Friday, July 1, 2011

MKURUGENZI WA MANISPAA ZNZ ASHATAKIWE TU AU YEYE NI RAISI WA Z;BAR..?


Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Zanzibar, Rashid Ali Juma katika mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) ofisini kwao Wekesi Kikwajuni siku chache baada ya matatizo yaliojitokeza kati ya Baraza la Manispaa na wafanyabiashara wa maduka ya Makontena Darajani ambapo maduka yote yalifungwa kutokana na amri ya huyu fur-uni japo kuwa mahaka ya znz iliamuwa yafunguliwe lakini yeye akasema yasifunguliwe je yeye ndio raisi wa znz sasa....??????
MKURUGENZI MANISPAA AWAJIBISHWE
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wameliweka “kiti moto” Baraza la Manispaa Zanzibar kwa kutaka Mkurugenzi wake awajibishwe  kwa kuikosesha serikali mapato ya mamilioni ya fedha.
Wakijadili makadirio ya bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (Ikulu) kwa mwaka huu wa fedha wa 2011-2012, wajumbe hao walisema manispaa hiyo inaikosesha serikali mapato kwa kuingia katika mikataba yenye lengo la kuwanufaisha watu binafsi.
Mwakilishi wa Kiwani (CUF), Hijja Hassan Hijja, alisema mikataba hiyo inahusu ukodishwaji wa Bustani ya Jamhuri kwa gharama ya shilingi milioni moja kwa mwezi, lakini baada ya kulipwa fedha hizo, shilingi 900,000 kati ya hizo zinazirudisha kwa mkodishaji ikiwa ni gharama ya matunzo ya bustani
Alikiambia kikao cha baraza hilo kinachoendelea Chukwani Mjini hapa kuwa
mkataba wa ukodishwaji bustani hiyo huo ni wa muda mrefu, lakini kutokana utekelezaji wake haoni kama utainufaisha serikali kimapato.
“Kila mkodishaji anapolipa shilingi milioni moja, kati ya hizo shilingi 900,000 zinarudi kwa mkodishaji kwa maelezo kuwa ni za kugharamia matunzo ya bustani, hapa pana harufu ya rushwa mheshimiwa Spika tunahitaji maelezo sahihi katika hili” alisema Hijja.
Mbali na kuikosesha serikali mapato, Hijja alisema uamuzi wa manispaa hiyo kufunga maduka 84 ya wafanyabiashara wa Darajani, kilikosesha pia serikali mamilioni ya fedha kitendo ambacho kinapaswa kuangalia kwa undani zaidi.
Alisema maduka yanalipa kodi kutokana na maduka hayo inaingiza serikali kiasi cha shilingi milioni 760 kila mwaka kutokana na kodi ya kila mwenye duka kwa mwaka.
Hijja alisema katika kipindi cha miezi sita kinachoishia mapema mwaka huu, maduka hayo yalifungwa kwa amri ya manispaa na kwamba hatua hiyo ilisababisha serikali kupoteza mamilioni ya fedha kwa kukosa mapato hayo.
“Maduka hayo yalifungwa kwa miezi sita kwa amri ya manispaa, serikali imepoteza mamilioni ya shilingi lakini mara mahakama inasema maduka yafunguliwe sasa hapa lazima tuwe makini katika masuala haya ya mapato kuna vitu vinafanyika huku baraza la manispaa hayaeleweki ni watu wachache wanatumia madaraka vibaya ” alisema Mwakilishi huyo ambaye yupo barazani kipindi cha pili
Alisema mkataba wa ukodishwaji wa Bustani ya Jamhuri na kufungwa kwa maduka katika eneo la Darajani kumesababisha mgogoro mkubwa kati ya serikali na wafanyabiashara jambo ambalo serikali ilitakiwa kuliangalia suala hilo kabla ya kuamua maamuzi ambayo hayana tija kwa wananchi wake na kusababisha wanachi kuichukia serikali yao kutokana na mamuzi ya watu wachache wenye kutumia vyeo vibaya kinyume na dhana ya uwajibikaji na utawala bora.
Alisema hatua ya kufunga maduka hayo ilitolewa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa misingi ya mUBAGUZI na kusababisha chuki kubwa miongoni mwa watendaji wa manispaa na wananchi.
“Mkurugenzi wa manispaa ni MBAGUZI, kwa muda mrefu sasa analalamikiwa kwa tabia hiyo, lakini bado anaendelea KULINDWA,” alisema Hijja na kuongeza kuwa “kama MNAMPENDA MCHUKUWENI AKAFANYE KAZI IKULU.”
