Wednesday, July 27, 2011

WAKATI UMEFIKA WA Z;BAR KUPATA MSADAA WALIO UWOMBA MIAKA MINGI KWA WAJARUMANI


Kuna tetesi za ukweli kuwa Zanzibar iliwai kufanya — kutiliana mkataba wa kujihami na Ujerumani. Mkataba huu ulikuwa na vipengele vingi vya kisheria na ustawi wa nchi.Kuna habari pia kilichomfanya Marahemu Idrissa Abdulwakil ‘kulazimishwa kujiuzulu’ na Nyerere ni pale alipofanya ziara ya Ujerumani bila kuwarifu au kutaka idhni ya wafalme wetu wa Tanganyika; na marehemu Idrissa alikuwa na azma ya kufufua mkataba huu au kuanzisha makubaliano mapya.Mimi sina fikra sahihi za 100% juu ya mkataba huu. Naomba anayejua atupe kidogo tupate ‘kuchakachua’ fikra zetu.Inaweza isiwe kitu sana lakini KATIBA MPYA INAKUJA: NCHI MOJA, KATIBA MOJA.Ahsateni Sana
Na Utawala wa DK.Shein mambo yamewiva. Sasa wakubwa na watendaji wake wanashutumiana wao kwa wao.Juzi baada ya Hamada Rashid kumuliza Mizengo Pinda kuwa ‘wapo wakubwa wa CCM na serikali wanauvuruga maridhiano na wanamdharau Maalim Seif”.Wengine wamethubutu kumuiita Maalim Seif “mbwa’. Hii haina shaka….iko siku tutawataja hapa ukumbini dhahir.Ukweli hasa Dr.Shein amezungukwa na watu waharibifu (spoliers) wakiongozwa na King wao Abdulhamid Yahya Mzee. Amezungukwa na watu wala rushwa, amezungukwa na watu wabaguzi…almuradi GNU haifai. Imekuwa ni kikwazo zaidi kwa maendeleo ya Zanzibar kuliko ilivyotarajiwa.Imefikia hadi mpaka barua inayokwenda kwa Rais Shein, lazima ipekuliwe na ‘vishawishi wake’. Wanadai kuwa Dr.Shein ni ‘Mpemba” kwa hivyo haaminiki. Allah yaalamu…..kama Shein ni ‘Mpemba’ au la. Tusubiri Katiba Mpya ituzike kabisa (kaburi letu lipo pale Mwanakwerekwe) la Zanzibar.

No comments:

Post a Comment