Friday, July 8, 2011

WAZIRI ATOWA SIRI YA ID YA Z;BAR WAPEWA NCHI ZA KIGENI WAKATI MTOTO WAKE MWENYEWE HANA ID YA Z;BAR

elect1
Juzi mjumbe mmoja wa BLW alitoboa siri moja. Aliarifu BLW kuwa mtoto wake anayesoma Chuo Cha Afya, Mbweni,hana kitambulisho cha Mzanzibari ‘Mkaazi” (Zanzibar IDs); lakini rafiki yao mmoja Mzambia anacho kitambulisho hicho, na anapata fursa zote za kiraia kama Mzanzibari au Mtanzania.Aliyesema maneno haya ni mwakilishi wa CCM — chama tawala; ambayo kwa kiasi kikubwa ndio waliobuni mpango huu wa kuwaptaia vitambulisho hata wasiokuwa Raia wa z;bar ili ukija uchanguzi washinde 2015. kwa minajili ya kuwapigia kura wao CCM ili washinde (USHINDI LAZIMA)!
Mtoto wake mwakilishi huyo, ananyimwa mikopo, au huduma nyenginezo za lazima kama RAIA WA ZANZIBAR, lakini mgeni ana-enjoy kila kitu cha z;bar.
(nadhani uchaguzi ujao Mzambia huyu atagombe ama Urais au hata jimbo, na tutampa kura so long atavaa shati kijani na manjanona pakacha kichwani basi tutampa tu).
Hii ndio Zanzibar yetu ya leo. Tunatiana kamba shingoni wenyewe kwa wenyewe.
Mimi binafsi yangu ninawajua tour guide kwa mamia ambao wanafanya kazi hiyo bila hata ya kuwa ni Watanzania au Wazanzibari. SMZ imekaa kimya, na inawajua.
Kuna wageni kwa maelfu wanafanya kazi si mahoteleini tu, bali hata ofisi za SMZ.
Sasa, mimi nilitegemea baada ya mwakilishi huyu ‘kutumbua jipu’ na kutoa siri hiyo ‘sensitive’ ndani ya chombo cha kutunga sheria, kitachofuata ni ama Mkuu wa Vitambulisho kusimamishwa kazi na kupelekwa mahakama na kwa kuuza utaifa wa zanzibar, au wanaohusika kuchukuliwa hatua akiwemo Waziri anayehusika na kadhia hii.
Bahati mbaya sana, BLW imekuwa ni sehemu ya kupiga soga na paha paa chereko chereko na, kuchekeshana na kuuliza maswali hayo kwa hayo yasiyokuwa na mantiki yeyote au hata yanayoweza kuisadiai Zanzibar. Kwa mfano, juzi limeulizwa swali eti kwa nini Rais wa Jamhuri ya Muungano hana mamlaka ya kusamehe wafungwa wa Zanzibar. Kwa kumbukumbu zangu, swali hili linaulizwa kila mwaka, na kila kikao cha BLW. Kweli ofisi ya BLW haiwezi kuona na kuyatoa maswali ya kipuuzi kama haya.
Akina Jaku na sijui nani na nani, maswali yao na wengine ni ya ..kimaskhara maskhara tu, hata wao wenyewe wanapoulizia hawako serious, utaona wanacheka na thihaka kibao kama wako markite ya darajani vile BLW siku hizi ni kama malindi pwani pale gawira wa vibuwa asubuhi utasikia thihaka na vichekesho vya kila aina ndio BLW la sasa.
Jambo kama hili kubwa, mtu mgeni anapewa kitambulisho cha nchi….Nakumbuka david Blankett wa Uingereza, enzi zile alikuwa Home Affairs Minister, alijiuzulu kwa sababu ya kufanya ‘hisani’ ya kumsaidia mkimbizi/mgeni kutoka nadhani Balkan (Yugoslavia au sijui …). Hata na kesi nyengine kama hizi zipo nyingi tu.
Leo Mzawa Zanzibar ananyimwa haki yake ya kimsingi, then, mnasema na kuhubiri Utawala Bora, au haki na sheria.
Je, kama leo serikali ya Muungano, itaamua katiba mpya ipigiwe kura ya maoni, au muungano wazanzibar wanautaka au hawautaki upigiwe kura. lakini takriban 100,000 people wageni, lakini wanazo zanzibar ID na wazenji hawana ID sasa wageni watasema muungano udumu wazenji hawata piga kura maana hawana ID, mtasemaje? Na kweli idadi hiyo ndio ya wageni – na wote wanazo ID za Zanzibar. Zanzibar hatufiki milioni moja. Ile hesabu ya kuwa tupo 1.2 milioni, si kweli. Ni fake data statistics. Na ndio akina hao Mzambia, Mrwanda,M Burundi, Mkenya,mganda na watu wa muzambiqi n.k
ZANZIBAR IMEKWISHA NYERERE KAFANYA KAZI NZURI SANA KUUWA UTAIFA WA ZANZIBAR NA SISI TUMEKA TUNAKULA UROJO TU FORO.

No comments:

Post a Comment