Wednesday, July 27, 2011

KATIBU MWENEZI WA CCM Z;BAR,ISSA HAJI GAVUUUU AZUKA NA UNAFIKI WAKE HUKU AKIJARIBU KUWAGAWA WAZENJI KWA KUTUMIYA UCHAMA


 SISI WAZENJI WOTE NI KITU KIMOJA HAKUNA TENA CCM WALA CUF BALI KUNA UZENJIBAR BASI SASA WEWE GAVU,KAVU,VUKUTU USITULETE SERE ZAKUTAKA KUWATENGANISHA WAZENJI KWA KUTUMIYA UCHAMA UCHANGUZI WA 2010 WALIYOSHINDA NI WAZANZIBAR SIO CHAMA SASA WEWE KAVU KAMA HUNA LA KUSEMA NYAMAZA AU UJUWE NYOTE WANAFIKI TUNAWAREKODI SIKU ZNZ IKIPATA UHURU WAKE BASI NYOTE MUWE KULEE TANGANYIKA KWA WANAFIKI WENZENU MUKIBAKI HAPA MUMEKWISHA TUNAWAMBIYENI KABISA NA MIKONO YETU IMEUNGANA NA KUWAZOMEYA NYINYI WANAFIKI VIBARA WA WATANGANYIKA.
Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kimeahidi kuendelea kutetea muundo wa serikali mbili katika sura ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Katibu Mwenezi wa CCM Zanzibar, Issa Haji Gavu, alisema kushindwa kutetea sura ya sasa ya Muungano ni kwenda kinyume na sera na ilani ya uchaguzi ya chama hicho.Gavu alisema chama chake kinaamini sura iliyopo ya Muungano inazidi kuungwa mkono na wananchi wengi na ndio maana kikashinda Uchaguzi Mkuu mwaka jana.Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya vipeperushi kusambazwa mjini Zanzibar kumtaka Waziri wa Kilimo, Mansour Yusufu Himid, kujiuzulu kwenye nyadhifa zake baada ya kuunga mkono Muungano wenye muundo wa serikali tatu.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Ardhi, makazi, Maji na Nishati, Mansour ambaye ni mjumbe wa NEC na Katibu wa Idara ya Fedha na Uchumi ya CCM Zanzibar, alisema Muungano wa sasa ni butu na wakati umefika wa kuangalia mwelekeo wa serikali tatu.Katibu huyo Mwenezi wa CCM aliwaambiwa waandishi wa habari kuwa viongozi wanaodai serikali tatu wanapingana na sera na ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
“CCM itaendelea kulinda na kutetea muundo wa serikali mbili katika mfumo wa Muungano kwa sababu sera hiyo ndiyo iliyotupatia ushindi katika uchaguzi mkuu mwaka jana,” alisema Gavu.Alisema kwa msingi huo wanachama na viongozi wanatakiwa kusimama imara kutetea serikali ya serikali mbili, lakini kila mwananchi atakuwa na uhuru wa maoni utakapofika mjadala wa Katiba mpya.Kuhusu mpango wa CCM wa kusafisha chama, Gavu alisema kujivua gamba hakumaanishi kuwafukuza viongozi, bali ni kuwataka kujisafisha na kurudi katika maadili ya uongozi.“Dhana ya kujivua gamba ndani ya Chama cha Mapinduzi haina maana kujiuzulu au kuwafukuza watu katika chama, watu hawakumwelewa Mwenyekiti wetu, lengo ni kujisafisha nakurudi katika maadili ya uongoz,i” alisema Gavu.Hata hivyo, alisema viongozi ambao watashindwa kujirekebisha kutokana na vitendo vyao watalazimika kujiondoa katika chama ili kufanikisha kuimarisha chama hicho.Hata hivyo, alisema mpango wa viongozi kuvua gamba unatakiwa kutekelezwa kwa watendaji na viongozi wanaoshutumiwa Tanzania Bara na Zanzibar kwa sababu tayari chama kimepitisha azimio hilo

No comments:

Post a Comment