mambo yake wenyewe bila kuingiliwa na Tanzania Bara.
Hivi sasa Zanzibar haiwezi kuomba hata Panadol or Aspirini kutoka jirani yetu Kenya kama hatuja pewa kibali kutoka Tanganyika na tutambiwa maswala hayo ni ya kigeni kwa hio ni mambo ya Muungano nilazima muzungumze na Mh Bened Membe awepe kibali, lakini chakushangaza uchumi wa wenzetu unakuwa na wakitoka kwenda kuomba misada njee hawahitaji kibali kutoka Zanzibar wao hujitokea tu, hata liwe jambo lile ni Muungano linatuhusu sote basi wao huondoka bila hata kuaga.
Jengine lakushangaza Muungano huu ulivyo chafuka na kuondosha uhalali wake na uaminifu wake nipale Zanzibar inapo wakilishwa kwa mambo ya Tanganyika yasio ya Muungano kufanywa kimataifa ni ya Muungano, mfano misada ya realway hii huombwa kwa jina la Tanzania lakini ikisha fika hutumika kwa jina la Tanganyika bila Zanzibar kufaidika chochote. na iko misada mingi tu wenzetu huomba kwa Ngao ya Tanzania lakini ikifika hutumika ndani ya Tanganyika na Zanzibar hainufaiki.
Na sisi Zanzibar tunapo kwenda njee ya nchi kuomba misada imekuwa vigumu kupewa, kwa vile wenzetu wamesha kwenda kupaka sumu kali kuwa nchi ni moja tu nayo ni Tanzania ndio muweze kuitambua Zanzibar sio nchi kimataifa, sasa hapa hukwama Zanzibar kuweza kusaidiwa kama nchi, ndio ukaona miradi na misada mikubwa mikubwa huishia Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Hata maswala ya Michezo Zanzibar tumekataliwa na tumeambiwa haitambulikani kuwa Zanzibar ni nchi, nchi inayo tambulikana ni Tanzania tu, sasa hili ndio kero kubwa la Muungano ambalo hata katiba yetu mpya ijayo na Baraza letu tukufu la Uwakilishi halija lizungumzia kuhusu kufufuka kwa Tanganyika na katiba yake ya Tanganyika itakayoweza kusimamia mambo yake yasio ya Muungano, kuliko utata huu tulionao ya mmoja kujifanya mjanja na kumzuthulumu mwengine na kufaidika yeye.
Mimi na hisi bila ya kuwepo Tanganyika wazi wazi ambae ndio mshirika ktk mkataba wa Muungano basi Zanzibar haitokuwa kiuchumi na itaedelea kuminywa kwa kisingizio cha Tanzania kwa faida za Tanganyika nyuma ya Pazia.
Kukiwepo Tanganyika inaweza kuondosha wasi wasi wa kila upande kuhisi unanyimwa haki zake za ndani zisizo za Muungano, bila ya hivyo tutageuzwa Punda mwenye kufanya kazi ngumu na jioni hapewi hata chakula nyeye ni kumfaidisha Bwana wake tu kwake yeye 0000000000.
Maana mikakati na uzio wa kuzuia uchumi wa Zanzibar usikuwe ni mingi kuliko fursa zenyewe, Kifupi Zanzibar ina watu 1.2 yani million 1 na laki mbili ? lakini hivi sasa wachilia mbali uchumi kukuwa ajira nyingi zikiwemo za utalii na utumishi wa kazi basi zimeshikiliwa na wageni kila ofisi ya serekali na biashara za kitali ni watanganyika sasa hii ni zanzibar au morogoro,mwanza,arusha au mbeya...? na huku wazanzibar walio wengi wakihaha kwa maisha magumu bila kazi mtu akiamka huishia vijiweni(maskani).
Lakini Utalii,Uwajiri wa Jeshi la wananchi,utumishi Serekalini Zote hizo hunufaika Zaidi wakuja kuliko wenyeji wenyewe,yani wazanzibar hivi karibuni nilishangaa na nikasema kweli Zanzibar ni nchi isio na wazalendo, maana nilipita forodhani ktk Jumba la makumbusho alilokuwa akikaa mfalme naona vijana wengi wafanya kazi wa pale ni watu wa kutoka tanganyika watu wa Bara na wamepikwa au wamejipika kichuki na kibaguzi maana historia wanayo mlisha mzungu pale ni chafu na niyachuki kwa kizazi cha Zanzibar ambacho kina mchanganyiko wa Rangi na makabila.
Sasa sehemu kama hizi za historia ya nchi yetu wanapewa watu wasio wa Zanzibar kuielezea tena vile wanavyotaka wao kweli amani na utulivu utapatikana Zanzibar.? kuna mambo nilazima tujifunze kutokana na wenzetu na mifumo yao walivyo ungana, nchi nyingi zilizo ungana ktk nchi zilizo endelea basi kila nchi wameungana kukuza uchumi sio kuuwa uchumi wao, kila nchi inalinda rasilimali zake za ndani na uchumi wake sikwamba wameunganisha yote kama hivi sie kupeleka kila chetu.
Mfano hai tu ni hivi karibuni ktk EU Ugerumani na Ufaransa waliweka utaratibu kamili hafla baada ya kuona wanapokea wagonjwa wengi wenye marathi sugu na makubwa kuja kutibiwa free, sasa na sisi ikiwa tutaimarisha wizara ya Afya na Elimu na mambo mengine mengi tu, bila ya kuweka kiwango na utaratibu maalum kweli Zanzibar tutaweza.? maana makundi ya wageni yatakayo miminika kwa vile milango iko wazi na Zanzibar ni huru atakae aje? tutabebeshwa mzigo tusio uweza.
Nilazima tuwena na utaratibu mpya wa Muungano huu umeshapitwa na wakati maana Tanganyika inajinufaisha peke yake kwa jina la Tanzania na Zanzibar hatunufaiki chochote isipokuwa wakati mwengine kupewa % 4.5 tena kwa kuvutana.
Kama tunataka Muungano wa kweli basi nilazima katika marekebisho ya katiba Tanganyika irudi kuja kusimamia mambo yake yasio ya Muungano na tukae pamoja kwa mambo ya Muungano yasio ya Muungano tuachieni wenyewe Wzanzibar tupapatuwe kivyetu, mimi hushangazwa na viongozi wetu kuwacha kuwatetea Wzanzibar walowengi ndani ya Zanzibar kutokana na mauthi ya Muungano na hutetea Muungano kwa Wzanzibar wachache wenye kujiweza waloko Tanzania Bara.
Mimi nasema hakuna mtu asonakwao hata Muungano uvunjike wanakaribishwa kurudi Nyumbani na kuja kukuza uchumi wa kwao,au wabaki huko huko ndio demokrasi ati tuna dugu zetu wangapi wanaishi U.K.,OMAN,CANADA,AMERICA,U.A.E NA EU wameja huko na wanaishi itakuwa hawa wa bara wataendeleya kuishi na watakuwa na passport  ya kitanganyika wakitaka kuja zanzibar watatambulika ni watanganyika basi hakuna tatizo. haiwezekani wao kuwa ndio kigezo na kikwazo cha Muungano, maara zote tusimamishe haki ya wengi ambayo ni Wzanzibar waloko ndani ya Zanzibar ndio Wazalendo na wenye kulinda nchi yao tusijaribu kubabaisha hoja na kutumia vigezo vya kidogo kwa kuwacha wengi kuteseka.
Muungu ibariki Zanzibar na Wzanzibar wote.

No comments:

Post a Comment