MNATAKA NINI KTK VISIWA HIVI WATANGANYIKA..?
NCHI YENU TANGANYIKA INA KILA KITU NA KUBWA NA TAJIRI
HAMUJA TOSHEKA TU BADO MUNATAKA KUVIMEZA VISIWA...?
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imesema mpango wa kuanzishwa kwa akaunti ya pamoja ya fedha kati ya SMZ na Serikali ya Muungano (SMT) upo katika hatua za mwisho.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Fedha, Uchumi, Mipango ya Maendeleo
Omar Yussuf Mzee alisema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Chake Chake kwa tiketi ya CUF, Omar Ali Shehe aliyetaka kujua suala la akaunti ya pamoja limefikia wapi hadi sasa.
Omar Yussuf Mzee alisema hayo wakati akijibu swali lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la Chake Chake kwa tiketi ya CUF, Omar Ali Shehe aliyetaka kujua suala la akaunti ya pamoja limefikia wapi hadi sasa.
Mzee alisema kifungu cha 133 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka kuanzishwa kwa akaunti ya pamoja ya fedha, ambayo itawekwa fedha yote itakayochangiwa na serikali mbili ya SMZ na SMT.
Alisema fedha zitakazochangwa ni kwa madhumuni ya shughuli za muungano wa Tanzania kwa mambo ya muungano tu.
Akifafanua kutokana na matakwa ya kifungu hicho cha katiba pamoja na sheria ya tume ya pamoja ya fedha, imetoa vigezo mbalimbali ikiwemo mwongozo kuhusu akaunti ya fedha ya pamoja itakavyokuwa inaendeshwa ikiwa ni sehemu ya mfuko mkuu wa serikali ya SMT umewasilishwa Septemba 2009.
Kwa upande wa SMZ ilitafuta mshauri mwelekezi kuishauri serikali kuhusu mfumo wa mgawanyo wa matumizi ya akaunti hiyo.
No comments:
Post a Comment