Kauli ya Mwakilishi huyo iliungwa mkono na takriban wajumbe wengi ambao wamesema kuna tatizo kubwa ambao serikal imeshindwa kuchukua dhidi ya Mkurugenzi ambaye anaonekana kwamba utendaji wake una mshaka makubwa kiutendaji huku shutuma nyingi za rushwa zikielkezwa kwake kutokana na mikataba ya makampuni ya simu za mkononi.
Akichangia bajeti hiyo Mwakilishi wa Kikwajuni (CCM) Mohmoud Mohammed Mussa alisema kufunga maduka ya Darajani ni sawa na kusamehe mapato ya shilingi million 760 zinazokusanywa na serikali kutoka kwa wafanyabiashara wa eneo hilo kwa mwaka.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu alihoji wingi wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya baraza la manispaa wakati baraza hilo makusanyo yake anatosheleza bila ya kupewa fedha serikalini.
“Baraza la Manispaa linapewa ruzuku ya shilingi 1094 millioni kutoka katika mfuko wa serikali makusanyo yake ni 1041 millioni sasa kwa nini wapewe ruzuku wakati fedha wanazokusanya zinatosheleza katika kujiendesha” alihoji Jussa.
Jussa alisema mvujaji wa mapato unaofanywa na baraza la Manispaa hauwezi kufuta dhamira ya utendaji kazi wa serikali katika baraza hilo kwa kuwa wananchi wa Zanzibar wamepoteza imani ya baraza hilo hata kama kuna mipango mizuri ya kuimarisha utendaji kazi.
“Mheshimiwa Spika baraza hili tulitaka iiundwe tume kuchunguza tuhuma zinazotuhumiwa baraza la manispaa ikiwemo mikataba ya simu za mkononi na harufu ya rushwa lakini serikali ilikataa lakini leo tunashuhudia ripoti iliyotolewa ambayo moja kwa moja inaonesha kuna rushwa katika baraza hili, lakini waziri unatwambia kuwa baraza limetayarisha mipango mizuri” alisema na kuongeza kwamba.
“Kitendo kilichofanyika huko nyuma hakiwezi kufunikwa na hiyo mipango mizuri maana hakifunikiki, wananchi wamepoteza imani na baraza hili wasafishwe ndio wananchi wataunga mkono hiyo mipango mizuri” alisema Jussa na kuungwa mkono na wajumbe wenzake.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Micheweni (CUF) Subeit Khams Faki alisema manispaa inakabiliwa na tatizo la ubadhirifu kwa miaka mingi sasa, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa na serikali
“Ubadhirifu upo manispaa, wanaohusika hawachukuliwi hatua zozote, kuna tatizo gani tunashindwa kumwajibisha mtu anayeshindwa kuwajibika?,” alihoji Subeit.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Zanzibar, Rashid Ali Juma anatuhumiwa kwa kuitumbukiza serikali katika mkataba wenye utata na makampuni mawili ya simu za mkononi ambapo katika ripoti hiyo imemhusisha moja kwa moja Mkurugenzi huyo.
Wakati hayo yakitendekea kujadiliwa ndani ya baraza la wawakilishi huku nje tayari madiwani katika ripoti yao walitoa mapendekezo na kuitaka serikali imuondoshe Mkurugenzi huyo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kuingia mikataba kinyume na sheria, kutumia madaraka yake vibaya na kuacha mji wa zanzibar kuwa katika hali mbaya na uchafu kila mahali.

hili jama lishaiba sana sasa kama hamukulifunguliya mashataka na kuhukumiwa basi serekali ya GNU-SUKARI MUTAKUWA HAMUNA MAANA HATA PESA MBILI hawa ndio watu wanaoirudisha nyuma zenji na wako wengi sana kama hawa na nimpaka WASAFISHWE WOTE HAWA la sivyo itakuwa kama munampingia mbuzi gitaa munasubiri acheze na wala hachezi anaendeleya kula nyasi zake ndio hiyo RUSHWA linakula to mpaka limejisahau vipi mahakama iseme maduka yafunguliwe na yeye aseme hayafunguliwi hii peke yake ashavunja sheria alikuwa ashikwe na kushtakiwa kwa kufanya hivi ila ndio hivyo haguswi labda BABU yake ni moja ktk wale waliyoshirikiana na JOHN OKELLO KUIPINDUWA ZNZ NDIO MAANA SEREKALI INAMUOGOPA INAMUACHA AFANYE ANAVYOTAKA MAANA SEREKALI NI YAO SIO...?

No comments:

Post a Comment