Thursday, July 14, 2011

JAJI MKUU WA Z;BAR AJIPENDEKEZA KWA MAJAJI WA KITANGANYIKA NA KUTAFUTA ULAJI MPYA NCHINI TANGANYIKA

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu

Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, ametaka kuwepo kwa ushirikiano wa majaji baina ya Tanzania bara na Zanzibar kwa lengo la kubadilishana uzoefu.Alitoa rai hiyo jana jijini Dar es Salaam alipotembelea Mahakama Kuu, Mahakama ya Kitengo cha Biashara na Mahakama ya Rufaa.
Alisema kitendo hicho kitasaidia kupeana uzoefu mbalimbali katika kufanya maamuzi mazuri katika kesi.
“Kama ingekuwa na uwezekano tubadilishane majaji ili wa Zanzibar waje Tanzania Bara na wa huku waende Zanzibar ili tubadilishane uzoefu,” alisema.Alisema lengo kubwa la ziara yake ni kutaka kujifunza pamoja na kujionea shughuli za mahakama zinavyofanyika na mambo mengine ya mahakamani.
Jaji Makungu alisema amefurahishwa na utendaji kazi wa mahakama ya Tanzania Bara kwa kuwa zinatumia teknolojia ya kisasa katika kuendesha kesi kwa kutumia njia ya mtandao.Alisema jambo hilo likifanikiwa kufikishwa katika mahakama zote litasaidia wananchi kupata taarifa za umakini dhidi ya mashauri yao.
Naye Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, alisema mahakama ya Zanzibar na ya Tanzania Bara zinatakiwa kuendeleza ushirikiano pamoja na kuelimishana mambo muhimu.Alisema kuna haja ya kusaidiana zaidi kutokana na kwamba sheria ni moja inayotumika, hivyo zinapaswa kushirikiana ili kuimarisha utoaji haki.Hata hivyo, Jaji Othman alisema Zanzibar na Tanzania bara zinakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti lakini serikali imeanza kulishughulikia.Msajili wa Mahakama ya Kitengo cha Biashara, John Kahyoz, alisema kwa sasa wameanzisha huduma mpya kwa wale wenye kesi katika mahakama hiyo kujipatia taarifa kupitia simu ya mkononi.Alisema lengo ni kupunguza mrundikano wa watu mahakamani, hivyo mtu kama atakuwa amechelewa kufika katika kesi yake anatuma ujumbe wenye maneno mafupi kwa kuandika kesi na namba yake kwenda namba 15564 kisha atapatiwa taarifa kama imeahirishwa au la.
Kahyoz alisema ifikapo mwakani wataanzisha kioski ambacho kitatumiwa kama mashine za ATM kupata huduma za kesi zinavyoendelea mahakamani badala ya kumtafuta karani atoe taarifa
HII NDIO MAHAKA KUU YA ZANZIBAR AMBAYO IKO UNGUJA
HII NDIO MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR AMBAYO IKO PEMBA
HII NDIO MAHAKAMA KUU NCHINI TANGANYIKA AMBAYO IKO DAR

SISI TUNAPINGANIA NCHI WEWE UNASEMA WAJE Z;BAR NA NYINYI MWENDE TANGANYIKA SIO. MAANA MUNAVYO IBA HAPO ZNZ HAVIWATOSHI KAMA KWELI UNATAKA MAENDELEYO NDIO PAKUSIMAMA NA KUKAZANIA SEREKALI KULETA MAMBO MAPYA NA TOKONOLAGIA SIO WEWE NA WENZAKO KWENDA BARA NA WABARA WAJE ZNZ.AU NDIO MBINU YENU YA KUTAKA KINA JAJI KIBATARI,JAJI MAKARANGIRA WAJE ZNZ KISHA SISI TUKIPIGANIA HAKI WATUSHIKA NA KUTUPELEKA MAHAKAMANI NA JAJI KIBATARI ASEMA TUNATISHIA AMANI YA NCHI MIAKA MIA JELA SASA MNATUPELEKA WAPI..? HAO MAJESHI NA POLISI NA WAUZA VINYANGO HAWATOSHI MUNATAKA KUTULETEYA NA MAJAJI SASA AU NDIO MUKO MBIONI KUUNGANISHA MAHAKAMA. ILI TUWE NA MAHAKAMA MOJA IKIFIKA 2014 WANALETA KATIBA MPYA NDIO ZANZIBAR ISHAKUFA HAKUNA TENA NCHI MAANA CHAMA KIMOJA KATIBA MOJA MAHAKAMA MOJA JESHI NA POLISI MOJA NA VYOTE VIMESHIKWA NA WAO.JE HAPO TUTAITA ZANZIBAR NCHI LABDA KACHORI NA BATATA ZA UROJO. NDIO TUKASEMA ZNZ INAULIWA NA WAZENJI WENYEWE NA ZNZ INAFANYWA IMEZWE NA WAZENJI WENYEWE PIA ZNZ HIHI ITATETEWA NA KUPIGANIWA UHURU WAKE NA WATU WENYE MOYO SIO NYINYI WANAFIKI WATAPIA MLO MSHIPA USHAKUSIMAMA WAKUTAKA KULA ZAIDI DUUUUH.UNAONA Z;BAR HAIKUTOSHI BORA UJIPELEKE BARA.AKILI ZENU ZIKO WAPI NYINYI..?HAYA NDIO MARADHI YA KUNUNUWA VYETE WATU KAMA HAWA HAWAKUPASI KILILAHI WAMENUNUWA VYETE WEE MPAKA WAMEFIKA NGAZI ZA JUU NA HAYA NDIO MADHARA YAKE SASA YA KUNUNUWA VYETI.M/MUNGU ILINDE ZANZIBAR NA VIONGOZI MAJAHILI.

No comments:

Post a Comment