Monday, July 4, 2011

NCHI TANZANIA,KATIBA YA TANZANIA Z;BAR HAKUNA ZNZ NI MKOA WA PWANI Z;BAR



Inawezekana mkaniona kama vile ‘kichekesho’ kwa kuzungumza mada hii mara kwa mara. Lakini tufahamau kuwa mada hii inayohusu katiba mpya ya TZ, ndio itakuwa bakora ya mwisho ya kutumaliza Wazanzibari, Uzanzibari na Zanzibar kama taifa.
Ukweli ni kuwa Wazanzibari wengi, au wote tunajinasibu sana na UTAIFA wetu, na naamini sana hatuko wanyonge,yaani tunaona fakhari kubwa na tunajinasibu mbele za watu wote. Na hata wale wanaotuona kuwa ‘si chochote si lolote” — hawa Watanganyika, tunapokuwa nje ya nchi hii wanatuona na wanatuonea choyo heshima tunayoipata mbele ya macho ya wengine tunapojitambulisha kama sisi ni Wazanzibari; maana ni kuwa sisi ni watu tunajulikana kwa uaminifu – less corrupt, wakweli, watu wenye akhlak…tabia nzuri, heshima n.k.
Hata hivyo, wenzetu, kwa sasa, hawa akina Pinda, Makinda, JK na CCM wake — wao slogan yao ni moja tu: NCHI MOJA, KATIBA MOJA.
Unafahamu nini unapoambiwa hivyo? Maana yake ni kuwa kama Tanzania tulikuwa tunasema ni “mmungano wa Tanganyika-Zanzibar” sasa hiyo inapotea na kuwa TANZANIA YA MOJA KWA MOJA, NA ZANZIBAR INAFUTIKA. KATIBA MOJA: maana yake hata ile katiba yetu ya Zanzibar ya 1984, aliyoisasisi Aboud Jumbe (then amefukuzwa) pia itakuwa haipo. Unaweza kudhani kuwa hii ni ‘joke’. NO. Akina Pinda wana maana hiyo, isiwepo tena Zanzibar.
JK anataka kumalzia Urais wake vizuri kwa kukamilisha kazi ya kanisa kwa ku-exchange utaifa wa Zanzibar. Sasa, kazi kwetu.
Enzi za miaka ya 80 na kidogo 90s, Zanzibar ilikuwa angalau inaweza kusema NO. Sasa, Shein, hawezi kukhalifu miadi ya CCM Tanganyika, na wateule wake. Hilo tulijue.
Atajifanya anafuata process/mchakato wa katiba; itapobidi kuamua, ataamua yeye.
Ni kweli kabisa kuwa tayari cabinet ya Zanzibar tayari imeshatekwa katika suala hili. Wao, ni watu wa YES – tena YES kubwa ya katiba mpya. Na Abubakar Khamis Bakari – ndiye kiranja wao. Abubakar haaminiki, hana msimamo. Amefanya mambo mengi ya kuiuza Zanzibar, na hata juzi tu amewauza wenzake wa CUF kwa kuwapatia VP1 bandia kwa ile private motion yake. Sasa, CUF wanajuta kuingia serikalini, na hata kupewa hicho cheo cha VP1.
Maalim Seif, VP1, hana kazi, hajulikani kazi zake hasa, hata bajeti yake imeundwa kwa mfumo wa kutengezwa zaidi kuliko uhalisia. Mkitaka ulizeni, mtaambiwa kuwa bajeti ya ofisi ya VP1, watendaji wake wamethubutu kusema kuwa ‘VP1 sio mwakilishi wa wananchi, hajulikani kazi zake pia mwenye hivi majuzi juzi tu kasema dar kwenye tv kuwa tanzania ni yetu wote sasa tukae kwa amani sisi z;bar tunasema z;bar ni yetu yeye seif asema tanzania ni yetu je hajatugeuka tu...?kama hatuja amka wala hatuamki tena natukumbuke seif mwenye alikuwa CCM najuwa kuna watu watakasirika kwa mimi kumtaja kipenzi chao seif ila huo sio umoja,ukweli na mashirikiano ya kizanzibar ikiwa mwengine akifanya kosa akosolewe lakini seif akifanya kitu basi asiguswe hivyo sio kuendeleya,mimi sikatai seif kafanya mengi ktk znz mpaka kufika hapa tulipofika ila je alikokuwa akitupeleka ndiko..?au alikuwa tu akitupeleka ili tusiwe na mawazo ya kutafuta kiongozi mwengine...?maana sasa nakumbuka hata siku alipozungumza na nyerere kule butiama na aliporudi znz akakata kusema nini kazungumza na nyerere na akasema mpaka nitakufa simuambi mtu je ni siri gani kubwa..?basi kama tutaikubali katiba mpya znz tujuwe ndio haiko tena ndio imekwisha.tayari washasema kuwa  seif  hastahiki kupata pesa nyingi kuliko ofisi ya VP2″. Kama mtaona porojo, ulizeni! Hiyo ndio GNU aliyoiunda Hon.Abubakar Khamis Bakari.
Sasa, mada yangu inahusu katiba mpya. Kama tutamtegemea sana mtu kama Abubakari basi tumekwisha. Mimi nionavyo, simply, tuikatae katiba mpya hata kama itakuwa ‘sweet’ kiasi gani kwetu. Na ninakuhakikishieni, haitokuwa. sweet kwa sababu hata siku Tanganyika, haiwezi kuipa haki Zanzibar. Hilo weka akilini mwako

No comments:

Post a Comment